Lipumba ndiye mwenye afadhali UKAWA

Lipumba ndiye mwenye afadhali UKAWA

kavulata

JF-Expert Member
Joined
Aug 2, 2012
Posts
16,252
Reaction score
16,171
Tatizo kubwa la wapinzani nchini wanahangaika zaidi na yanayotokea ndani ya CCM badala ya kuhangaika na mambo ya wananchi na yale yaliyoko ndani ya vyama vyao vya upinzani. Wapinzani wanajadili waliotangaza nia CCM badala ya kuanza mapema kuongelea nani anafaa kuwa mgombea wao 2015 dhidi ya mgombea atakaeteuliwa na CCM (Lowassa? Sitta? Membe? Pinda? Mwigullu? Sumaye? Wassira? Makamba? Nyarandu? Kigwangala?, Migiro? Makinda? au.....?). Ni vema hata vyama vya upinzani kuanza kujitokeza kutangaza nia ili watu waanze kuwajadili kidogokidogo.

Upinzani ina Professor LImbumba hadi sasa ambaye ana haiba ya kugombea urais 2015. Lipumba hana kashifa yoyote mbaya kwenye jamii itakayoweza kutumiwa na wagombea wengine kumpinga. Lipumba hana tamaa, hana ukabila wala udini ni mwislamu wa kawaida tu anayemcha mungu, ni msomi na mchumi, na hajawahi kunyang'anya mke wa mtu.

Kama UKAWA ikimuandaa vizuri Lipumba, kumpamba na kumuunga mkono kwa hali na mali anaweza kushindana na mgombea yeyote kutoka CCM.
 
Kama ambavyo wewe ulivyo na afadhali ndani ya Chichiem.... Kweli baba yako hakupoteza mbegu bure.
 
Ndani ya UKAWA kwa sasa mtu mwenye lugha ya utawala ni Dr Slaa,na baadae naona mtatiro,wenje,halima mdee,mnyaa,kafulila.Ilala kwa sasa hapa tz hakuna anayemfikia slaa
 
Mwenye umakini na uthubutu wa urais Tanzania kwa tiketi ya CCM ni Dr. Lowassa our beloved brother aliyeshiba na aliyeonyesha nia ya kuwatumikia wenye Njaa akiwemo (B.M & M.P bila kumsahau N. Lazaro).
 
Muda ukifika tutajadili kwanza zoezi tulilonalo ni kuhamasisha wananchi wajue UKAWA na kukataa Katiba ya CCM hatutaki kuanza kupaluana kama CCM kwanza lazima tuunde mfumo mzuri wa uteuzi badala ya fujo
Ila kama umetumwa na CCM pole sisi tutachagua mgombea wetu vizuri hata Mbati au Lwetama
 
Ndani ya UKAWA kwa sasa mtu mwenye lugha ya utawala ni Dr Slaa,na baadae naona mtatiro,wenje,halima mdee,mnyaa,kafulila.Ilala kwa sasa hapa tz hakuna anayemfikia slaa
Mungu alishatoa maelekezo kwa kanisa katoliki kuwa slaa kalaaniwa mbinguni na duniani.
 
Naamini hata UKAWA wenyewe wanajua wanachokifanya ndani ya umoja wao, sina hakika kama hawana kabisa ajenda za nani agombee nafasi hizo. Hebu tuwe na subira tukiwa na imani kwamba viongozi wengi ndani ya vyama vya UKAWA wana uzoefu wa kutosha sana na siasa za hii nchi na wengine ni wasomi, yaani ni maprofesa wa kitanzania, siyo wa kichina, katika mambo ya siasa na mambo mengine mbalimbali.

Nafikiri UKAWA wanaongozwa na nidhamu katika kutangaza nia ya kugombea nafasi mbali mbali za uongozi, na hasa katika taasisi kubwa kabisa ya urais, siyo kama CCM ambayo kila anayejisikia (awe na kashifa za ufisadi, wizi n.k) akijisikia tu anatangaza kuwania nafasi hiyo ambayo kiukweli inastahili kupewa heshima kubwa na anayetangaza nia basi walau afanane kweli na hiyo nafasi.

Ni vizuri umetoa maoni yako na mtazamo wako juu ya Prof. Lipumba, naamini watakaohusika katika uteuzi wa mgombea wa urais watazingatia pia maoni yako katika uteuzi wao.
 
Usiwachagulie UKAWA, kiongozi wa kugombea, muda ukifika watawania nafasi na watakaoteliwa wenyewe, ccm mna tatizo kubwa la kutaka kushughulikia vyama vya upinzani badala ya kuwatumikia wananchi na ndio maana jamii imeanza kuwakataa kwa kasi kwani uwekezaji wenu upo kwenye kutaka kuua vyama vya wenzenu huku mkileta porojo kwenye huduma jambo ambalo halitawaoko, 2015 ndio hii subirini muone kivumbi chenu. Kuna kila dalili za chama chenu kufa kabisa kuanzia mei mwaka huu, ikiwa chama chenu kitampitisha yeyote zaidi ya Lowasa tegemeo lenu basi mamvi lazima akiangamize hicho chama ambacho kwa miaka 19 iliyopita amekifanyia uwekezaji, na hata akipita hawezi kufua dafu kwa mgombea wa Ukawa na jinsi anavyouota uraisi kila siku toka azaliwe sidhani kama hataingia SELOU kulianzisha, nacheka sana nikiifikiria future ya ccm nusu mwaka ujao.
 
Ndani ya UKAWA kwa sasa mtu mwenye lugha ya utawala ni Dr Slaa,na baadae naona mtatiro,wenje,halima mdee,mnyaa,kafulila.Ilala kwa sasa hapa tz hakuna anayemfikia slaa

Nimetaja sifa za Lipumba, taja sifa za Slaa kama kweli unataka kuisaidia UKAWA. Hatusemi Dkt. Slaa hafai ila tunataka anayefaa zaidi kwa kupitia mijadala kama hii. Tunajenga nyumba moja haifai kugombea fito.
 
Mtoa mada mbona mke wako anachukuliwa na wanaume wengine na hatusemi?
 
Nimetaja sifa za Lipumba, taja sifa za Slaa kama kweli unataka kuisaidia UKAWA. Hatusemi Dkt. Slaa hafai ila tunataka anayefaa zaidi kwa kupitia mijadala kama hii. Tunajenga nyumba moja haifai kugombea fito.

Waliokutuma kupima kina cha maji wambie kuna mafuriko.
 
Muda ukifika tutajadili kwanza zoezi tulilonalo ni kuhamasisha wananchi wajue UKAWA na kukataa Katiba ya CCM hatutaki kuanza kupaluana kama CCM kwanza lazima tuunde mfumo mzuri wa uteuzi badala ya fujo
Ila kama umetumwa na CCM pole sisi tutachagua mgombea wetu vizuri hata Mbati au Lwetama

Mgombea atakuwa rais wa watanzania wote atahitaji kura za watu wote sio wana ukawa tu, ni vema watanzania wakamjua rais wao mtarajiwa mapema ili wawe na muda mrefu wa kumjadili.
 
baadh ya wanachama wa CHADEMA hawatak kabisg kusiki jina la LIPUMBA sijajua tatizo ninin?
 
Mgombea atakuwa rais wa watanzania wote atahitaji kura za watu wote sio wana ukawa tu, ni vema watanzania wakamjua rais wao mtarajiwa mapema ili wawe na muda mrefu wa kumjadili.
Tutamchagua mama yako apeperushe bendera ya ukawa usiogope ...
 
Tatizo kubwa la wapinzani nchini wanahangaika zaidi na yanayotokea ndani ya CCM badala ya kuhangaika na mambo ya wananchi na yale yaliyoko ndani ya vyama vyao vya upinzani. Wapinzani wanajadili waliotangaza nia CCM badala ya kuanza mapema kuongelea nani anafaa kuwa mgombea wao 2015 dhidi ya mgombea atakaeteuliwa na CCM (Lowassa? Sitta? Membe? Pinda? Mwigullu? Sumaye? Wassira? Makamba? Nyarandu? Kigwangala?, Migiro? Makinda? au.....?). Ni vema hata vyama vya upinzani kuanza kujitokeza kutangaza nia ili watu waanze kuwajadili kidogokidogo.

Upinzani ina Professor LImbumba hadi sasa ambaye ana haiba ya kugombea urais 2015. Lipumba hana kashifa yoyote mbaya kwenye jamii itakayoweza kutumiwa na wagombea wengine kumpinga. Lipumba hana tamaa, hana ukabila wala udini ni mwislamu wa kawaida tu anayemcha mungu, ni msomi na mchumi, na hajawahi kunyang'anya mke wa mtu.

Kama UKAWA ikimuandaa vizuri Lipumba, kumpamba na kumuunga mkono kwa hali na mali anaweza kushindana na mgombea yeyote kutoka CCM.

Allah Akbar!
 
Back
Top Bottom