Lini Vyuo Vikuu binafsi nchini Tanzania vitazalisha wanataaluma wa kada ya uprofesa wa kutosha?

mbinguni

JF-Expert Member
Jan 2, 2013
2,746
1,051
Tàasisi nyingi BINAFSI hadi sasaivi havijaweza kuzalisha kada ya uprofesa vyenyewe. Kwanini haviwekezi ktk kuzalisha watu wao na badala yake kutegemea wastaafu wa vyuo vikuu vya serikali?

Nawasilisha.
 
Tàasisi nyingi BINAFSI hadi sasaivi havijaweza kuzalisha kada ya uprofesa vyenyewe. Kwanini haviwekezi ktk kuzalisha watu wao na badala yake kutegemea wastaafu wa vyuo vikuu vya serikali? Nawasilisha.
Ni ukiritimba na roho mbaya tu ya wahadhiri na walimu wa chuo kikuu UDSM

Zamani chuo kikuu wanaanza watu 200 kozi ya Medicine wanamaliza 2

Wengine wanafelishwa makusudi

Kozi ya Economics wanaanza 50 wanamaliza 3

Walimu waliona sifa wanafunzi kufeli hapo Udsm, Mwalimu alijitapa na kujisifia kuwa mwaka huu wote mtarudi kufanya Supplementary

Walimu wa udsm wengi walisoma kwa Taabu na wametoka kwenye maisha màgumu sana hivyo kukufanya wewe usome Degree miaka sita kwao wanaona furaha

Chanzo cha mambo yote ni chuo kikuu cha kwanza udsm the kufelisha watu makusudi ili wabaki Professor wachache tu nchini

Chuo ilikuwa ni kama sehemu ya vita vile, Usichezee ukatili wa walimu wa zamani hasa hapo UDSM

Alipoingia Rais Kikwete mwaka 2005 ndio alibadilisha mambo hasa chuo cha UDSM

Kikwete alianza kuwekeza na kusomesha walimu kwa mkopo nafuu ili wakafundishe shule za kata

Kikwete alipiga mkwara walimu wa Udsm kuwa Waache ushamba na ujinga wa miaka ya 1970 Yeye akiwa mwanafunzi kikwete

Alitoa onyo kali pale Udsm wakati huo kuwa Tanzania ina watu wengi lakini Wasomi wachache kwa ujinga wa Professor wa UDSM

Alitoa maneno yale makali mbele ya Thabo Mbeki na aliyatoa kabla ya hapo alipokuwa Rais

Walimu wa Udsm walifelisha watu makusudi kabisa, Walitaka wabaki wenyewe tu

Bila Kikwete hali mpaka Leo ingekuwa mbaya zaidi,

Kikwete aliruhusu vyuo Private vianze kupokea wanafunzi wengi wa Degree ya ualimu na alihakikisha pesa za Loan Board zinafika vyuo vya private ikiwemo ada

Nina mengi ya kukusimulia

Rais hayati Magufuli akaja akaanza kutibua tena vyuo binafsi kwa kuanza kuvifungia kirahisi rahisi tu

Tume rudi tena nyuma hatua elfu moja
 
Ni ukiritimba na roho mbaya tu ya wahadhiri na walimu wa chuo kikuu UDSM

Zamani chuo kikuu wanaanza watu 200 kozi ya Medicine wanamaliza 2...
Magufuli aliharibu sana. Je , ni kwanini SASAIVI hasa kwenye vikuu vya binafsi kama SAUT wanao wana taaluma wachache sana kwa ngazi ya uprofesa? Nini sababu?
 
Back
Top Bottom