Nyaka-One
JF-Expert Member
- Oct 27, 2013
- 4,628
- 6,563
Mwaka 1983 hautasahaulika kwa mashabiki wengi wa muziki hapa Tanzania na duniani kote baada ya mwanamuziki mkongwe Lionel Richie aliyejiengua kutoka kundi la "The Commodores" kuachia wimbo wake wa "All Night Long" uliokuwa katika album yake ya pili baada ya kuachana na hilo kundi lake la "The Commodores".
Kwa watanzania na katika nchi zingine za Afrika Mashariki kunakozungumzwa zaidi kiswahili wimbo huo ulipendwa zaidi kutokana pia na kuwa na baadhi ya maneno ya kiswahili kama "karamu" na "jambo, jambo". Lakini pia watu wengi kutoka Afrika Mashariki kutokana na kukunwa vilivyo na wimbo huo walikwenda mbali zaidi kwa kudai kwamba kulikuwa na maneno mengine ya kiswahili kama "Japo unipe senti moja". Binafsi pamoja na kuwa na umri mdogo kwa wakati huo niliamini kwamba hayo maneno ni kweli yalikuwa katika wimbo huo.
Hata hivyo ukweli ni kwamba maneno pekee ya kiswahili yaliyo katika huo wimbo wake maarufu ni "karamu" na "jambo" na hakuna maneno mengine zaidi. Maneno yaliyokuwa au yanayodaiwa kuimbwa kwa kiswahili wakati sivyo yanakwenda hivi "Tam bo li de say de moi ya, Hey Jambo Jumbo" ambayo ndiyo yalidhaniwa kuwa ni "Japo unipe senti moja".
Lionel Richie mwenyewe katika moja ya interview zake aliwahi kukiri kwamba hayo maneno (Tam boli de say de moi ya, Hey Jambo Jumbo) hayakuwa na maana yoyote (gibberish).
Kwamba wakati anaandika wimbo huo alimtafuta rafiki yake mmoja aliyekuwa akifanya kazi Umoja wa Mataifa ili amsaidie kumwandikia maneno machache kutoka katika moja ya lugha za Afrika lakini huyo rafiki yake kutokana na ubize aliokuwa nao akadai angehitaji wiki kadhaa mbele kuyapata maneno hayo.
Kwa vile Lionel Richie alikuwa akiyahitaji maneno hayo kwa haraka ili kukamilisha wimbo wake hakuweza kusubiri zaidi hivyo ikabidi yeye mwenyewe abuni maneno yake ya kuweka na hivyo akajikuta ameweka maneno hayo yasiyo na maana yoyote japo kiukweli yaliweza kuunogesha sana wimbo wenyewe.