MwanaCBE
JF-Expert Member
- Sep 23, 2009
- 1,771
- 804
NDALICHAKO tuma Polisi wavamie nyumbani kwa LIPUMBA, ukague vyeti vyake!
Siamini kama anamiliki PhD huyu!
Hawawezi kwani naye ni mtumwa mwenzao wa chama
NDALICHAKO tuma Polisi wavamie nyumbani kwa LIPUMBA, ukague vyeti vyake!
Siamini kama anamiliki PhD huyu!
Prof anajidhalilisha sana na kudhalilisha academic credentials zakeAmeandika barua ya kutengua kujiuzuru kwake uwenyekiti. Alijivua uwenyekiti akaenda fanya biashara zake binafsi sasa amerudi na kuutaka uwenyekiti kama vile aliuweka store.
Akili zao zinafananaLipumba amefanya kama alivyo fanya seif zanzibar. Seif alijitangazia ushindi na sasa Lipumba kajitangaza yeye ni mwenyekiti.
Jamani, ngoma sasa inogile. Prof. leo kakomaa hataki kabisa kuambiwa amesimamishwa uanachama.
Hii safi sana maana maalim anaendesha chama kama mali yake.
===========
Akihojiwa na mtangazaji Spencer Lamerk wa ITV usiku huu, Prof. Ibrahim Haruna Lipumba amesema kuwa yeye bado ni Mwenyekiti halali wa CUF.
Prof. Lipumba amesema kuwa kufuatia kutengua barua yake ya kujiuzulu Uenyekiti, aliandika barua kwa Katibu Mkuu wake kutaka kurejea kazini kama Mwenyekiti. Katibu Mkuu alimjibu kuwa anatafuta ushauri wa kisheria.
Kuhusu kikao cha Baraza Kuu la CUF kilichomsimamisha uanachama, Profesa Lipumba amesema kuwa kikao hicho hakikuwa halali kwakuwa hakukuwa na akidi ya Wajumbe wa kutoka Tanzania Bara. Amesema kuwa Katibu Mkuu hamshirikishi Naibu Katibu Mkuu Bara na kuonekana akiendesha chama kiimla.
Prof. Lipumba amesema kuwa Katibu Mkuu asipotaja tarehe ya yeye kurejea kazini kama Mwenyekiti, atasubiri barua ya Msajili wa Vyama ili aanze kazi tena kama Mwenyekiti wa taifa wa CUF.
Wee zito angewezaje kuleta huo ujinga CDM. Tangu 2008 aliambiwa afanye chochote au aende kokote akashindwa.Huyu jamaa Hana tofauti Na zitto naona anatapa tapa.
Alijua atabembelezwa,.. Kakutana na msoto mkali, kachenji gia juu kwa juuTamaa ya madaraka watu kama hawa ni hatari sana.alijiuzulu mwenyewe leo hii anarudi kwa nguvu.
Sikuwahi kujua Title ya Prof inaficha upumbavu mwingi wa mtu
Lipumba amefanya kama alivyo fanya seif zanzibar. Seif alijitangazia ushindi na sasa Lipumba kajitangaza yeye ni mwenyekiti.
Anatumiwa na MACCM ili kudhoofisha CUF na hatimaye kudhoofisha UKAWA. Kauli zake zinaweza kusababisha shari na hata watu kupigana kuumizana, kutiana vilema na hata kuuwana, lakini hili polisiccm haliwahusu maana kama kitengo cha MACCM wanakaa pembeni ili kuangalia mtafaruku wa ndani ya CUF na huku wakimsaidia Lipumba kwa kila namna ili aendelee kuivuruga CUF.
Alimtaarifu maalim Seif kwani yeye ndio mwenye maamuzi ya kumrudisha? Alimtaarifu kwa barua rasmi ama kwa mdomo?
Lipumba kapatwa na nini?