Lipumba aondoka nchini baada ya kujiuzulu

Lipumba aondoka nchini baada ya kujiuzulu

Noel france

JF-Expert Member
Joined
Oct 8, 2012
Posts
1,159
Reaction score
1,054
Wasalamu wanandugu,

Habari nilizozisikia hivi punde ni kwamba Prof. Ibrahim Lipumba ameondoka nchini na ndege ya Rwanda jana baada ya kumaliza kuongea na waandishi wa habari.

==========================================

SAA chache baada ya Profesa Ibrahim Lipumba kutangaza kujiuzulu wadhifa wa Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi (CUF), ametoweka nchini.

Hata hivyo, haikufahamika mara moja amekwenda nchi gani na atakaa kwa muda gani.

Profesa Lipumba aliondoka nchini baada ya kumaliza mkutano wake na waandishi wa habari katika Hoteli ya Peacok jijini Dar es Salaam, ambako alitangaza kujiondoa katika chama chake na katika Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa).

Taarifa zilizopatikana, baada ya kumaliza mkutano na waandishi, alielekea Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA), na aliondoka nchini kwa kutumia ndege ya Shirika la Ndege la Rwanda (Rwanda Air).

Awali kiongozi huyo ambaye alivaa suti ya ‘dark blue' na shati jeupe alikuwa apande ndege ya Shirika la Ndege la Kenya (KQ) 485, lakini alibadili mwelekeo baada ya kufika uwanjani na kuamua kupanda Rwanda Air kuelekea Kigali saa 9 alasiri.

Chanzo cha uhakika kutoka uwanjani hapo, kililieleza MTANZANIA kuwa Profesa Lipumba, alifika saa 7:00 mchana akiwa na vijana wawili wa kiume ambao walionekana kama walinzi wake.

Katika muda huo ambao Profesa Lipumba alikuwa katika taratibu za kuondoka, palikuwapo na ndege nne tu za kwenda nje ya nchi.

Vijana hao ambao hawakujulikana majina yao, walikuwa wakifuatilia kila hatua ya kile alichokuwa akikifanya Profesa Lipumba, huku yeye akionekana mwenye wasiwasi na msongo mkubwa wa mawazo.

"Profesa Lipumba anaonekana hayuko katika hali ya kawaida, anaonekana ni mtu mwenye msongo wa mawazo, na pia ana wasiwasi kama vile kuna jambo linamsumbua.

"Macho yake yalionekana ni mekundu mithili ya mtu aliyekuwa akilia kwa muda mrefu, huku uso wake ukionekana hauna furaha," kilisema chanzo chetu.

Wakati hayo yakiendelea, Katibu Mkuu wa CUF, Maalim Seif Sharif Hamad, amelazimika kukatisha shughuli za kiserikali alizokuwa nazo Zanzibar na kwenda jijini Dar es Salaam kunusuru hali ya sintofahamu ndani ya chama hicho.

"Ndiyo hivyo imeshatokea, lakini tayari katibu mkuu amekuja bara kuhakikisha mambo yanakaa sawa na chama hakiyumbi," alisema kiongozi wa CUF ambaye hakupenda kutajwa gazetini.

Chanzo: Mtanzania
 
Wasalamu wanandugu;habari nilizozisikia ivi punde,nikwamba Prof.Ibrahim Lipumba ameondoka nchini na ndege ya uganda jana baada ya kumaliza kuongea na waandishi wa habari.
chanzo rfa magazeti

Anaenda wapi kufanya nini? Au ndio anaenda kuongezewa mpunga wa MICCM?? Ameshachelewa. Wana CUF tumeshafunguka siku nyingi
 
Wadau.

Akiwa amepewa sabuni ya roho ndani ya ulinzi unaomridhisha,huyu bwana aliyemsifia sana EL siku alipojiunga UKAWA kapanda ndege ya Kagame RWANDAIR kufika Nairobi then aunganishe Kenya Airways mpaka uwanja uitwao OLIVER THAMBO...

Yadaiwa atatoka Johannesburg baada ya siku tatu kwenda London.

Lengo ni kukwepa hasira za wana CUF aliowasaliti.
 
Mara baada ya kuhitimisha mkutano wake na waandishi wa Habari, Lipumba aliongozana na walinzi wake wawili, kuelekea uwanja wa ndege wa Dar es Salaam, na kusafiri kwenda mapumzikoni nje ya nchi.
Source: Gazeti la Nipashe
 
Kumbe muongo hivi, yaani atasaidia harakati za UKAWA na CUF akiwa nje tena katika kipindi hiki kigumu cha kuelekea uchaguzi!?
 
Anaenda wapi kufanya nini? Au ndio anaenda kuongezewa mpunga wa MICCM?? Ameshachelewa. Wana CUF tumeshafunguka siku nyingi

nasikia amekwenda kupumzika. Ila usishangae uwenda kaenda kuchukua chake
 
Anaogopa Kufanyiwa Umafya na lile Genge linalomzingira Slaa asiongee na Media, hata yeye mwenyewe juzi chupu chupu Kufanyiwa mbaya ndo akaahirisha mkutano
 
Back
Top Bottom