Prof. Lipumba: Rais Samia ajiwekee malengo ya kushinda tuzo za Mo Ibrahim kwa kurejesha Utawala bora na Demokrasia

Miss Zomboko

JF-Expert Member
May 18, 2014
3,644
2,000
Mwenyekiti wa CUF, Profesa Ibrahim Lipumba amemshauri Rais Samia Suluhu Hassan kujiwekea malengo ya kutwaa tuzo ya Mo Ibrahim ya utawala bora kwa kurejesha utawala bora unaojali msingi ya demokrasia.

Ameyasema hayo leo Alhamisi Aprili mosi, 2021 katika mkutano wake na waandishi wa habari jijini Dar es salaam akitaka pia mawaziri na watendaji wa Serikali wapewe mikataba ya kupimwa utendaji wao.

"Rais Samia ajiwekee lengo la kushinda tuzo ya Mo Ibrahim. Huyo ni tajiri aliyeanzisha taasisi ya kuzishawishi nchi za Afrika kuwa na utawala bora. Wanaangalia maraisi waliostaafu na waliotimiza vigezo vya utawala bora," amesema Profesa Lipumba.

Amesema wakati huu ambao Rais Samia yuko kwenye fungate la urais anapaswa kujipanga, kujijenga kisiasa badala ya kutafuta maslahi.

"Iwe ni miaka minne na nusu au tisa na nusu atakayotawala, basi ajiwekee lengo la kupata tuzo. Ajiwekee lengo la kulinda na kuheshimu haki za binadamu na utawala bora, ukifika muda watu waone kuwa anafaa kupata tuzo ya Mo Ibrahim," amesema.

Pia Profesa Lipumba amemtaka Rais Samia atambue kuwa uchaguzi mkuu wa 2020 haukuwa halali na hivyo aanze mkakati wa mabadiliko ya katiba yatakayoleta tume huru ya uchaguzi.

Ameendelea kusema kwakuwa Rais Samia alikuwepo kwenye Bunge la Katiba anajua mabadiliko hayo yanawezekana.

"Bahati nzuri amemteua Profesa Kabudi (Palamagamba) kuwa waziri wa katiba na sheria. Ni matumaini yetu kwamba tuwe na katiba yenye maoni ya wananchi.”

"Ndani ya rasimu ya Jaji Warioba, kuna mfumo wa tume huru ya uchaguzi. Makamishna waombe wafanyiwe tathmini, sheria ya uchaguzi ibadilishwe iendane na rasimu ya katiba ili tuwe na tume huru maana hii iliyopo ni tume ya kupanga matokeo," amesema.

Kwa upande mwingine, Profesa Lipumba amemshauri kiongozi mkuu huyo wa nchi kuwapa mikataba ya utendaji mawaziri na watendaji wa serikali ili kupima utendaji wao na kuwawajibisha.

Huku akitoa mfano wa kukamatwa kwa aliyekuwa mkurugenzi wa Mamlaka ya Bandari (TPA), Deusdedit Kakoko, Profesa Lipumba amesema Rais Samia ameonyesha uwajibikaji.
 
kigogo warioba

JF-Expert Member
Jul 11, 2015
5,747
2,000
Huyu hawezi kutoa ushauri
Yaani mtu aliesaidiwa kurudi ofisini na dola ndio aishauri dola tena!?
Huyu ni mataga
Hata hivyo ushauri wake hauvuki hata magomeni
Maana mfumo wa nchi tu ulivyo hauwezi kumfanya mtu akashinda hio tuzo
Rais samia akitaka kurekebisha mfumo mzima itamchukua hata miaka kumi tena
Ndio hawa hawa akina lipumba watakuja kudai kashindwa kufanya haya na haya
Nakumbuka huyu liprofeseri ndio aliovuruga mchakato wa katiba mpya kwa kususia!
Leo anapata wapi hekima ya kuishauri serikali?
 
Nyamatare1987

Senior Member
Mar 29, 2021
184
250
Mwenyekiti wa CUF, Profesa Ibrahim Lipumba amemshauri Rais Samia Suluhu Hassan kujiwekea malengo ya kutwaa tuzo ya Mo Ibrahim ya utawala bora kwa kurejesha utawala bora unaojali msingi ya demokrasia.

Ameyasema hayo leo Alhamisi Aprili mosi, 2021 katika mkutano wake na waandishi wa habari jijini Dar es salaam akitaka pia mawaziri na watendaji wa Serikali wapewe mikataba ya kupimwa utendaji wao.

"Rais Samia ajiwekee lengo la kushinda tuzo ya Mo Ibrahim. Huyo ni tajiri aliyeanzisha taasisi ya kuzishawishi nchi za Afrika kuwa na utawala bora. Wanaangalia maraisi waliostaafu na waliotimiza vigezo vya utawala bora," amesema Profesa Lipumba.

Amesema wakati huu ambao Rais Samia yuko kwenye fungate la urais anapaswa kujipanga, kujijenga kisiasa badala ya kutafuta maslahi.

"Iwe ni miaka minne na nusu au tisa na nusu atakayotawala, basi ajiwekee lengo la kupata tuzo. Ajiwekee lengo la kulinda na kuheshimu haki za binadamu na utawala bora, ukifika muda watu waone kuwa anafaa kupata tuzo ya Mo Ibrahim," amesema.

Pia Profesa Lipumba amemtaka Rais Samia atambue kuwa uchaguzi mkuu wa 2020 haukuwa halali na hivyo aanze mkakati wa mabadiliko ya katiba yatakayoleta tume huru ya uchaguzi.

Ameendelea kusema kwakuwa Rais Samia alikuwepo kwenye Bunge la Katiba anajua mabadiliko hayo yanawezekana.

"Bahati nzuri amemteua Profesa Kabudi (Palamagamba) kuwa waziri wa katiba na sheria. Ni matumaini yetu kwamba tuwe na katiba yenye maoni ya wananchi.”

"Ndani ya rasimu ya Jaji Warioba, kuna mfumo wa tume huru ya uchaguzi. Makamishna waombe wafanyiwe tathmini, sheria ya uchaguzi ibadilishwe iendane na rasimu ya katiba ili tuwe na tume huru maana hii iliyopo ni tume ya kupanga matokeo," amesema.

Kwa upande mwingine, Profesa Lipumba amemshauri kiongozi mkuu huyo wa nchi kuwapa mikataba ya utendaji mawaziri na watendaji wa serikali ili kupima utendaji wao na kuwawajibisha.

Huku akitoa mfano wa kukamatwa kwa aliyekuwa mkurugenzi wa Mamlaka ya Bandari (TPA), Deusdedit Kakoko, Profesa Lipumba amesema Rais Samia ameonyesha uwajibikaji.
Mo Ibrahim sasa hivi kawa kama mke wa pili wa Kagame kila tukio yuko pembeni yake🤣🤣🤣
 
Kiranga

JF-Expert Member
Jan 29, 2009
57,376
2,000
Rais arejeshe utawala bora kwa sababu ndicho kitu Watanzania wanataka na ndiyo kitu sahihi kufanya, si kwa sababu ya tuzo ya Mo Ibrahim.

Mo Ibrahim asingeanzisha tuzo, Lipumba angetaka rais asirejeshe utawala bora?

Mo Ibrahim akiifuta tuzo leo, Lipumba bado atamtaka rais arejeshe utawala bora?
 
DeepPond

JF-Expert Member
Nov 18, 2017
12,495
2,000
Kinachomuuma uyu mzee,

Marehemu alifariki kabla hajatimiza ahadi yake ya kumpatia angalau wabunge watano.
 
brazaj

JF-Expert Member
Jul 26, 2016
8,914
2,000
Mo Ibrahim sasa hivi kawa kama mke wa pili wa Kagame kila tukio yuko pembeni yake🤣🤣🤣

Kagame hawezi kupata tuzo ya Mo.

Tume ya Mo inahitaji utendaji haki ndiyo maana hiyo haikuwamo kwenye hesabu za mpendwa wetu sana - jiwe.
 
Bambushka

JF-Expert Member
Jan 9, 2020
2,534
2,000
Akafie mbele mchumia tumbo wahedi huyo. Yeye ameshashinda tuzo ngapi??
Prof Le'Pumba kabisa! Gademiti!
Tiyari anataka kunajisi utawala wa Raisi Samia,
Tena akome kujipendekeza na kimbelembele chake!
Wakati akiwa makamu hajawahi kumsemea ajitahidi awe raisi, sasa anamuhimiza ashinde tuzo, nyang'au huyu!

Everyday is Saturday............................... :cool:
 
zandrano

JF-Expert Member
Jan 24, 2017
2,526
2,000
Prof; sasa uzee umemkamata kwani hakumbuki kuwa mkataba uliopo ni ILANI YA CHAMA yenye kurasa 303?!

wanao takiwa kuitekeleza ilani hiyo ni Mawaziri, Makatibu wakuu, wakuu wa mikoa , wilaya, ma Ras na Ma Das, watendaji wote wa serikali wakishirikiana na wabunge na Madiwani pamoja na watendaji wa vijivji na kata.

ilani ya CCM pia ndio mkataba kati ya Serikali na wananchi, ikifika 2025 tutawahukumu kutokana na ilani hiyo,
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom