Lipumba 'aisigina' CHADEMA bungeni

Lipumba 'aisigina' CHADEMA bungeni

Obesity

Senior Member
Joined
Dec 21, 2012
Posts
111
Reaction score
46
Chama Cha Wananchi (CUF), kimesema vurugu zinazoendelea bungeni zinasababishwa na Kambi Rasmi ya Upinzani inayoongozwa na Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe, kushindwa kujenga hoja na mbinu za kuwabana wabunge wa Chama Cha Mapinduzi (CCM).

Akizungumza jijini Dar es Salaam jana, Mwenyekiti wa CUF, Profesa Ibrahim Lipumba alisema wabunge wa Chadema wana tabia ya kufuata mfumo wa kwenda bungeni na hoja zinazobeba chama chao na si za Watanzania wote kama jinsi CCM wanavyofanya.

“Kambi rasmi ya upinzani imepoteza uwezo wa kujenga hoja za mashiko na mbinu madhubuti za kuwabana wabunge wa CCM bungeni na badala yake Chadema, wamekuwa na tabia mbaya ya kubeba chama chao,” alisema Profesa Lipumba.

Alisema kambi rasmi ya upinzani pia imeshindwa kulinda utaratibu mzuri wa kutetea masilahi ya umma bila jazba na hoja zenye mashiko kama ilivyokuwa miaka ya nyuma ilipokuwa ikiongozwa na CUF, Kiongozi huyo alisema kambi ya upinzani inapaswa ijipange upya kwa utaratibu na mikakati mizuri ya kuteta hoja za wananchi bila kuyumbishwa na wabunge wa CCM.

“Bunge usiwe uwanja wa kuonyesha mbwembwe za chama bali uwe uwanja wa kutetea haki za wananchi, wabunge wanapaswa wabadilishe mitazamo ya kuona bungeni ni sehemu ya kujionyesha kisiasa na chama chako kinafanya nini nje ya Bunge,” alisema Lipumba.

Alisema viongozi wa Serikali wanapaswa kubadilika kuhusu namna ya kutoa majibu bungeni.

Profesa Lipumba alisema mawaziri wengi wanakuwa wakitoa majibu mepesi katika maswali ya msingi yanayoulizwa na wabunge wa upinzani.

Alisema Bunge linatumia muda na pesa za walipakodi vibaya kwa baadhi ya wabunge kuwa na ubishi usiokuwa na tija, kutoleana matusi na wengine kuingilia hoja za wenzao bila sababu za msingi.

Profesa Lipumba pia alisema Spika wa Bunge, Anne Makinda amepoteza uwezo wa kuliongoza Bunge.



Source: Gazeti la mwananchi
 
Tangia CUF ijiunge na CCM, Lipumba amekuwa akianza kutoa pumba naye.
Hoja ya Mnyika ya maji darisalamu ilikuwa inataka kuleta maji kwa wanachama wa CHADEMA tu???
Hoja ya Nassari ya Elimu je, ilikuwa elimu kwa wana CHADEMA tu???
 
CUF ndoa yenu na magamba ndo iliwaponza hadi mkawa watu wa ndio mzee hata leo,waacheni chadema wakimbize
 
Asante profesor kwa kuliona hilo, hapa juzi kati niliweka uzi unaonyesha jinsi "wabunge wachadema wanavyokera sana" bungeni hawa mambumbu na waendeshwa na hisia wakaleta vioja kama walivyowabunge wao na kukosa hoja za kuwatetea wabunge wao matokeo yake wanaanza mbona mbona n wewe usubiri waje utakiona cha mtema miwa.
 
Eti huyu nae ni prof MB. Nasari alikuwa sahihi kumbe; Nonsense and contradicting comments from the Prof; Kama anakiri kuwa Speaker na Msaidizi wake wamekosa uhalali na uwezo wa kuliongoza Bunge maana yake ni kwamba, bunge letu linaenda kama kipofu. Kambi lasmi ya upinzani haina jinsi pale inapoona hakuna haki.

Huyu Prof, hajawahi kuingia Bungeni hata sikumoja na kutoa hoja zake inakuwaje anasema CHADEMA wameshindwa kwa sasa wakati, sisi tunaona CHADEMA inawatetea wananchi na Kuiwajibisha serikali isiyosikivu ya CCM. Asichotaka kujua huyu Prof, ni kwamba wabunge wa CCM wamegeuka kuwa serikali na hawaangaishi vichwa vyao kufikiria bali kusubilia wakati wa kuunga hoja na ndipo usikia ndiyooooooooooooooooooooo. Kambi lasmi ya Upinzani bungeni inafanya kile watanzania tuanachokitegemea, yeye Lipumba asubirie kugombea tu uraisi ambao ni msindikizaji siku zote.

Hana jipya huyu Lipumba na hakuna lolote ambalo anaweza kuwaeleza watanzania kuwa ameifanyia nchi hii tofauti na kugombea urais kila terms, CUF imepoteza mwelekeo na si chama cha upinzani tena bali Chama Swaiba wa CCM. CHADEMA Shikilia hapo hapo ndipo ushindi ulipo 2015 general election.

Hata CCM wawatumie CUF na kuvinunua vyama vidogo vidogo vya upinzani ili kuwademolarize, CHADEMA endelea kutwanga potepote, ukweli ni kwamba CCM na serikali yake wamebanwa na hawana ujanja tuendako.
 
Chadema alicho sema Lipumba ni Ukweli kabisa,mko na mawazo ya Chama zaidi hata hapa JF
 
The Truth An Offense But Not A Sin"
 
Mzee Lipumba uzee umemfika tayari na mshale wa umri upo saa moja kasoro. Kama cvyo basi ndoa inakulevya mzee wangu.
 
Mke kumtetea mumewe ni jambo la kawaida. Hongera Pro uchwara.
 
The truth is there even you ignore it. Time will tell no matter what situation occurs .revolution must occurs
 
Prof, ungetutolea mfano wa hizo hoja ambazo ni kwa ajili ya cdm, ndio maana CUF ilishindwa kuendelea kuwa chama kikuu cha upinzani.

In short, kama cuf ilikuwa ikijenga hoja bungeni iweje leo cdm iwazidi na kuwa chama kikuu cha upinzani?

Kama hata walishindwa kupambana na propaganda ya udini ndio wataweza kujenga hoja za kuikwamua tanzania na umaskini?

Ni bora CUF watoe boriti katika jicho lao ndio waone kibanzi kwenye jicho la cdm.
 
Lipumba katika observations zao hajaona kabisa ya Mwigulu na Lusinde?
 
Namheshimu sana Prof. Lakini naona kajichanganya mno katika hoja hii.
Anaposema wapinzani wanashindwa kujenga hoja halafu wakati huo huo anasema mawaziri wanatoa majibu mepesi, hapo anamaanisha nini?
Majibu mepesi kwa maswali gani? Waliyojiuliza mawaziri wenyewe au kutoka upinzani. Kama ni kutoka upinzani amewezaje kujua kwamba jibu ni jepesi iwapo swali halikuwa na hoja ya msingi kwa wa-Tz kama alivyodai yeye mwenyewe?

Binafsi nimeona Mh. Lipumba ameshindwa kujieleza.
 
Tangia CUF ijiunge na CCM, Lipumba amekuwa akianza kutoa pumba naye.
Hoja ya Mnyika ya maji darisalamu ilikuwa inataka kuleta maji kwa wanachama wa CHADEMA tu???
Hoja ya Nassari ya Elimu je, ilikuwa elimu kwa wana CHADEMA tu???

Hoja zinaletwa kihuni,kila mbunge anamatatizo yake jimboni kwake.nafikiri ugeni wa bungeni,na wote waliofukuzwa ni mara yao ya kwanza kuingia bungeni.
 
Back
Top Bottom