mkalamo
JF-Expert Member
- Sep 7, 2013
- 343
- 359
Nimefuatilia kwa ukaribu harakati za uchaguzi wa Kinondoni na Siha,huko kote vyama vya Chadema na CUF wameweka wagombea,ingawa nguvu Kubwa inaelekezwa Kinondoni.
Majimbo yote mawili yanafanya uchaguzi baada ya wabunge wa chadema na CUF kusaliti/kudharau uaminifu waliopewa na wananchi na kukimbilia CCM ambapo wamerudishwa kuwapigia magoti wananchi waliowasaliti.
Hii kwangu si hoja katika hili ninalokusudia kuliangazia
Hoja yangu ipo hapa katika mzozo wa chama cha CUF unaoendelea sasa
Ni wazi kila mmoja kwa upande wake ama anaitakia CUF mema au kujionesha kuitakia mema katika macho ya watu huku mioyoni mwao wakiwa ni wenye dhamira ya kukiangamiza chama hicho.
Kiuhalisia ugomvi wao kwa namna yoyote haupaswi kuiathiri CUF na ni wajibu wa kila mmoja kuipigania CUF nje ya mgogoro ili watakapomaliza makando kando yao yule atakayeshinda aikute CUF bado ni imara
TUNAPIMAJE DHAMIRA HIYO SASA?
Uchaguzi wa Kinondoni,CUF upande wa Maalim haukuweka mgombea na haukuwa na nia ya kuweka mgombea kwa mujibu wa taarifa ya mwenyekiti wa kamati ya Mpito,Mtatiro ni kuwa kwa umoja wao wa UKAWA wangeusia uchaguzi
Kamati Kuu ya Chadema ikabadilisha uamuzi wake bila kushirikisha upande wa CUF Maalim na kuamua kuwa na mgombea
CUF ya Lipumba nayo ikaweka mgombea wa Ubunge Kinondoni kama ilivyo Chadema
Nje ya migogoro yao Lipumba,Seif na Mtatiro pamoja na wafuasi wao wataendelea kuwa CUF
Katika mazingira hayo ndiyo mashirikiano ya kupigania CUF ya ndani yanapohitajika
Chadema imebeba udhaifu huo kuutangazia umma kuwa mgombea wao anaungwa mkono na CUF ya Maalim pamoja na Mtatiro na kumuita mgombea wa CUF ni kibaraka wa CCM.
Mtatiro na Maalim wamekaa kimya juu ya hilo na kutoa fursa kwa chadema kuuaminisha umma kuwa mgombea wa CUF ni kibaraka wa CCM
Tujaalie sasa mgombea wa CUF ya Lipumba ameshinda Kinondoni,na mahakamani Upande wa Maalim ukashinda na kutambuliwa kuwa ni uongozi wenye mamlaka ya kutomtambua Lipumba.
Katika mazingira hayo kama mgombea wa CUF atashinda Kinondoni Maalim na Mtatiro watakipokea chama kikiwa na mbunge ambaye ni kibaraka wa CCM kwa mujibu wa Chadema na ukimya wa upande wa Maalim
Na kama Mtatiro na Seif upande wao utashinda na kisha wagombea Ubunge wa sasa katika jimbo la Kinondoni na Siha wakawa wameshindwa ina maana Maalim na Mtatiro ukimya wao utakuwa umechangia kuidhoofisha CUF na wao watapokea CUF iliyo dhaifu
Katika mazingira hayo ndipo unaweza kujiuliza ni nani msaliti halisi wa CUF?
Nakaribisha mjadala kutoka kwa waungwana