Chungu, Tamu Mabadiliko Baraza la mawaziri 2022

Peter Stephano 809

Senior Member
Feb 29, 2020
117
158
Baada ya Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan kufanya mabadiliko mbalimbali kwenye baraza lake la Mawaziri watu wameibuka na maoni tofauti tofauti.

Katika mabadiliko hayo rais ameunda wizara 3 zenye mwonekano mpya, amewahamisha na kuwaondoa kabisa baadhi ya Mawaziri kwenye baraza hilo huku wengine wakipata Uteuzi kwa mara ya kwanza.

Je ipi ni Chungu,tamu ya uteuzi huo wadau na raia wamebaini?

Kundi la kwanza la raia wanasifu mabadiliko hayo kuwa yana manufaa makubwa kwakuwa rais amesuka kikosi kazi chenye kuendana na maono yake.

Mabadiliko hayo yanatimiza ahadi yake aliyoitoa januari 4 alipokuwa anapokea ripoti ya matumizi ya fedha ya mpango wa UVIKO19 ambapo alisema anakusudia kufanya mabadiliko kwenye baraza lake la Mawaziri.

Aidha wanaosifu mabadiliko hayo wanasema rais alirithi baraza hilo kutoka kwa mtangulizi wake hivyo kulikua na kila sababu kufanyiwa marekebisho ili apate mawaziri wa kuendana nae.

Si hivyo tu bali wanaeleza kuwa kuna kundi la mawaziri ambao hawakuwa wafuasi wa sera za rais na serikali iliyopo madarakani hivyo ilikuwa ni lazima waondolewe ili kuwapisha wengine.

Kwani hata rais alisema atafanya mabadiliko ili kuwaweka kando wale wenye maono ya uchaguzi mkuu wa 2025 wakajiandae wakiwa nje ya uwaziri.

Hata hivyo kundi la pili linalounga mkono mabadiliko haya linaonekana kutoridhishwa na baadhi ya uteuzi na uhamisho wa mawaziri kutoka wizara moja kwenda nyingine mfano kumtoa Mohammed Mchengelwa kwenye wizara ya Utumishi kwenda wizara ya utamaduni wakidai kuwa alitimiza majukumu yake kwa asilimia mia akiwa huko hivyo hakukuwa na haja ya mabadiliko hayo.

Aidha kundi hili linapendekeza rais angefanya uteuzi kulingana na taaluma na utashi wa mawaziri husika kwa kuwateua kushika nyadhifa zenye kuakisi taaluma zao.

Hata hivyo kundi hili linapongeza uhamisho wa Ummy Mwalimu kurejeshwa wizara ya Afya ambayo alikuwepo awali kabla ya kuhamishiwa tamisemi.

Kundi la mwisho linabainisha udhaifu wa mfumo wa Uteuzi kuendelea kuto zingatia masuala ya jinsia na umri kwani bado Vijana na wanawake wanaonekana kupewa nafasi finyu katika uteuzi huo huku wanao teuliwa kuwa ni wale wale wanajirudia kwa miaka mingi Sasa.

Je, mabadiliko haya ni Chungu au tamu kwa ujumla?

Peter Mwaihola kitaaluma ni mwandishi wa Habari na Mchambuzi wa Masuala ya siasa na jamii.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

1 Reactions
Reply
Top Bottom