Elections 2010 Lipumba kupewa nafasi baraza la Mawaziri?

Malunde-Malundi

JF-Expert Member
Jan 10, 2008
1,288
130
Kuna tetesi kuwa JK ameamua kufanya kweli, baada ya Lipumba kumtambua sasa kumpa uwaziri mkuu au kuunda nae serikali ya umoja wa kitaifa kwa kuchagua akina Rashid mohamed kuwa mawaziri wa JK nk, ili kuendeleza ule muafaka wa Zanziba na huku kughiribu kuwa alikuwa bega jwa bega na wapinzani; naona kuna siri sirini; ngoja tuone nini kitatokea
Hii inathibitisha kuwa Chadema kuendelea kuwa chama cha upinzani kwa Tanzania nzima
 
hicho kitu hakiwezi kufanywa na CCM kwani kumpa madaraka Lipumba ni sawa na kujipalilia makaa,
 
wampe wasimpe haituhusu ila jk atambue siku imekaribia,siku ambayo dunia nziama itamgeuka
 
JK kwa unafiki anaweza kumpa kweli, lakini kwa mujibu wa katiba kwa kuwa ameshinda kwa zaidi ya 50% ya kura zilizopigwa, hana sababu ya kumshirikisha Lipumba. Katiba inamruhusu kuunda serikali ya CCM.
 
jamani tuwe tunafanya utafiti kabla kuzua mambo. Katiba ya JMT inasema waziri mkuu atatokana na wabunge wa kuchaguliwa.
 
Kitu hicho ni uongo kwan kwa mujibu wa katiba yetu Waziri mkuu hutokana na chama chenye wabunge wengi zaidi bungeni. Sasa je ni cuf pia maalim seif tayari ni kiongozi wa ngazi za juu huko zenji anawezaje kuwa na vyeo viwili? That's imposible my friend.
 
Someni Katiba kwanini Lipumba hawezi kuwa waziri mkuu. Sio mbunge wa kuchaguliwa


SEHEMU YA TATU
WAZIRI MKUU, BARAZA LA MAWAZIRI NA SERIKALI

51.-(1) Kutakuwa na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano atakayeteuliwa na Rais kwa kufuata masharti ya ibara hii na ambaye kabla ya kushika madaraka yake ataapa mbele ya Rais kwa kiapo kinachohusika na kiti cha Waziri Mkuu kitakachowekwa na Bunge.
(2) Mapema iwezekanavyo, na kwa vyovyote vile ndani ya siku kumi na nne, baada ya kushika madaraka yake, Rais atamteua Mbunge wa kuchaguliwa kutoka katika Jimbo la Uchaguzi anayetokana na chama cha siasa chenye Wabunge wengi zaidi Bungeni au kama hakuna chama cha siasa chenye Wabunge wengi zaidi, anayeelekea kuungwa mkono na Wabunge walio wengi kwa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano, naye hatashika madaraka hayo mpaka kwanza uteuzi wake uwe umethibitishwa na Bunge kwa azimio litakaloungwa mkono na kura za Wabunge walio wengi.
 
JF imekuwa na wazushi wengi post zingine pelekeni kwenye jokes hapa leteni habari za ukweli
 
Ni maneno tu ya kijiwen.hayana ukwel wowote.tusubir tu kulikaria jit tena mpaka 2015..mungu ashuke na hashuk.
 
Ndio hawa hawa waliozusha kuwa yule msomali anatayalishwa kuwa Spika!! Jana ilikuwa siku ya mwisho ya kuchukua fomu na yeye hakuchukua kwahiyo angojee pengine anaweza kumrithi Makamba!!
 
Tetesi hii labda ilianza kabla J.K. hajashauriwa na A.G. Werema kwamba kumteua Mtanzania ambaye sio Mbunge wa kuchaguliwa Jimboni ni kinyume na Katiba.

Kama J.K. amependa sana kujikomba kwa Lipumba, basi amteue Mbunge kwa kutumia madaraka yake ya kuweza kuteua Wabunge 10, halafu amteue Waziri wa Fedha. Katiba inatamka kwamba mtu hawezi kuteuliwa waziri kama sii Mbunge. Lakini mtu huyo anaweza kuwa Mbunge wa Viti Maalum, Mbunge wa Kuteuliwa ama Mbunge wa kuchaguliwa ktk Jimbo.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom