Badala ya SUMA kuagiza matrekta kutoka India, wangelitoa oda ya aina hii ya matrekta ili kuchangia gharama za utafiti na uboreshaji wakeTrekta hii ina uwezo wa kulima ekari 5 kwa siku,linasaga na kukoboa nafaka kilo 300 kwa siku.Pia linatumika kama pampu ya maji. Ilibuniwa na kutengenezwa na Dr Patric Jonathan mwaka 2008 mkoani Arusha katika kituo cha zana za kilimo na ufundi vijijini (CAMARTEC).Picha ni leo mchana katika Banda la CAMARTEC kwenye viwanja vya Mnazi Mmoja katika Maadhimisho ya Wiki Ya Utumishi wa Umma. Picha na Victor Makinda
Tatizo tukikubali kila kitu kitengenezwe Tanzania na kila mtu atajua bei ile 10 % ya watafunaji itatokea wapi mkuu Nyambala.Nnavyoijua bongo hizo innovations zinaishiaga kwenye maonyesho tu, kuna wale jamaa pale mlimani IPI wana compactor waliitengeneza mwishoni mwa miaka ya tisini lakini huwa inaonekana kwenye maonyesho tu, baada ya hapo stoo, kufuli. Sijaelewa bado tatizo ni nini.
Mh! mbona ame-copy na lu-paste Valmet?....kubuni kitu kipya it should be different from what is existing....ni wazi hata hayo matairi alinunua dukani akaja kufunga humo....Bado sana aisee!!
Mh! mbona ame-copy na lu-paste Valmet?....kubuni kitu kipya it should be different from what is existing....ni wazi hata hayo matairi alinunua dukani akaja kufunga humo....Bado sana aisee!!
Nyumbu......tutafika tu,
Siyo kila mahali panahitaji umwagiliaji. Usukumani matreka yametumiwa tangu miaka ya 1950 kwenye kilimo cha pamba na kulikuwa na ufanisi mkubwa. Matatizo yalianza baada ya kuuwa vyama vya ushirika vya awali na kuingiza haya mabodi kama Bodi ya Pamaba ambayo yalileta ufisadi unaoendelea mpaka leo kwa kuwakandamiza wakulima. Teknolojia yakisasa inahitajika hata bila ya umwagiliaji. Lakini mkulima wa kawaida ataweza kuinunua wakatii bei anazopewa ni za wizi wa mchana?Tatizo siyo zana za kilimo ila kilimo cha uhakika sasa kama utakuwa na zana bora za kisasa halafu mkishalima shamba mnasubiria mvua hapo mi sioni kama kuna ufanisi wowote.pamoja na serikali kuendelea kubuni zana mpya na za kisasa mbinu hizo zingetakiwa ziende sambamba na uendelezaji wa mabonde ya umwagiliaji.