Wana jamii forum, jukwaa la sheria nauliza lini sheria inakubaliwa kutungwa leo na kutumiwa kuhukumu matukio yaliyopita. Nauliza kwa sababu siku za nyuma nilikuwa nimeajiriwa na shirika moja la umma, tukaelewana niache kazi na kulingana na sheria za wakati ule, Nilikuwa na haki ya kupewa pension ya kila mwezi mpaka mwisho wa maisha yangu. Baada ya miaka 5 ikatungwa sheria ya kufuta sheria ile na kutaka mtu akiacha kazi kama hajafikia umri 55, asipewe pension mpaka ifikie 55. Ajabu sheria hiyo mpya ikatukumika hata kwa waliostaafu kabla ya kutungwa sheria hiyo mpya.
Sasa nauliza kwa wataalamu wa sheria, ni haki kukumbwa na sheria hiyo mpya? Ni katika mazingira yapi sheria mpya inaweza kutumika kuhukumu matendo yaliyopita na inaenda nyuma kwa muda gani?
Sasa nauliza kwa wataalamu wa sheria, ni haki kukumbwa na sheria hiyo mpya? Ni katika mazingira yapi sheria mpya inaweza kutumika kuhukumu matendo yaliyopita na inaenda nyuma kwa muda gani?