Yoda
JF-Expert Member
- Jul 22, 2018
- 37,597
- 46,204
Wiki hii zaidi ya takribani watu 20 wamepoteza maisha kwa mpigo katika ajali ya barabarani, hii imekuwa habari kubwa na kufika kwenye vyombo vingi vya habari kwa sababu watu hawa wamefariki kwa mpigo ila huwezi kukosa watu wengi kadhaa waliopoteza maisha kwenye ajali za barabarani hasa barabara kuu.
Matukio ya aina hii sio ya nadra nchini, watu wengi wamepoteza maisha kupata ulemavu kwa ajali za aina hii. Mengi yamefanywa na serikali ikiwemo kuweka speed limit za km 50, matuta, matrafiki wengi barabarani, operations za ukaguzi wa magari n.k .
Haya yote ni sawa ila ukweli ni kwamba barabara za single road ni changamoto kubwa sana kwa safari ndefu za mkoa kwa mikoa au wilaya kwa wilaya.
Kuna wakati gari ni lazima zifanye overtaking, kuna wakati lazima zikwepe muendesha bodaboda, mtembea kwa miguu au mifugo kwa ghafla. Kwenye barabara za single road haya yote hatari kwa sababu kosa au tatizo dogo litakolomfanya dereva atoke upande wake linaweza kuwenda kusababisha ajali kubwa kwa gari ambako liko upande wake sahihi.
Kwenye barabara za double road dereva anakuwa na nafasi kubwa ya kuweza kurekebesha makosa au kuhimili gari katika matukio ya ghafla bila kuleta madhara makubwa kwa abiria na magari mengine.
Pia mwendo wa km 50 kwa sasa kwenye safari ndefu unamchosha dereva na abiria kwa ujumla, ni vigumu sana kuuzingatia.
Serikali sasa inapaswa ije na mkakati wa kuzifanya barabara kuu zote za mikoani na wilayani double roads tena zenye kutenganishwa katikati kwa vizuizi vya blocks.