Lipumba: JK atamaliza urais vibaya | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Lipumba: JK atamaliza urais vibaya

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Saint Ivuga, Mar 21, 2011.

 1. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #1
  Mar 21, 2011
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 39,276
  Likes Received: 19,423
  Trophy Points: 280
  Lipumba: JK atamaliza urais vibaya Send to a friend Sunday, 20 March 2011 21:04 0diggsdigg

  Burhani Yakub,Tanga
  CHAMA cha Wananchi (CUF) kimesema Rais Jakaya Kikwete atamaliza muda wake akiwa ameshindwa vibaya kusimamia shughuli za Taifa la Tanzania.

  Alisema endapo Rais Kikwete anataka kukumbukwa katika historia, atumie muda uliobaki katika kuhakikisha katiba inafanyiwa marekebisho na tume ya uchaguzi inakuwa huru.

  Ushauri huo ulitolewa jana na Mwenyekiti wa CUF,Profesa Ibrahimu Lipumba wakati akizindua kitaifa oparesheni Zinduka katika viwanja vya Tangamano jijini Tanga.

  Alisema kati ya marais waliomtangulia kuongoza Tanzania kuanzia awamu ya Baba wa Taifa, Mwalimu Nyerere hakuna rais aliyeshindwa vibaya kusimamia masuala ya kitaifa kama Rais Jakaya Kikwete, tofauti na matarajio ya wananchi ambao walikuwa na imani kubwa wakati wakimchagua mwaka 2005.

  “Kikwete ameshindwa kusimamia elimu ameweka rekodi ya kufelisha wanafunzi wa kidato cha nne ambayo haijawahi kutokea tangu tupate uhuru,kwenye afya mambo ni magumu katika uchumi, huko hakusemeki
  ameshindwa kuzuia mfumuko wa bei, mpaka sasa umeme ni ngonjera tu miaka 50 ya uhuru Tanzania iko gizani,”alisema Lipumba.

  Mwenyekiti huyo ambaye pia ni mchumi alisema chanzo cha kuanguka kwa uchumi wa Tanzania ni baada ya Rais Jakaya Kikwete kushindwa kuwadhibiti mapapa wa rushwa na ufisadi nchini akiwaogopa na kuwaacha wafanye wanachotaka jambo ambalo limewakatisha tama wananchi.

  “Utawala wa Kikwete unakabiliwa na ombwe la uongozi, na hii inatokana na mfumo wa CCM ambao ameshindwa kila kitu,lakini kwa ushauri wangu ni kuwa kama anataka akumbukwe na historia basi ajikite zaidi katika kusimamia
  marekebisho ya katiba na tume ya uchaguzi”alisema Lipumba.

  Alisema jambo pekee ambalo Rais Kikwete ameanza kulisimamia ni kulivalia njuga suala la marekebisho ya katiba kwa kuhakikisha inabalishwa kulingana na matakwa ya Watanzania na si vinginevyo.

  Lipumba alisema mchakato wa katiba unatakiwa uanze haraka ili kutoa fursa kwa Watanzania kuchangia maoni yao, lakini alisisitiza kuwa inatakiwa kwenda sambamba na kuunda tume ya uchaguzi ili huru na siyo kuwa na katiba ya sasa ambayo inafanya kazi ya kuchakachua kura na matokeo.

  “Tume iliyopo haifai, hata kwenye tovuti yake haiandiki idadi halisi ya wapiga kura, imechakachua hadi daftari la wapiga kura, tunataka tume isiyowatumia watendaji wa Halmashauri wakiwamo wakurugenzi watendaji
  na maofisa watendaji,”alisema Lipumba ambaye aaliambatana na Mbunge wa jimbo la Wawi Hamad Rashid Mohamed.

  Aliwata wananchi kutumia fursa hiyo kwa kujitokeza kutoa maoni ya marekebisho ya katiba kwa kuwa ni haki yao na kwamba wahakikishe wanapendekeza masuala muhimu yenye kuligusa Taifa.

  Kuhusu suala la kufanya maandamano na mikutano ya hadhara,Lipumba alisema ni haki ya vyama vya siasa na wananchi kuandamana kudai marekebisho ya katiba na kulalamikia mambo ambayo haendi sawa kutokana na uzembe wa viongozi wa Serikali ya CCM.

  Aliwaasa wananchi kujihadhari na kauli zinazotolewa na baadhi ya viongozi wanaosema Tanzania haitatawalika na kwamba kinachotakiwa ni kufuata taratibu kwani Serikali iliyopo itang’olewa madarakani kwa kura na siyo vurugu.

  “Msikubali kushabikia kauli zenye kuashiria vurugu,kama tusipoangalia tutasababisha CCM iendelee kushika dola,napenda kuwaeleza kuwa CCM imeshafikia mwisho tutaing’oa kwa kufuata taratibu”alisema Lipumba.
   
 2. SILENT WHISPER

  SILENT WHISPER JF-Expert Member

  #2
  Mar 21, 2011
  Joined: Jun 26, 2009
  Messages: 2,231
  Likes Received: 53
  Trophy Points: 145
  :hatari::hatari::hatari:
   
 3. Mphamvu

  Mphamvu JF-Expert Member

  #3
  Mar 21, 2011
  Joined: Jan 28, 2011
  Messages: 10,708
  Likes Received: 933
  Trophy Points: 280
  Wakati wa CCM umefika mwisho wakati ndo wanakula pamoja nchi huko Visiwani... Mbona Lipumba anatuchezea akili jamani...
   
 4. M

  Mtabe JF-Expert Member

  #4
  Mar 21, 2011
  Joined: Sep 20, 2010
  Messages: 675
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Picture please
   
 5. S

  SeanJR Member

  #5
  Mar 21, 2011
  Joined: Feb 26, 2011
  Messages: 38
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  lipumba *****,anatapatapa ka mwanamke mjamzto wa miezi 7! Haeleweki anamcmamo gani! Rabish lipumba
   
 6. czar

  czar JF-Expert Member

  #6
  Mar 22, 2011
  Joined: Oct 11, 2010
  Messages: 340
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Sasa akimaliza vibaya inatusaidiaje sisi? Badala ya kutupa mwongozo wa kufanya unatabiri umekuwa shehe Yahya wewe? Tuambie kwa ugumu huu tufanye hivi au vile.
   
 7. Gama

  Gama JF-Expert Member

  #7
  Mar 22, 2011
  Joined: Jan 9, 2010
  Messages: 9,224
  Likes Received: 1,411
  Trophy Points: 280
  Acha ujinga wako, umemaliza kutapika sasa toa hoja.
   
 8. Gama

  Gama JF-Expert Member

  #8
  Mar 22, 2011
  Joined: Jan 9, 2010
  Messages: 9,224
  Likes Received: 1,411
  Trophy Points: 280
  Kwani huwezi kujadiri hoja?!‎؛‎, tazama key words from original post- huduma duni za afya, matokeo mabaya ya kidato cha nne kuliko yaliyo wahi kutokea toka tupate uhuru, mfumuko wa bei, ongezeko la mafisadi.............................. Bado tu hunacha kujadiri mpaka uanze kumjadiri mtoa hoja?!. Be a graet thinker and not sinker.
   
 9. e

  emrema JF-Expert Member

  #9
  Mar 22, 2011
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 270
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Uchochezi na uharibifu wa amani huo..... na yeye ajadiliwe na SISIEMU yao! Ikiwezekana akamatwe.
   
 10. Mphamvu

  Mphamvu JF-Expert Member

  #10
  Mar 22, 2011
  Joined: Jan 28, 2011
  Messages: 10,708
  Likes Received: 933
  Trophy Points: 280
  Sijui kama unaijua siasa vizuri ndugu, siasa ni unafki. Ni lazma tujue kuhusanisha maneno na vitendo, huwezi kutamka vitu ambavyo hakuna mazingira ya kuvisimamia, halafu tuunge mkono. Back to CUF, hata watamke nini, hawana uwezo wa kuavocate wakati tayari kuna maridhiano kati yao na serikali ya CCM wanayoituhumu, na kama ni mfuatiliaji mzuri, matamko ya CUF yanakinzana, leo hili, kesho lile. Cant swallow that man...
   
 11. LD

  LD JF-Expert Member

  #11
  Mar 22, 2011
  Joined: Aug 19, 2010
  Messages: 3,021
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  Ulimuona wapi huyo aiseeee!!!
   
 12. S

  SeanJR Member

  #12
  Mar 22, 2011
  Joined: Feb 26, 2011
  Messages: 38
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Gama una macho ila ukipofu ,unamasikio ila u kiziwi! Lipumba ukimfuatilia huoni mcmamo wake,cku chache alikua akiponda CDM na kumtukuza kikwete,kwenye hii thread yake anamwambia kikwete atamaliza vibaya! CDM Ilipita mikoani ikipinga ugumu wa maisha,kuilipa dowans na n.k,lipumba hakuliona hilo akadai wanataka kumpindua kikwete,leo hii anarudi kulekule kwa CDM,au yeye ndo anataka ampindue kikwete! gama acha uvivu wa kufikiria na acha ushabiki usio na maana! Ugumu wa maisha unazidi hvyo hatutaki kiongozi asie na msimamo kama lipumba!!
   
 13. S

  SeanJR Member

  #13
  Mar 22, 2011
  Joined: Feb 26, 2011
  Messages: 38
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Haa ha haaa, Yupo mitaa ya hapa kwetu alikua mpole alivyofika miezi 7 tu,mara nataka kuku,ukileta anazira na anakuambia amekinai hataki tena nlitee udongo! Ndo hali ya lipumba...CDM walipita mikoani kupinga mfumuko wa bei,kuilipa dowans,kufeli kwa 4m 4,kudai katiba mpya n.k,lipumba akadai wanataka kupindua nchi LEO hii anadai kikwete atamaliza vibaya na kupita mlemle mwa wanaCDM.Tumuelewe huyu ndie anaetaka kumpindua kikwete au anatuyeyusha!!
   
Loading...