maramia
JF-Expert Member
- Jul 17, 2015
- 2,030
- 1,345
Nadhani huyu profesa wetu wa uchumi kaanza kuchanganyikiwa. Eti anamshauri Magufuli aiendeshe nchi na atutawale akiwa amelenga kuja kuipata tuzo ya tajiri Mohamed Ibrahim inayotolewa kwa Rais wa Afrika anayefanya vizuri kwenye utawala wake.
"Mpania maji hayanywi" usianze kumdanganya Rais wetu afanye kazi kwa kupania mamilioni ya Mohamed ambayo hatujui anayapataje, Magufuli hataki vya bure na hatafanya kazi kwa kupania au kwa malengo ya kupata mapesa baada ya kustaafu. Kuutafuta urais wenyewe hakuupania kama nyie mlivyokuwa mnaupania iweje hayo mapesa?
Kama ni kuipata hiyo tuzo ataweza kuipata bila kufuata huo ushauri wa Lipumba, Rais akiqualify vigezo vilivyowekwa kuipata ataipata tu maana riziki haivutwi, inakuja yenyewe.
Hata tuzo ya Nobel Prize hakuna hata siku moja binadamu katika dunia hii amewahi kuipania akaipata, kama yupo Lipumba tuwekee hapa.
Nakushauri Profesa badala ya kuanza kumpa JPM ushauri wako feki mwache apige kazi, wewe kama bado una busara rudi CUF ukamshauri Seif Shariff ashiriki uchaguzi wa marudio Zanzibar au unyamaze.