Sky Eclat
JF-Expert Member
- Oct 17, 2012
- 57,597
- 215,267
Rais Magufuli amtaka Mo Dewji kujali maslahi ya wafanyakazi wake kama Anavyoijali Simba
Rais Magufuli amemtaka Mfanyabishara Mohamed Dewji (Mo Dewji), kuhakikisha anajali maslahi ya wafanyakazi wake kama anavyofanya katika Timu ya mpira wa miguu ya Simba Sports Club ambapo amemsihi kwamba wafanyakazi hao nao wanastahili kupata maslahi yao.
Rais magufuli amesema ivho leo Alhamisi Agosti 1, alipokuwa akizungumza katika hafla ya uzinduzi wa Kiwanda cha Kusaga Nafaka cha 21st Century Food and Packaging, kilichopo Kurasini jijini Dar es Salaam, kinachomilikiwa na mfanyabiashara huyo.
“Mohamed Dewji ninakupongeza sana katika hili na ninakuomba uwajali wananchi wanaofanya kazi hapa hasa maslahi yao kwahiyo unapokuwa unaangalia maslahi ya Simba uangalie pia masilahi ya wafanyakazi wa 21st century food and packaging,” amesema.
Aidha ameiataka Kampuni ya Metl Group iliyopo chini ya mfanyabishara huyo kuachana na utaratibu walionao wa kuagiza ngano kutoka nje ya nchi na badala yake kuanza kulima ngano nchini kwani kwa kufanya hivyo itasawadia Watanzania wanaohitaji ajira.
“Ninatoa wito kwa Kampuni ya Metl Group chini ya Mohamed Dewji, nilipokuwa ninapewa maelekezo nmeambiwa mahindi yanatoka Tanzania ambayo yanatengenezwa tani 300 kwa siku lakini ngano inayotengeneza tani 1400 kwa siku inaagizwa kutoka nje hii tuibadilishe,” amesema.
“Katika maisha yangu nilikua ninafahamu kulikuwa na mashamba makubwa sana ya ngano kule Manyara lakini sasa hivi hayatumiki na kuna wakati wawekezaji wakijaribu wanachomewa moto sasa nitoe wito hata kwa Kampuni yako muanze kulima ngano kwani mtakuwa mmesaidia Watanzania wengi,” amesema.
Mhe. Rais Magufuli amefungua kiwanda cha kusaga unga wa mahindi na ngano cha 21st Century Food Packaging chenye uwezo wa kusaga tani 1,500 kwa siku.
▪Mo aahidi kumuunga mkono Mhe. Rais Magufuli kwa kuwekeza shil Bil 860 utakaozalisha ajira 100,000 ifikapo mwaka 2025

Kwa mshahara huu, Mo Dewji utajiri wako unatokana na unyonyaji wa wafanyakazi wako
Huwa najiuliza sana taasisi kama Forbes inatumia vigezo gani kumjua tajiri namba moja katika nchi husika. Wanashindwa hata kutembelea wafanyakazi wa kampuni za tajiri husika kuangalia hali zao nao zikoje? Juzi hapa nilileta bandiko kuhusu mishahara ya wafanyakazi wanaofanya katika kampuni za...
www.jamiiforums.com