PreGE2025 Lindi: ACT Wazalendo wazindua 'Operesheni Linda Demokrasia' kupigania kurejeshwa kwa thamani ya kura kwenye Uchaguzi

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Joined
Apr 18, 2017
Posts
4,783
Reaction score
14,975
WhatsApp Image 2025-03-29 at 20.37.32_5361e228.jpg

WhatsApp Image 2025-03-29 at 20.37.32_2ef72bec.jpg

Chama cha ACT Wazalendo kimesema kuwa kipaumbele cha Chama hicho kwa sasa ni kupigania mageuzi ya mfumo wa uchaguzi na kurejesha thamani ya kura ya kila Mtanzania kwenye uchaguzi.

Msimamo huo umeelezwa na Kiongozi wa Chama Mstaafu wa ACT Wazalendo, Ndugu Zitto Kabwe, ambaye alikuwa mgeni rasmi katika Kongamano la Uzinduzi wa Operesheni ya Chama, Operesheni Linda Demokrasia, lililofanyika katika Jimbo la Lindi Mjini leo tarehe 29 Machi 2025.

Ndugu Zitto Kabwe amesema kwamba Operesheni Linda Demokrasia inalengo la kurudisha thamani ya kura kwa Mtanzania. Alisema haya akilaani ukiukwaji wa sheria na misingi ya haki katika chaguzi tatu zilizopita.

"Kwa chaguzi tatu mfululizo thamani ya kura imepotea. Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2019 hakukuwa na kura, takribani wagombea wote wa upinzani walienguliwa. Mwaka 2020 tuliona kwa mara ya kwanza kura feki zikozagaa hovyo barabarani. Mwaka 2024 wakafanya kama mwaka 2020" alisema Zitto Kabwe.
WhatsApp Image 2025-03-29 at 20.37.31_3e756546.jpg

WhatsApp Image 2025-03-29 at 20.37.33_37f8ba3a.jpg
Ndugu Zitto amesisitiza kuwa hoja kuu ya Operesheni Linda Demokrasia ni mageuzi katika Tume ya Uchaguzi ili kuhakikisha kwamba uchaguzi unakuwa huru, wa haki na wa kuaminika.

"Tume ya Uchaguzi yenye wajumbe kama Omari Mapuri ambaye amewahi kuwa Mwenezi wa CCM inawezaje kutenda haki kwa watu wote? Sheria ya sasa ya Tume Huru ya Uchaguzi imeweka utaratibu kuwa angalau wajumbe wa Tume ya Uchaguzi wapatikane kwa ushindani. Watu waombe na wafanyiwe usaili. Serikali ya CCM haitaki kutekeleza jambo ambalo wamelitunga wenyewe."

Zitto Kabwe amesema kutokana na kuvurugwa kwa demokrasia nchini, matokeo yake ni kuporomoka kwa uzalendo miongoni mwa wananchi.

"Kwa wizi wa kura CCM wanadhani wanatukomoa CCM. CCM wanalikomoa Taifa. Mapenzi kwa Taifa yanaporomoka, watu hawajivunii tena Utanzania, wanavumilia kwa sababu hawana pa kwenda." alisisitiza Zitto Kabwe.
WhatsApp Image 2025-03-29 at 20.37.34_d16922a8.jpg
Kwa upande wake, Makamu Mwenyekiti Bara wa ACT Wazalendo Ndugu Isihaka Mchinjita amewahimiza wananchi kupambana kuhakikisha kuwa misingi ya demokrasia nchini inarejeshwa.

"Kulinda demokrasia ni wajibu namba moja wa raia. Raia wanapokosa uhuru wa kuamua nani awe kiongozi wao wanakuwa watumwa ndani ya nchi yao," alisisitiza Ndugu Mchinjita.

Chama cha ACT Wazalendo kinaendelea na programu mbalimbali za Operesheni Linda Demokrasia ikiwemo Makongamano ya kufafanua dhana hiyo kwenye Mikoa mbalimbali na ziara kwa wadau mbalimbali wa demokrasia.

Imetolewa na Shangwe Ayo,
Naibu Katibu wa Habari, Uenezi na Mahusiano na Umma, ACT Wazalendo
29 Machi 2025
 
Zito anafanya siasa za kimkakati sana!yaani siasa za msimamo wa.kati!

Wakati chadema wanafanya siasa Kali za kushambulia!!!

KAZI ipo
 
Chama cha ACT Wazalendo kimesema kuwa kipaumbele cha Chama hicho kwa sasa ni kupigania mageuzi ya mfumo wa uchaguzi na kurejesha thamani ya kura ya kila Mtanzania kwenye uchaguzi.

Msimamo huo umeelezwa na Kiongozi wa Chama Mstaafu wa ACT Wazalendo, Ndugu Zitto Kabwe, ambaye alikuwa mgeni rasmi katika Kongamano la Uzinduzi wa Operesheni ya Chama, Operesheni Linda Demokrasia, lililofanyika katika Jimbo la Lindi Mjini leo tarehe 29 Machi 2025.

Ndugu Zitto Kabwe amesema kwamba Operesheni Linda Demokrasia inalengo la kurudisha thamani ya kura kwa Mtanzania. Alisema haya akilaani ukiukwaji wa sheria na misingi ya haki katika chaguzi tatu zilizopita.

"Kwa chaguzi tatu mfululizo thamani ya kura imepotea. Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2019 hakukuwa na kura, takribani wagombea wote wa upinzani walienguliwa. Mwaka 2020 tuliona kwa mara ya kwanza kura feki zikozagaa hovyo barabarani. Mwaka 2024 wakafanya kama mwaka 2020" alisema Zitto Kabwe.
Ndugu Zitto amesisitiza kuwa hoja kuu ya Operesheni Linda Demokrasia ni mageuzi katika Tume ya Uchaguzi ili kuhakikisha kwamba uchaguzi unakuwa huru, wa haki na wa kuaminika.

"Tume ya Uchaguzi yenye wajumbe kama Omari Mapuri ambaye amewahi kuwa Mwenezi wa CCM inawezaje kutenda haki kwa watu wote? Sheria ya sasa ya Tume Huru ya Uchaguzi imeweka utaratibu kuwa angalau wajumbe wa Tume ya Uchaguzi wapatikane kwa ushindani. Watu waombe na wafanyiwe usaili. Serikali ya CCM haitaki kutekeleza jambo ambalo wamelitunga wenyewe."

Zitto Kabwe amesema kutokana na kuvurugwa kwa demokrasia nchini, matokeo yake ni kuporomoka kwa uzalendo miongoni mwa wananchi.

"Kwa wizi wa kura CCM wanadhani wanatukomoa CCM. CCM wanalikomoa Taifa. Mapenzi kwa Taifa yanaporomoka, watu hawajivunii tena Utanzania, wanavumilia kwa sababu hawana pa kwenda." alisisitiza Zitto Kabwe.
Kwa upande wake, Makamu Mwenyekiti Bara wa ACT Wazalendo Ndugu Isihaka Mchinjita amewahimiza wananchi kupambana kuhakikisha kuwa misingi ya demokrasia nchini inarejeshwa.

"Kulinda demokrasia ni wajibu namba moja wa raia. Raia wanapokosa uhuru wa kuamua nani awe kiongozi wao wanakuwa watumwa ndani ya nchi yao," alisisitiza Ndugu Mchinjita.

Chama cha ACT Wazalendo kinaendelea na programu mbalimbali za Operesheni Linda Demokrasia ikiwemo Makongamano ya kufafanua dhana hiyo kwenye Mikoa mbalimbali na ziara kwa wadau mbalimbali wa demokrasia.

Imetolewa na Shangwe Ayo,
Naibu Katibu wa Habari, Uenezi na Mahusiano na Umma, ACT Wazalendo
29 Machi 2025
Huyu alikuwa anachambua reports za CAG kila mwaka lakini toka alambe asali hana habari, sasa hivi wakimpa ubunge kwisha habari yake atakaa kimya mpaka maslahi yake yatakapo guswa tena. Hana tofauti ni madalali wengine.
 
Kiongozi mstaafu wa Chama cha ACT WAZALENDO ZITTO KABWE amesema Siasa ya Tanzania imerudi nyuma kule ilikotoka kutokana na kuminywa Kwa demokrasia

Zitto ameyasema hayo kwenye kongamano la viongozi wa mkoa wa lindi ambalo limezindua operesheni Linda demokrasia yenye lengo ya kurudisha thamani ya kura inayopigwa na wananchi.

Aidha ZITTO ameeleza kwamba lengo la operesheni hiyo ni kurejesha heshima ya kura Kwa kuwa kwenye chaguzi tatu zilizofanyika hakukua na kura kabisa.

Awali makamu mwenyekiti wa ACT WAZALENDO bara ISIHAKA MCHINJITA ameeleza kwamba operesheni hiyo ina nia ya kuhakikisha watanzania ndio wenye dhamana ya nchi yao.

act1.jpg
act2.jpg
 
Hawa nao kwa kuzunguuka tu hawajambo, hiyo kwa interpretation nyingine ni kwamba wamemuelewa LISSU; na wamekuja kwa mlango wa nyuma lakini ni ile ile NO REFORM NO ELECTION.
 
Back
Top Bottom