Lindi: Kikosi kazi Chaundwa kuchunguza mauwaji ya Wanawake wawili walionyongwa na kubakwa

Neiwa

JF-Expert Member
Feb 17, 2012
728
633
JESHI la Polisi mkoani Lindi, limeunda kikosi kazi kwa ajili ya kufuatilia na kubaini mauaji yanayofanywa dhidi ya wanawake katika Wilaya ya Nachingwea mkoani humo yaliyoibuka hivi karibuni.

Kwa mujibu wa taarifa ya Kamanda wa Polisi mkoani humo, Renatha Mzinga, LEO Jumanne Mei 27, 2014 amesema mauaji hayo yamefanyika kati Mei 21 hadi 25, 2014 ambapo wanawake wawili katika Kata ya Nambambo Wilayani humo walikutwa wakiwa wamekufa kwa kunyongwa na kuchomwa vijiti sehemu za siri.

Mzinga, amesema uchunguzi wa daktari juu ya vifo hivyo umeonyesha kabla ya kuuwawa, marehemu, Shida Danford (19), mkazi wa kijiji cha Majengo ‘B’ Wilayani humo na Fatuma Barbabas (20), mkazi wa Majengo ‘E’ walibakwa na kuvuliwa nguo zote ambapo baada ya muda watuhumiwa waliwatelekeza kabla ya kunyongwa.

“Jeshi la Polisi tumeamua kuunda kikosi hicho baada ya kushtushwa na matukio hayo mawili tena ambayo yanafuatana na kutokea kwa siku tunazohisi nimefuatana, sasa tusipolitilia mkazo hili suala linaweza kusababisha maafa makubwa hapo baadae” alikaririwa na FikraPevu.

Amesema wakati marehemu, Fatuna Barbanas (20), katika uchunguzi wa daktari ulionyesha kuwa alipigwa na kitu chenye ncha kali kabla ya kifo chake na kupelekea mauti kumkuta ambapo pia alikuwa amewekewa vijiti katika sehemu za siri bada ya kubakwa.

Mume wa msichana huyo, Omari Yohana (25-28), anashikiliwa na Polisi mkoani humo kutokana na kumtishia maisha mke wake, Futunata Barnabas, baada ya ndoa yao kuvunjika ili iwasaidie Polisi katika upelelezi wa tukio hilo.

“Huyu mwanaume wa huyu binti walifarakana siku chache silizopita kabla ya tukio la mauaji hayo, uchunguzi umeonyesha kuwa walikuwa na ugomvi wa kugawana Ufuta waliolima kwa pamoja baada ya mmoja wao kutaka kujinufaisha mwenyewe na wakati

wamefanyakazi pamoja, ikilinganishwa kuwa kipindi hiki ni cha kilimo hicho katika ukanda huu ambapo mwanaume huyo alimtishia mwenzake kuwa atamfanya kitu kibaya” alisema Mzinga

Kumbukumbu zinaonyesha kuwa siku za hivi karibuni kumekuwepo na wimbi la Wanawake kuuwawa kwa kunyongwa na kuchinjwa katika wilaya ya Butiama mkoani Mara, FikraPevu imewahi kuripoti matukio hayo, ambapo iliundwa timu maalum ya kuchunguza tukio hilo na Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini, IGP Ernest Mangu, katika Wilaya hiyoambapo wanawake nane (8) waliuwawa na baadhi ya watuhumiwa kufikishwa Mahakamani kwa kukiri kuhusika na mauaji hayo.

Chanzo: Lindi: Kikosi kazi Chaundwa kuchunguza mauwaji ya Wanawake wawili walionyongwa na kubakwa | Fikra Pevu | Kisima cha busara!
 
Back
Top Bottom