Tetesi hii labda ilianza kabla J.K. hajashauriwa na A.G. Werema kwamba kumteua Mtanzania ambaye sio Mbunge wa kuchaguliwa Jimboni ni kinyume na Katiba.
Kama J.K. amependa sana kujikomba kwa Lipumba, basi amteue Mbunge kwa kutumia madaraka yake ya kuweza kuteua Wabunge 10, halafu amteue Waziri wa Fedha. Katiba inatamka kwamba mtu hawezi kuteuliwa waziri kama sii Mbunge. Lakini mtu huyo anaweza kuwa Mbunge wa Viti Maalum, Mbunge wa Kuteuliwa ama Mbunge wa kuchaguliwa ktk Jimbo.