Elections 2010 Lisa M Rockerffeller urge Tanzanians to reject Kikwete a 2nd Term

Status
Not open for further replies.

- Unajua mimi kujadili haya ni sawa na kujadili mambo ya Slaa na mke wa watu, siwezi kwenda that low maana haina faida yoyote wka taifa langu, pole sana bro sitajadili this great thinking zako za mitaani mitaani, hapa ni Great Thinkers tunajadili mustakabali wa taifa!

William.

Mkuu Kama Ishu ya Slaa na Mke wa Watu ndiyo iliyopelekea ( Kwa mujibu wa Greta Thinker wewe) Wamama wajifungulie Chini, watoto wasome chini ya Miti, Watu waishi katika Lindi la Umaskini huku Vigogo na Watoto wao wakikonga Raha katika nchi ya akina Lisa, Vigogo na watoto wao wakisoma na Kutibiwa katika nchi ya akina Lisa basi huna Budi Kuijadili. Lisa anazungumzia mambo ya Msingi ambayo hata sisi kila siku tunalia juu yake, Ubadhirifu uliokithiri wa Viongozi wetu walioamua kujikatia sehemu kubwa ya Keki ya Taifa na Kuitumbua wao pamoja na watoto wao na Vimada wao ( Wengine wanaishi katika Nchi ya Lisa)
 
- Hao wazungu wangetuachia mambo yetu ya ndani tutayaamua wenyewe, wao wazungu mabaya waliyotufanyia Africa sio madogo eti, huyu mdada anasahau kwamba ni wizi wa familia yake kwa taifa lake ndio uliopelekea kuanzishwa kwa sheria ya Standard Act, ili kuzuia monopoly za wizi wa familia yake kwa wananchi wa US, sasa kama yeye ni mkweli angeanza kuwarudishia serikali ya US na wananchi wake hela walizoiba huko mpaka kuanzishiwa sheria.

- Africa bwana tunakuaga so desparate na ushindi wa uongozi kwamba hata huwa hatuulizi maswali magumu, halafu baadaye ndio tutakuja kuanza kutafutana uchawi, huyu dada hana moral authority yoyote ya kutufundisha wa-Tanzania kuhusu uzuri na ubaya wa viongozi wetu, kwa sababu tunayajua vizuri matatizo yetu, yeye na familia yake warudishe zile hela zote walizowabia wananchi wenzao huko US through biashara zao za mafuta na ngano!

Ahsanteni.

William.

Mkuuu Asssumme Kwa msisisitozo nasema assume JK kashinda Uchaguzi .Assume tena wewe kama mtu wake wa karibu anakuuliza ebu nishauri nimabie ukweli udhaifu wa serikali yangu iliyopita na udhaifu wa utendaji wangu ulikuwa ni upi ili nirekebishe mambo ? Utamjibu nini ?
 
Familia ya Rockfeller wapo huru hapa Marekani mbali ya pesa zao, walikuwa Magavana, na bado wana Seneta kule Western Virginia. Na kama tungependa kuchunguza familia sijui kama na wewe ungekuwa na haki ya kuzungumza. Wale walioko kwenye nyumba za glasi ni bora wasiwe wa kwanza kutupa mawe. Mimi hapa Marekani ninasomea mambo hayo ya madini juu ya tunavyonyonywa sasa nikimsikia Kikwete na Ngeleja wanasema eti sheria mpya walioitunga ni nzuri inanisikitisha sana. Hata alivyosema hivyo jana Jaji Bomani alibakia kinywa wazi.
YouTube - JK akizungumzia suala la Madini Michuzi Jr

- Familia ya huyu dada ni ya wezi period ndio maana wakatungiwa Anti Trust Act na shirika lao la Standard Oil kuvunjwa, sasa hivi wamebakishiwa Chase Bank tu, sasa mkoloni kutoka hiyo familia hawezi kunisaidia kujua kiongozi gani ananifaa Africa,

- Again hapa tunaongelea taifa kama unajua wizi wa familia yangu unaweza kuuweka hapa au ukaufungulia topic yake, maana hapa tunajadili mkoloni anayetaka kutuamilia kiongozi wetu awe nani!

William.
 
The Rockfeller family is very influential in all american circles, be it in government or civil organizations; if Lisa Rockfeller has discovered that Kikwete is the protector of corruption kingpins in Tanzania then believe me word will spread across all influential foundations and the U.S govt [ if it hasn't already] that Kikwete is not different from Mobutu and funds from America will dry up!! If the funds dry up then all the promises he has made on the campaign trail will go up in smoke!! Tutakuwa tumeliwa tena na mkwere na genge lake.

Tena mimi nitamwandikia huo dada afanye kampeni ya kukata misaada Tanzania mpaka CCM ing'oke maana ndo inayowatia kichwa na kuwa na akili mgando ya kushindwa kufikiria mipango madhubuti ya kuinua uchumi.
 
- Familia ya huyu dada ni ya wezi period ndio maana wakatungiwa Anti Trust Act na shirika lao la Standard Oil kuvunjwa, sasa hivi wamebakishiwa Chase Bank tu, sasa mkoloni kutoka hiyo familia hawezi kunisaidia kujua kiongozi gani ananifaa Africa,

- Again hapa tunaongelea taifa kama unajua wizi wa familia yangu unaweza kuuweka hapa au ukaufungulia topic yake, maana hapa tunajadili mkoloni anayetaka kutuamilia kiongozi wetu awe nani!

William.

Huyu William Mbabaishaji tu, Green Card Yenyewe apate wapi. Huyu anatetea Kikwete na hataki kutoka Marekani, usituzingue wwe
 
China hawatoi msaada kwa Marekani bali wananunua bonds ambazo wanajua hapo baadae watafaidika. Ni uamuzi wa kibiashara. Sisi tunaochangiwa ili tuweze kunua vyandarua ndio wenye matatizo. Kama hatuoni shida kodi za wananchi wao zinapogharamia sehemu kubwa ya bajeti basi hivyo hivyo inatubidi tukubali wanapotu-criticize. Hatukutakiwa kuwa hapa tulipo miaka 50 baada ya uhuru!

Amandla.......
 
Mkuuu Asssumme Kwa msisisitozo nasema assume JK kashinda Uchaguzi .Assume tena wewe kama mtu wake wa karibu anakuuliza ebu nishauri nimabie ukweli udhaifu wa serikali yangu iliyopita na udhaifu wa utendaji wangu ulikuwa ni upi ili nirekebishe mambo ? Utamjibu nini ?

- Nitamueleza kama ambavyo nimemueleza mara nyingi kwamba, bado tuna udhaifu wa kusimamia sheria tukiweza kusimamia sheria basio mengine yote yatajinyoosha yenyewe, tatizo letu kubwa ni kutoheshimu sheria zetu wenyewe.

william.
 
Huyu William Mbabaishaji tu, Green Card Yenyewe apate wapi. Huyu anatetea Kikwete na hataki kutoka Marekani, usituzingue wwe

Mkuu Usijali sana maana Kesho Mustakabali wa nchi hii unarejeshwa Mikononi mwa Wananchi!

Tanzania will never be the same, watu wanataka amabadiliko na Safari ya Mabadiliko ndio imeshaanza ila Masultani hawaipendi
 
China hawatoi msaada kwa Marekani bali wananunua bonds ambazo wanajua hapo baadae watafaidika. Ni uamuzi wa kibiashara. Sisi tunaochangiwa ili tuweze kunua vyandarua ndio wenye matatizo. Kama hatuoni shida kodi za wananchi wao zinapogharamia sehemu kubwa ya bajeti basi hivyo hivyo inatubidi tukubali wanapotu-criticize. Hatukutakiwa kuwa hapa tulipo miaka 50 baada ya uhuru!

Amandla.......

- Kutu-criticize ni one thing na kutuambia nani anafaa na nani hafai kuwa kiongozi wetu ni totally another story, ninaktaa mkoloni kutuambia nani hafai na nani anafaa kua kiongozi wetu, sijakaataa kuwa criticized!

william.
 
- Siwezi kujadili hoja za Mzungu kunifundisha nani ananifaa kua kiongozi wangu Africa, ndio maana tulimfukuza bila ya yeye kupenda huku Africa Ni ili tuwe huru na tuamue mambo yetu wenyewe, kama tutaenda kumuomba msaada ni uamuzi wetu sio wake!

William.

Tuache kupotosha tuliwafukuza lini kwa vita ipi? UMESAHAU KUWA TULIPEWA UHURU UN?tena kwa kiherehere chetu? wakati mwingereza alipewa atuangalie tu tukiwa na uwezo ndio atukabidhi nchi yetu?
 
- Familia ya huyu dada ni ya wezi period ndio maana wakatungiwa Anti Trust Act na shirika lao la Standard Oil kuvunjwa, sasa hivi wamebakishiwa Chase Bank tu, sasa mkoloni kutoka hiyo familia hawezi kunisaidia kujua kiongozi gani ananifaa Africa,

- Again hapa tunaongelea taifa kama unajua wizi wa familia yangu unaweza kuuweka hapa au ukaufungulia topic yake, maana hapa tunajadili mkoloni anayetaka kutuamilia kiongozi wetu awe nani!

William.

Jamaa anajipendekeza kwa JK labda atampatia kitengo baada ya baba mtu kutoswa!!
 
Mimi naona tatizo letu ni kutokubali ukweli.Ukweli ni kuwa kikwete ameshindwa kusimamia rasilimali za taifa hili,amekumbatia mafisadi na ameshindwa kusimamia uwajibikaji katika utumishi wa umma.Huyu dada hajasema jipya hapo,Watanzania kwa mamilioni tulishaona hayo na tulishaamua hatutampa 2nd term huyu bwana!Whats the hussle?
 
Tuache kupotosha tuliwafukuza lini kwa vita ipi? UMESAHAU KUWA TULIPEWA UHURU UN?tena kwa kiherehere chetu? wakati mwingereza alipewa atuangalie tu tukiwa na uwezo ndio atukabidhi nchi yetu?

- Historia iko wazi kwamba hawakutaka kuondoka, ndio maana Mwalimu alienda UN kuwafukuza waondoke na waliondoka na tukawa huru!

William.
 
- Nitamueleza kama ambavyo nimemueleza mara nyingi kwamba, bado tuna udhaifu wa kusimamia sheria tukiweza kusimamia sheria basio mengine yote yatajinyoosha yenyewe, tatizo letu kubwa ni kutoheshimu sheria zetu wenyewe.

william.

Na wa kwanza kuonyesha kuwa anataii sheria wanatakiwa kuwa viongozi. Kama mwenyekiti wa chama JK hajachukua full resposibility. Mfan wamemzuaia bashe na mwakalebela bila tuhuma zao kuthibitishwa b na vyombo husika lakini wameruhusu Mramba na Chenge waendelee kugombea kwa kisingizio vyombo husika bado havijawaona na makosa.

Kama mwenyekiti wa chama ameshindwa kuwaweka pembeni baadhi ya wale wanaotuhumiwa wakati huo huo akawatosa baadhi. Huoni kuwa kiongozi mwenyewe ndo tatizo na sio sheria.
 
Tusisahau kupiga kura kesho na Kuhamasisha Waliolala

Saa ya Mabadiliko ni sasa
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom