Lissu Aleta Tabu | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Lissu Aleta Tabu

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by TandaleOne, Sep 7, 2010.

 1. TandaleOne

  TandaleOne JF-Expert Member

  #1
  Sep 7, 2010
  Joined: Sep 4, 2010
  Messages: 1,617
  Likes Received: 118
  Trophy Points: 160
  Lisu akoroga msafara wa Slaa
  Monday, 06 September 2010 20:13

  Salim Said, Singida


  MGOMBEA wa kiti cha ubunge wa Singida Mashariki kupitia tiketi ya Chadema, Tundu Lissu, amevuruga msafara wa mgombea urais wa chama hicho, Dk Willbrod Slaa, baada ya kumuamuru dereva wa gari lililokuwa limembeba mgombea urais, kuingia ghafla katika kituo cha mafuta cha Singida mjini jambo ambalo ni hatari.

  Tukio hilo la aina yake na ambalo liliwashangaza na kuaacha midomo wazi watu waliokuwa katika msafara huo, lilitokea saa 7:25 mchana wa juzi, wakati msafara wa Dk Slaa ukiwa njiani kuelekea katika Kata ya Iglansoni, ukitokea Kata ya Sepuka katika Wilaya mpya ya Ikungi, mkoani humo.


  Msafara huo ulikuwa na magari matano yaliyoongozana, mbele yakiongozwa na gari la polisi.


  Tukio hilo lilikuja baada Lissu kugundua kuwa gari la Dk Slaa, lilikuwa na upungufu wa mafuta na hivyo akaamua lipelekewe kwenye kituo cha mafuta, lakini bila kutoa taarifa kwa polisi na viongozi wengine.


  Baadhi watu, waliielezea kitendo hicho kuwa ni hatari na kwamba kilikuwa ni cha kuwadharau polisi waliokuwa wakiongoza msafara huo.


  Watu walioshuhudia tukio hilo, walisema kitendo hicho, kingeweza kusababisha ajali katika msafara huo.


  Mkurugenzi wa Ulinzi na Usalama wa Chadema Sabula, alikemea kitendo hicho na kutaka kusirudiwe tena kwa kuwa kinahatarisha maisha ya mgombea na watu wengine katika msafara.


  "Sasa umefanya nini Lissu, huwezi kuitoa gari ya mgombea katikati ya mwendo na kuiingiza sheli, wakati mbele tunaongozwa na polisi, ni hatari, kisijirudie tena kitu hicho," alisema Sabula kwa hasira.


  Baada ya kuingia katika kituo hicho cha mafuta, Lissu alishuka katika gari la mgombea na kwenda kwenye gari lake na kulipia mafuta.

  Baadaye, alipanda gari lake badala ya lile la mgombea kama ilivyokuwa kabla ya tukio hilo.

  Wakati hayo yakifanyika gari la polisi lililokuwa na askari sita wakiwemo wawili wenye silaha, lilikwenda kuegesha umbali wa mita 300, ili kusubiri msafara huo, uliokuwa umekatika.


  Katika tukio lingine, gari hilo la Dk Slaa lilipata pancha wakati likielekea katika mkutano uliopangwa kufanyika Iglansoni saa 9:00 alasiri.


  Hata hivyo, Dk Slaa alifaulishwa katika gari la Lissu ili awahi katika eneo la mkutano na kumwacha dereva na mlinzi mmoja wakibadilisha tairi.


  Source:Mwananchi
   
 2. Mtu wa Pwani

  Mtu wa Pwani JF-Expert Member

  #2
  Sep 7, 2010
  Joined: Dec 26, 2006
  Messages: 4,095
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 135
  ndo hao, basi hata protocol hamjui, nyny kweli mmejiandaa kushika dola ?

  Chadema ni watu wa maajabu, sawa ndio mnajifunza
   
 3. Baba_Enock

  Baba_Enock JF-Expert Member

  #3
  Sep 7, 2010
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 6,802
  Likes Received: 164
  Trophy Points: 160
  Kikwete amefaulishwa mara ngapi katika misafara akiwa Rais Wa JMT kutokana na matatizo ya magari?

  Kile kisa cha kuwekewa mafuta "yaliyochakachuliwa" kule Moshi kiliishia wapi vile?

  Give me a break! That is very low from Mwananchi (if at all that is the source)
   
 4. J

  JokaKuu Platinum Member

  #4
  Sep 7, 2010
  Joined: Jul 31, 2006
  Messages: 12,751
  Likes Received: 4,974
  Trophy Points: 280
  ..lingeishiwa mafuta njiani, mbali na vituo vya mafuta, ingekuwa lawama zaidi.

  ..zaidi, kwanini hakuna network ya mawasiliano kwenye magari yote yaliyoko ktk msafara?

  ..lazima gari analopanda Dr.Slaa liwe na mtu anayeweza kuwasiliana moja kwa moja na magari ya polisi yanayowaongoza.
   
 5. TandaleOne

  TandaleOne JF-Expert Member

  #5
  Sep 7, 2010
  Joined: Sep 4, 2010
  Messages: 1,617
  Likes Received: 118
  Trophy Points: 160
  Ur online.Check it
   
 6. Mtu wa Pwani

  Mtu wa Pwani JF-Expert Member

  #6
  Sep 7, 2010
  Joined: Dec 26, 2006
  Messages: 4,095
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 135

  hili ndilo la muhimu, hawa bwana hawajajipanga, unaona hata kwenye kampeni zao hawana strategies, tatizo si kutia mafuta tatizo gari ya mgombea kuitoa kwenye msafara bila ya mawasiliano, na hii ndio inazumziwa ni hatari, akipata ajali mseme imekuwa planned kumhujumu


  kwa hili wamekosea na nnaamini watajirekebisha bado wadogo na wachanga, na kwenye kupewa nchi ndio bado kabisa


  ila kidogo kidogo mtakuwa watani, ila mpunguze uhuni
   
 7. Tuko

  Tuko JF Bronze Member

  #7
  Sep 7, 2010
  Joined: Jul 29, 2010
  Messages: 11,186
  Likes Received: 397
  Trophy Points: 180
  TandaleOne, Mtu wa Pwani, Joka kuu... is this a story to discuss?!!!!!!!!! (Ndo maana nasema siku hizi CCM inaungwa mkono na vichwa maji...)
   
 8. J

  JokaKuu Platinum Member

  #8
  Sep 7, 2010
  Joined: Jul 31, 2006
  Messages: 12,751
  Likes Received: 4,974
  Trophy Points: 280
  Mtu wa Pwani,

  ..of course Chadema bado ni chama kichanga, inaeleweka kwamba hawana mapesa, na resources, kama walizonazo CCM.

  ..lakini hilo halina maana kwamba hawana uwezo wa kuongoza.

  ..kwenye nchi za wenzetu wagombea wote wa Uraisi hupatiwa ulinzi na serikali. pamoja na kutoa magari ya kuongoza msafara wa Chadema, Polisi walipaswa kutoa huduma ya mawasiliano ktk msafara huo.

  Tuko,

  ..binafsi sioni kama stori ina mtiririko au mantiki yoyote.

  ..lakini wakati mwingine ni lazima kujibu story kama hizi ili kuwekana sawa.
   
 9. Mwita Maranya

  Mwita Maranya JF-Expert Member

  #9
  Sep 7, 2010
  Joined: Jul 1, 2008
  Messages: 10,569
  Likes Received: 104
  Trophy Points: 145
  Hakuna sababu yoyote ya msingi kuwalaumu mwananchi,

  walichofanya wao ni kutuhabarisha kilichojiri kwenye msafara wa Dr. Slaa, sasa kama habari hiyo haikukupendeza hicho ni kitu kingine.

  Ni suala la kuzingatia utaratibu tu, kama alivyonukuliwa mkuu wa usalama bw. Sabula.

  Mwananchi hawawezi kubebeshwa lawama yoyote kwa huo mkasa. Kama umekereka sana muulize Tundu Lisu.
   
 10. TandaleOne

  TandaleOne JF-Expert Member

  #10
  Sep 7, 2010
  Joined: Sep 4, 2010
  Messages: 1,617
  Likes Received: 118
  Trophy Points: 160
  Hivi,maisha ya viongozi na familia zao ambayo Chadema wamekuwa mstari wa mbele kuyaongelea hapa JF si udaku??Au akija mtu mwingine akisema anakuwa kichwa maji??
   
 11. Bigirita

  Bigirita JF-Expert Member

  #11
  Sep 7, 2010
  Joined: Feb 12, 2007
  Messages: 13,976
  Likes Received: 688
  Trophy Points: 280
  wewe ndo umeishiwa kabisa! yani kutoa gari kwenye msafara ndo uchanga??? Mbayuwayu kashikishwa cheque imeandikwa laki tatu kwa maneno, na laki mbili kwa tarakimu, naye kakamatia ameduwaa like a mbayuwayu he is!!
   
 12. TandaleOne

  TandaleOne JF-Expert Member

  #12
  Sep 7, 2010
  Joined: Sep 4, 2010
  Messages: 1,617
  Likes Received: 118
  Trophy Points: 160
  Maneno yako yako kwenye taarabu.Ni mazuri.
   
 13. M

  Mwafrika JF-Expert Member

  #13
  Sep 7, 2010
  Joined: Nov 20, 2006
  Messages: 5,490
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 0
  madrassa al sul
   
 14. TandaleOne

  TandaleOne JF-Expert Member

  #14
  Sep 7, 2010
  Joined: Sep 4, 2010
  Messages: 1,617
  Likes Received: 118
  Trophy Points: 160
  Takwimu hazidanganyi:Wanafunzi wanaojiunga na vyuo vikuu vilivyopo nchini Tanzania waliongezeka kutoka 55,296 mwaka 2005/2006 hadi 118,000mwaka 2009/2010
   
 15. M

  Mwafrika JF-Expert Member

  #15
  Sep 7, 2010
  Joined: Nov 20, 2006
  Messages: 5,490
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 0
  madrassa al sul al jihad
   
 16. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #16
  Sep 7, 2010
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,236
  Likes Received: 308
  Trophy Points: 180
  Na je quality ya output hiyo unaisemeaje?
  Wait a minute: nadhani huko ulikotokea ni "the more you waffle the more you ean!...huh!
  Yani ukiposti pumba mingizaidi uko likely kupata MKOKO kama aliopewa Mume wa zamani wa Mama-Slaa!..huh!(Vigezo na Masharti kuzingatiwa!)
   
 17. TandaleOne

  TandaleOne JF-Expert Member

  #17
  Sep 7, 2010
  Joined: Sep 4, 2010
  Messages: 1,617
  Likes Received: 118
  Trophy Points: 160
  Is that how u get paid??Nahisi una uzoefu.Am a freethinker.What I see here from a person like u ni utoto.Mimi nimepost habari,cha msingi kama unaona haina umuhimu ni kuacha.
   
 18. omarilyas

  omarilyas JF-Expert Member

  #18
  Sep 7, 2010
  Joined: Jan 24, 2007
  Messages: 2,127
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Hivi Mwafrika umewahi kujiuliza hivi vibweka vyako vyenye elements za kebehi kwa imani za watu wengi humu zinasaidia ama kuathiri vipi maslahi ya chama ama mgombea wako/unayejinasabisha nae hasa wakati kama huu. Being sensitive to other people feelings and faiths is one of the most important political tool that you and some friends of yours need to learn and embrace...

  omarilyas
   
 19. Ndachuwa

  Ndachuwa JF-Expert Member

  #19
  Sep 7, 2010
  Joined: Mar 8, 2006
  Messages: 4,530
  Likes Received: 725
  Trophy Points: 280
  What is news behind this event of fueling Dr. Slaa's car?. Dr Slaa is not president yet so the issue of protocol do not apply at the moment
   
 20. TandaleOne

  TandaleOne JF-Expert Member

  #20
  Sep 7, 2010
  Joined: Sep 4, 2010
  Messages: 1,617
  Likes Received: 118
  Trophy Points: 160
  Some people still believe others cannot think.
   
Loading...