Lini bunge letu litafanya kazi zake za kibunge

sammosses

JF-Expert Member
Jan 24, 2011
1,682
1,110
Watanzania wanashindwa kuelewa ni lini bunge letu tukufu litakaa na kufanya kazi zake za kibunge!Ni mshangao ambao wananchi wana jiuliza kila siku kwa bunge letu kuacha kufanya kazi zake za kibunge na kuwa chombo cha utetezi dhidi ya tuhuma mbalimbali za kifisadi zinazo iandama serikali ya CCM.

Ina tia uchungu kuona kiti cha spika kina tumika vibaya kuhakikisha serikali haibanwi na bunge kwa hoja zenye kuleta tija na mapinduzi ya kiuongozi ndani ya serikali.Hali kama hii imekuwa ikipelekea kila anaye chaguliwa kupitia mfumo huu wa kulindana kuchafuka na kupoteza haiba yake kutokana tu na kulinda mfumo ambao ameukuta.

Kibaya zaidi wanao umia ni wananchi ambao wanatumika kama chombo cha kupitishia watu wasio na maslahi kwa jamii husika kwa kuwachagua na kushindwa kutekelza ahadi walizo ahidi.Tumeona bunge letu linaelekea kumaliza kikao chake cha kupitisha bajeti za mapato na matumizi ya serikali kwa mwaka 2012/13,swali hapa ni je bajeti hizo zimemnufaishaje mwananchi wa kawaida kiasi cha kuweza kuliamini bunge na kuona ndiyo kimbilio pekee na chombo cha kumtetea mwananchi huyu.


Wabunge wanaelekea kuhitimisha vikao vyao vya kuongeza maslahi katika mifuko yao kwa posho za sleeping and dogging allowance,sasa ni zamu yetu wananchi kuhoji mara watakapofika majimbo kutuletea mrejesho wa waliyoyajadili na kuleta tija kwa mustakabali wa maendeleo ya nchi na watu wake.

Kikubwa zaidi tunachotegemea kutoka kwao ni uhamasishaji wa sensa ya kitaifa inayokwenda kufanyika muda mfupi ujao.Si ajabu wengine wasionekane hata majimboni kwa kigezo cha kamati za bunge.Ifike wakati wanaporudi kutoka mjengoni tuwaulize wametuwakilisha vipi ilihali wakulima wanazidi kunyanyasika kwa kushindwa kupatiwa bei nzuri ya mazao yao.


Mrejesho huu wa bunge toka bungeni ni sawa kabisa na Riwaya katika vitabu vya secondary pale Obi Okonkwo alipotumwa na jamii yake kwenda kusoma ili alete ukombozi na fikra kwa kusoma sheria ambayo itatumika kuepuka unyanyasaji katika jamii yake lakini yeye alipofika kwenye mjengo wa huko abroad aliamua kuachana na kilichompeleka na kusomea mambo yasiyo na tija kwa jamii yake,tena mbaya zaidi kwa kupuuza hata mila za kwao na kutukuza mila za kigeni.

Mfano huu hauna tofauti na wabunge wetu,tunachowatuma wanakiweka pembeni na kuendeleza ya kwao na kusahau kazi kubwa inayo wasababisha kuwa ndani ya mjengo.Wananchi tusipobadilika tutaendelea kuchezewa na kupoteza haki zetu za kuchagua watu tuwatakao kwa maslahi ya taifa na watu wake.


Kuchezewa huku ni pamoja na dhihaka zinazofanywa na wabunge wetu kwa kudai waongezewe posho kwa kuwa tu posho hizo haziishi hapo mjengoni bali huwa zinawafikia wapiga kura wao.Tuamke tufikirishe akili zetu na kuacha habari ya kutumiwa kama chombo cha manufaa kwa wachache na tujue haki zetu za kuwachagua zinatumika vizuri?
 
Umeongea vizuri, lakini itabidi usubiri hadi bunge letu liwe na wabunge wapinzani wa kweli zaidi ya 66% ya wabunge wote
 
Umesomeka mkuu. Lakini huku kwetu, mbunge hakuchaguliwa na wananchi, kwani hata mkurugenzi aliyebandika matokeo feki alikimbia halmashauri yake hadi leo.

Hivyo mbunge tuliyenaye, hawajibiki kwetu bali kwa mamlaka iliyomweka madarakani.

Kwa hali hiyo halaumiwi, wala hata mikutano haitishi. Kwa wale mliochagua wabunge wenu, mna haki ya kuhoji hilo, na kama mlifanya makosa 2010, msirudie 2015.
 
Ukweli haupingiki,wabunge wengi walichakachua na ndio maana wamekubali kuwa rubber stamp ndani ya bunge kwa kupitisha mambo ovyo ovyo,wengi wao wakisikia bunge limevunjwa wanaweza kufa kwa pressure maana hata kama ukihitisaha uchaguzi leo wana uhakika wa kutorudi na wengi wao wana madeni ambayo hawajayalipa kutokana na ama kukopa kwa ajili ya kucheza rafu kwenye uchaguzi au waliuza nyumba zao wakitegemea kulipa wakiwa bungeni.

Jambo jingine hata wale vinara wakupinga ufisadi nao kwa sasa hawakunjui,walikuwa wakiimba kijamaa kumbe upande wa pili walikuwa wakicheza kibepari matokeo yake leo wameaibika mchana kweupe pepepe.

Bunge pia kupitia kiti cha Spika kiache dramatize,haiwezekani kiti kitumike kuwataka baadhi ya wabunge kutoa ushahihidi wa tuhuma zao kisha zikipelekwa kwenye kamati ya maadili zinaishia huko huko bila wananchi kujuzwa,mchezo huo ni mchafu una stahili kukemewa.Vinginevyo mh.Spika atumie busara kuliko kutuletea mchezo wa maigizo ndani ya bunge.

Wale wabunge wa kmitaifa wasikatishwe tamaa na kushambuliwa na wabunge wenzao,kwani kuvunjika kwa koleo si mwisho wa uhunzi,pamoja na uchache wao sisi wapiga kura ndiyo tunapambanua nani wabunge maslahi na nani wabunge wa kitaifa,japokuwa kuna baadhi ndani ya tenga lililooza bado wanafurukuta ila kwa ushauri wa bure lila na **** hazitengemani ni bora wangejitoa wakakaa pending angalu kurudisha imani kwa wapiga kura wao.



Umesomeka mkuu. Lakini huku kwetu, mbunge hakuchaguliwa na wananchi, kwani hata mkurugenzi aliyebandika matokeo feki alikimbia halmashauri yake hadi leo.

Hivyo mbunge tuliyenaye, hawajibiki kwetu bali kwa mamlaka iliyomweka madarakani.

Kwa hali hiyo halaumiwi, wala hata mikutano haitishi. Kwa wale mliochagua wabunge wenu, mna haki ya kuhoji hilo, na kama mlifanya makosa 2010, msirudie 2015.
 
Umeongea vizuri, lakini itabidi usubiri hadi bunge letu liwe na wabunge wapinzani wa kweli zaidi ya 66% ya wabunge wote

Kabla hatujapata bunge la wapinzani 66% ni bora tuonyeshe kuwa tuna chukia kuona yanayo endelea kwani haikuwa dhamira yetu kuona wana tugeuka wakati tuliwaamini tukawapa dhamana hiyo ya kutetea wananchi na kuisimamia serikali.
 
Sasa kama mnachagua wabunge ka mwigilu mnafikiri bunge litakua kama bunge kweli? Chagueni wabunge wenye sifa na stahili ya kua wabunge
 
Sasa kama mnachagua wabunge ka mwigilu mnafikiri bunge litakua kama bunge kweli? Chagueni wabunge wenye sifa na stahili ya kua wabunge
Tatizo kubwa nadni ya bunge letu ni kwa wabunge kutokujitambua na kukubali kutmika kuidhalilisha elimu yao,hawezekani mbunge msomi ana simama kuchangia hoja utumbo mtupu,kisha ana jinadi na kujiita msomi.Uko wapi uprofesa wao ilihali wakishindwa kuitetea taaluma yao kisa tu wameonya kwenye party caucus. Hatuwezi kuwa na wabunge waliokosa hoja ndani ya bunge mpaka nje ya bunge na kubaki kuwashambulia wabunge wenzao kwa kuwa tu wao wapo kwa ajili ya maslahi ya chama.Bunge la leo halina tofauti na vijiwe vya kahawa,limekuwa kijiwe cha kupiga soga na kelele ambazo zinapelekea bunge letu kuonekana kama Mwafrika bar. Tunawasubiri kwa hamu mtupatie mrejesho wenu kwa yale tuliyowatuma vinginevyo nasi tuna tafuta kanuni na sheria itakayo turuhusu kusaka kura kwa ajili ya kuwang'oa majimboni kabla ya muda wenu kutimia kwa makosa ya kutugeuka wananchi na kukubali kutumika kama jamvi la kupitishia maovu ndani ya nchi
 
Ni mpaka wabunge watakapo jitambua kila mtu kwa nafas yake. Mtaongea yooote lakini bila wabunge kujitambua na bila ya kuwa na elimu ya uraia kujua wajibu wao ni nini, itakuwa sawa na kumpigia mbuzi gitaa acheze.
 
Bunge letu litafanya kazi za kibunge pale tu CCM kitakapokuwa chama cha upinzani.
 
Pia ni muhimukupitia mchakato huu wa katiba kubanaisha kazi za bunge kwa ufasaha na nini hatua zitachukuliwa iwapo bunge litawageuka wananchi ili liwezwe kuwajibishwa kuliko tunachokiona hivi sasa.Serikali itekeleze majukumu yake bila kuingilia uhuru wa mihimili mingine,maana hali hii ikikithiri inaweza kuleta machafuko makubwa ndani ya nchi kwani wanao umia ni wananchi nasi serikali.Pia bunge litumike kuikemea serikali pale inapoingilia mhimili mwingine kama mahakama
 
Takribani mwaka toka uzi huu unapigia kelele bunge lakini halibadiliki,tufanyeje wananchi ili bunge lijue tumechoshwa na yanayoendelea ndani ya bunge
 
Back
Top Bottom