Lipumba ndiye mwenye afadhali UKAWA

Lipumba ndiye mwenye afadhali UKAWA

Naamini hata UKAWA wenyewe wanajua wanachokifanya ndani ya umoja wao, sina hakika kama hawana kabisa ajenda za nani agombee nafasi hizo. Hebu tuwe na subira tukiwa na imani kwamba viongozi wengi ndani ya vyama vya UKAWA wana uzoefu wa kutosha sana na siasa za hii nchi na wengine ni wasomi, yaani ni maprofesa wa kitanzania, siyo wa kichina, katika mambo ya siasa na mambo mengine mbalimbali.

Nafikiri UKAWA wanaongozwa na nidhamu katika kutangaza nia ya kugombea nafasi mbali mbali za uongozi, na hasa katika taasisi kubwa kabisa ya urais, siyo kama CCM ambayo kila anayejisikia (awe na kashifa za ufisadi, wizi n.k) akijisikia tu anatangaza kuwania nafasi hiyo ambayo kiukweli inastahili kupewa heshima kubwa na anayetangaza nia basi walau afanane kweli na hiyo nafasi.

Ni vizuri umetoa maoni yako na mtazamo wako juu ya Prof. Lipumba, naamini watakaohusika katika uteuzi wa mgombea wa urais watazingatia pia maoni yako katika uteuzi wao.

Au mnasubiri watakaomeguka kutoka CCM? Kufanya hivyo itakuwa hatari kwa UKAWA.
 
Bwiru boy, I like your diplomatic way of answering.
 
UKAWA haichaguliw mgombea na gamba bali wanaUKAWA wenyewe ndiyo watachagua anayewafaa iwe Slaa, Lipumba, Mbowe ni sawa tu.OVER

#GOODMORNING
 
ukawa wasipochanga karata zao vizuri bado watausikia urais kwenye redio tu.
watanzania hatutachagua rais kisa tu katoka ukawa bali rais bora.
kukiwa na rais bora kutoka ccm na ukawa basi ukawa watapata kura yangu,
lakini rais kutoka ccm akiwa bora (mf. Sita) na ukawa wakiwa na rais bogus basi ukawa wausahau kabisa ushindi.

Tatizo kubwa la wapinzani nchini wanahangaika zaidi na yanayotokea ndani ya CCM badala ya kuhangaika na mambo ya wananchi na yale yaliyoko ndani ya vyama vyao vya upinzani. Wapinzani wanajadili waliotangaza nia CCM badala ya kuanza mapema kuongelea nani anafaa kuwa mgombea wao 2015 dhidi ya mgombea atakaeteuliwa na CCM (Lowassa? Sitta? Membe? Pinda? Mwigullu? Sumaye? Wassira? Makamba? Nyarandu? Kigwangala?, Migiro? Makinda? au.....?). Ni vema hata vyama vya upinzani kuanza kujitokeza kutangaza nia ili watu waanze kuwajadili kidogokidogo.

Upinzani ina Professor LImbumba hadi sasa ambaye ana haiba ya kugombea urais 2015. Lipumba hana kashifa yoyote mbaya kwenye jamii itakayoweza kutumiwa na wagombea wengine kumpinga. Lipumba hana tamaa, hana ukabila wala udini ni mwislamu wa kawaida tu anayemcha mungu, ni msomi na mchumi, na hajawahi kunyang'anya mke wa mtu.

Kama UKAWA ikimuandaa vizuri Lipumba, kumpamba na kumuunga mkono kwa hali na mali anaweza kushindana na mgombea yeyote kutoka CCM.
 
Mleta mada anataka kuleta janja ya nyani,anyway, ni uhuru wake wa kidemokrasia na tunauheshimu.Kikubwa,UKAWA km ilivyo ccm na wengine,kila mmoja ana TARATIBU ZAKE PALE MUDA SAHIHI KWAKE UNAPOWADIA.So,kawaambie hao wanaotaka kujua UKAWA pakoje kwa sasa,Waambie tu hapaingiliki,hapavurugiki,wapo makini na vipaumbele walivyonavyo!Mnaweza kumtaja yeyote,ila wenye kuchagua ni sisi UKAWA,Nyie kaendeleeni kujichimbia Kaburi kwani April kwenye Katiba Inayopendekezwa tunawafuta ktk ramani ya siasa.Ombeni ushauri kwa KANU namna ya kuzoea kuwa wafu!
 
maccm kila anaejisikia kutangaza nia ana tangaza,na akishatangaza nia wanaanza kutukanana mfano wengine wanashutumiana kwa ufisadi waziwazi ,na endapo hawatamchagua lowassa ccm inakufa,na endapo mtamchagua lowassa ccm inakufa.hahahaha patamu hapo yetu macho
 
Nyie maCCM hii mbinu yenu yakutaka kuivuruga UKAWA haitofanikiwa kamwe! Iko hivi viongozi wa UKAWA wote wako makini na yeyote atakayepeperusha bendera ya UKAWA tutamfia.
 
Mleta mada anataka kuleta janja ya nyani,anyway, ni uhuru wake wa kidemokrasia na tunauheshimu.Kikubwa,UKAWA km ilivyo ccm na wengine,kila mmoja ana TARATIBU ZAKE PALE MUDA SAHIHI KWAKE UNAPOWADIA.So,kawaambie hao wanaotaka kujua UKAWA pakoje kwa sasa,Waambie tu hapaingiliki,hapavurugiki,wapo makini na vipaumbele walivyonavyo!Mnaweza kumtaja yeyote,ila wenye kuchagua ni sisi UKAWA,Nyie kaendeleeni kujichimbia Kaburi kwani April kwenye Katiba Inayopendekezwa tunawafuta ktk ramani ya siasa.Ombeni ushauri kwa KANU namna ya kuzoea kuwa wafu!

Watakaomchagua rais ni wananchi wote sio UKAWA, mgombea hawezi kuwa siri ya UKAWA tu hata kidogo, wananchi wanaishi na wagombea, wanawafahamu uzuri na ubaya wa kila mwananchi, walete kwao mapema wagombea ili wakuelezeni uzuri na ubaya wao ili iwasaidieni katika kufanya maamuzi.
 
Si kweli,km ndivyo basi hamna haja ya uchaguzi,wananchi WOTE waseme tu kuwa tunamtaka rais toka UKAWA.
Wapo watakaompigia mgombea wa CCM,UKAWA,ACT,ADC,TLP,CHAUMA, nk.Muda Sahihi kwetu Bado,na sio SIRI,muda ukifika wananchi watamfahamu!Hatuwezi kukukubalia wewe matakwa yako BINAFSI, tupo kwa ajili ya UMMA,ambao una changamoto nyingi zaidi ya hiyo ya kumfahamu Mgombea Urais wa UKAWA.Lengo la Uzi wako ni kuwavuruga wanaUKAWA kwa Maoni yako yasiyo na malengo mazuri,wajikute wanaanza ligi isiyo na Tija!
 
Nafahamu kuwa changamoto kuu kuliko zote ya UKAWA ni kutayarisha MoU kwa wanahisa, yaani nani awe nani na nani apate nini kama mende atafanikiwa kuliangusha kabati. Hata hivyo kuwa na kiongozi mwenye mvuto, anayekubalika kwa kanda, makabila na dini zote na asiye na kashifa is equally important.
 
WanaUKAWA hawana haja ya mambo ya "Kanda zote,dini zote,na makabila yote", tuna haja na "MAMA TANZANIA NA WATANZANI".Mbinu yenu ya kuwagawa watanzania kwa Dini zao,Makabila yao,na Kanda zao,imefika UKOMO, Bakini nayo ndani ya chama chenu kwani ndiyo SERA yenu.HATUPO KWA MATAKWA YAKO NA CCM YAKO BALI WATANZANIA WANAOTESWA NA HALI YA NCHI YAO ILIVYO KWA SASA!
 
Kama uzi huu ningeandika "Mbowe ndiye mwenye afadhali UKAWA", uchangiaji ungekuwa tofauti kabisaaa! watch out!
 
Tatizo kubwa la wapinzani nchini wanahangaika zaidi na yanayotokea ndani ya CCM badala ya kuhangaika na mambo ya wananchi na yale yaliyoko ndani ya vyama vyao vya upinzani. Wapinzani wanajadili waliotangaza nia CCM badala ya kuanza mapema kuongelea nani anafaa kuwa mgombea wao 2015 dhidi ya mgombea atakaeteuliwa na CCM (Lowassa? Sitta? Membe? Pinda? Mwigullu? Sumaye? Wassira? Makamba? Nyarandu? Kigwangala?, Migiro? Makinda? au.....?). Ni vema hata vyama vya upinzani kuanza kujitokeza kutangaza nia ili watu waanze kuwajadili kidogokidogo.

Upinzani ina Professor LImbumba hadi sasa ambaye ana haiba ya kugombea urais 2015. Lipumba hana kashifa yoyote mbaya kwenye jamii itakayoweza kutumiwa na wagombea wengine kumpinga. Lipumba hana tamaa, hana ukabila wala udini ni mwislamu wa kawaida tu anayemcha mungu, ni msomi na mchumi, na hajawahi kunyang'anya mke wa mtu.

Kama UKAWA ikimuandaa vizuri Lipumba, kumpamba na kumuunga mkono kwa hali na mali anaweza kushindana na mgombea yeyote kutoka CCM.

Angalia hii video halafu ndo urudi hapa na hizi porojo zako
m.youtube.com/watch?v=ujwfFUUAD70
 
Back
Top Bottom