Lipumba ndiye mwenye afadhali UKAWA

Lipumba ndiye mwenye afadhali UKAWA

baadh ya wanachama wa CHADEMA hawatak kabisg kusiki jina la LIPUMBA sijajua tatizo ninin?

sio hawataki jina la lipumba,UKAWA wamekubaliana chama kilichokua na mgombea mwenye kura nyingi 2010 ndicho kitatoa mgombea.lakini pia bado hawajaanza harakati za kumpata.kila watu wana mfumo wao ,ukawa hawafanyi kwa kuiga ccm
 
Hawa ukawa wanapoteza muda tu kujifurshisha hamna lolote jipya
 
Slaa asijaribu atakufa kama watabiri walivyo tabiri.
 
CCM Mnahangaika Mpaka Mnaingia Kupendekeza Majina Ya Wagombea Wa Upinzani?Mtaisoma Mwaka Huu!Kwa Mtazamo Huu Tunaikwamisha Katiba Inayopendekezw,
 
mkuu kavulata jikite kutafuta mgombea atakayepeperusha bendera ya chama chenu, achana na UKAWA...hawakuhusu.
 
Last edited by a moderator:
Tatizo kubwa la wapinzani nchini wanahangaika zaidi na yanayotokea ndani ya CCM badala ya kuhangaika na mambo ya wananchi na yale yaliyoko ndani ya vyama vyao vya upinzani. Wapinzani wanajadili waliotangaza nia CCM badala ya kuanza mapema kuongelea nani anafaa kuwa mgombea wao 2015 dhidi ya mgombea atakaeteuliwa na CCM (Lowassa? Sitta? Membe? Pinda? Mwigullu? Sumaye? Wassira? Makamba? Nyarandu? Kigwangala?, Migiro? Makinda? au.....?). Ni vema hata vyama vya upinzani kuanza kujitokeza kutangaza nia ili watu waanze kuwajadili kidogokidogo.

Upinzani ina Professor LImbumba hadi sasa ambaye ana haiba ya kugombea urais 2015. Lipumba hana kashifa yoyote mbaya kwenye jamii itakayoweza kutumiwa na wagombea wengine kumpinga. Lipumba hana tamaa, hana ukabila wala udini ni mwislamu wa kawaida tu anayemcha mungu, ni msomi na mchumi, na hajawahi kunyang'anya mke wa mtu.

Kama UKAWA ikimuandaa vizuri Lipumba, kumpamba na kumuunga mkono kwa hali na mali anaweza kushindana na mgombea yeyote kutoka CCM.

huna akili wewe kwani kujitangaza mapema ni sifa?tumia akili usikurupuke
 
Umelewa na kichapo cha selikali za mitaa?mtafuteni makonda aje awasaidie kuwaambia nini mpost mme wako mwenye anajua.
 
nimetaja sifa za lipumba, taja sifa za slaa kama kweli unataka kuisaidia ukawa. Hatusemi dkt. Slaa hafai ila tunataka anayefaa zaidi kwa kupitia mijadala kama hii. Tunajenga nyumba moja haifai kugombea fito.

hatusemi dokta profesooor kanali baba riz
 
Hiviii yule M/KITI feki wa CCM aliyejipachika UENYEKITI FEKI wa KATA PALE UBUNGO na baadae akaambulia kipigo cha MMBWA MWIZI na kuokoa maisha yake kwa kutumbukia mtaroni je aliishia wapi?? aliupata huo uenyekiti au ndo aliambulia kichapo?
 
Angalia hii video halafu ndo urudi hapa na hizi porojo zako
m.youtube.com/watch?v=ujwfFUUAD70

Nimeiangalia video kama ulivyoagiza sikuona kitu kipya. Issue kubwa kwenye video yako hii ni suala la mahakama ya Kadhi kwa waislamu. Swala hili wala sio la Lipumba pekee bali liko kwenye sera na irani za chaguzi za vyama vya siasa pia. Hata wagombea wakristo walishawahi kuwaahidi waislamu kuwapatia mahakama hii ya Kadhi kama wakishinda urais. Suala la kadhi linakuzwa kupita kiasi bila ya sababu za msingi. Nijuavyo mimi hata kama waislamu wakipewa mahakama ya kadhi kikatiba hakuna jipya litakalotokea kwa waislamu wala kwa wenzao wakristo, kwani mahakama hizi ziko katika nchi nyingi hata zile zinazotuzunguuka na hata za ulaya. Dunia ya leo hata waislamu wenyewe watakataa kuhukumiwa kiislamu na mahakama hizi, maana hata waislamu wetu vijana kwa wakubwa, viongozi na wafuasi wao, wengi wao ni wazinifu, wala rushwa wakubwa, wakwepa kodi, wanywa pombe, na kufanya makosa menginge yanayokatazwa na uislamu. Hivyo hata mahakama ya kadhi ikiwepo itabakia tu kama white elephant ndani ya jamii, itapata wateja wachache sana wanaohitaji masuala ya mirathi na talaka tu. Lakini kwakuwa wapo wachache wanaoidai kunadhambi gani wakapewa ili kupunguza joto? Hiyo haiwezi kumtia doa Professor Lipumba kwani hata yeye anahitaji kura za watu wote hata wale wanaohitaji mahakama ya kadhi. Hata CCM ilifanya hivyo kwenye irani yake ya uchaguzi ya mwaka 2005 ili kuvutia kura za wapenda mahakama ya kadhi. Hata Mrema na wengine walishawahi kuahidi mahakama ya kadhi waislamu ingawa yeye ni Mkristo. Ukawa haihitaji kusimamisha mgombea ambaye hataki kura za wananchi wanaohitaji kupewa mahakama ya kadhi, maana hatujui UKAWA itakosa kura ngapi kwasababu ya puuzi kama huo. Tafuteni mgombea ambaye anaweza pia wa kwenda kuomba kura hata kwa Kadinali Pengo, kwa askofu Malasusa, Kwa askofu Mokiwa, kwa Lusekelo, kwa Rwakatare, kwa Mufti sheikh Idd Simba, na kwa sheikh Issa Ponda na wafuasi wao. Huyo ndiye mgombea atakayewafaa nyie 2015. nakushanga ww unavyoshangaa kuona Lipumba kavaa kanzu na kwenda kuomba kura za watu wanaotaka mahakama ya kadhi kitu ambacho hata CCM wanakifanya. Wewe siasa hujui (ni pandikizi ndani ya UKAWA) kaa kando vinginevyo utaifanya safari yenu ya kwenda Ikulu iwe ndefu na ngumu sana.

Ndiyo maana Bado nasisitiza kuwa kwa hali ya sasa ndani ya UKAWA ilivyo Professor Lipumba hana mpinzani. Tomasa watu wote ndani ya UKAWA kuanzia kushoto hadi kulia na juu hadi chini utakuta ni Lipumba amewazidi wenzie kisifa, anakubalika kwa makundi yote ya wasomi, wana-uchumi, waadilifu, waislamu, wakristo hapa nchini na hata nje ya nchi. Huu sio ushabiki wa kijinga kama wengine wanavyodhani, vinginevyo labda msubiri akina Mwigulu watakaotemwa kwenye mchujo wa CCM hapo baadaye.
 
mkuu kavulata jikite kutafuta mgombea atakayepeperusha bendera ya chama chenu, achana na UKAWA...hawakuhusu.

Maajabu! Wasishinde CUF wanaoshida Zanzibar mshinde nyie msioshinda Tanganyika?
 
dah mkubwa umeona mbali sana kwa hili nakubali kwa% kwasababu ukawa walau nayo iweze kuweka upinzani wa kutosha hawanabudi kumpitisha prof ;slaa bado kiwango ca siasa ni ndogo sana pia anatukanika na anakashifika tofauti na ibrahm hana kashfa,ana haiba ya urais,taaluma ya ufumbuzi wa tatizo hasa ujengaji wa hoja lakini ukawa itakuwa haija fanya kitu kama itamsimika huyo fundi wa matusi na mwenye tetesi za ukabila na mdini japo hakuna uhakika basi ccm itashinda kwa wastani wa 73%
 
dah mkubwa umeona mbali sana kwa hili nakubali kwa% kwasababu ukawa walau nayo iweze kuweka upinzani wa kutosha hawanabudi kumpitisha prof ;slaa bado kiwango ca siasa ni ndogo sana pia anatukanika na anakashifika tofauti na ibrahm hana kashfa,ana haiba ya urais,taaluma ya ufumbuzi wa tatizo hasa ujengaji wa hoja lakini ukawa itakuwa haija fanya kitu kama itamsimika huyo fundi wa matusi na mwenye tetesi za ukabila na mdini japo hakuna uhakika basi ccm itashinda kwa wastani wa 73%

Hebu tuwape ushauri wa bure UKAWA, ingawa sio lazima waufuate. Lazima wafahamu kuwa ndani ya UKAWA wamo mamluki weengi watakaofanya kazi ya kuwapotosha. Gogolo la uteuzi litabutuka muda mfupi kabla ya uchaguzi, heri litokee sasa ili wawe na muda wa kulishuhulikia. Dkt. Slaa ni mtu makini sana anayefaa nafasi ya uwaziri mkuu, Mbatia waziri wa elimu, Mbowe waziri wa mambo ya ndani, Mtatiro wizara ya ujenzi, Zitto waziri wa fedha, Mnyika waziri wa ulinzi, Tundu Lissu makamu wa Rais/Sheria na Katiba, Mdee Ardhi, Selasini maliasili, n.k. Tena UKAWA mkishinda tangazeni kuchukua watu chapa kazi hata kutoka CCM kwenye baraza lenu la mawaziri kwa lengo la kuharakisha maendeleo ya wananchi.
 
Risi wa kweli huwa anaombwa na chama chake sio unaomba mwenyewe tena kwa kuhonga n.k. Kiongozi wa kweli alazimishi uongozi maana yeye hajijui watu ndio wanajua unafaa au laaa.
 
Uongozi sio elimu kubwa,umbo kubwa au kuongea sana,uongozi ni karama ( kipaji) .
 
huna akili wewe kwani kujitangaza mapema ni sifa?tumia akili usikurupuke

ukijitangaza mapema wananchi watakisaidia chama katika kufanya uteuzi wake wa mwisho. Wananchi wanazo sifa na kashfa za kila mwananchi hapa nchini, kama aliyejitangaza ni mtembea na wake za watu watakujulisha tu. Lakini pia wananchi wanazifahamu hata afya za watu kama aliyejitangaza ana tatizo la kifafa, pressure, kisukari, busha, mtindio wa ubongo wananchi wanaomfahamu watasaidia chama katika uteuzi wa mgombea wao. Kwakufanya hivyo chama kitaepuka kuteua mgombea mgonjwa ambaye hataweza kuzunguuka nchi nzima kufanya kampeni.
 
mkuu kavulata jikite kutafuta mgombea atakayepeperusha bendera ya chama chenu, achana na UKAWA...hawakuhusu.

Hakuna rais wa UKAWA kuna Rais wa Tanzania, rais wa UKAWA watu watamkataa tu. Watanzania wanaokubalika kwa dini zote wapo, wanaokubalika kwa makabila yote wapo, wanaoweza kudumisha muungano wapo, wenye majibu ya uchumi na wanaokerwa na hali za maisha za watu wetu wapo, wanaokubalika kitaifa na kimataifa pia wapo. Muhimu ni kuwa makini katika kuwagundua na kuwapa nafasi. Usilete ukanda kwenye mambo ya msingi.
 
Uongozi sio elimu kubwa,umbo kubwa au kuongea sana,uongozi ni karama ( kipaji) .

Tooba! Chief Mangungo aliuza nchi yake ya Msovero kwa akina Karl Peters kwa kukosa elimu, unataka kuturejesha huko?
 
Back
Top Bottom