Lijue tatizo hili hatari la umeme linaloitwa voltage surge


T

twaleeb

JF-Expert Member
Joined
Oct 13, 2016
Messages
237
Likes
69
Points
45
T

twaleeb

JF-Expert Member
Joined Oct 13, 2016
237 69 45
>>>> LIJUE TATIZO HILI HATARI LA UMEME LINALOITWA VOLTAGE SURGE LINALOWEZA KUSABABISHA MADHARA MAKUBWA NYUMBA UNAYO ISHI AU OFFISINI UNAPOFANYIA KAZI

Inaandikwa na TWALEEB BIN AUF

NINI MAANA YA VOLTAGE SURGE
Voltage Surge pia Kwa lugha ya kitaalamu hujulikana kama Transient Voltage.Ni tukio la mabadiliko ya kiwango cha umeme(voltage) au Mkondo wa umeme(Current),tukio ambalo hutokea kwa muda mfupi sana kwa kasi ya 1/6 ya mzunguko wa umeme(voltage cycle).
Voltage surge kawaida hupotea ndani ya 50 microseconds wakati current surge hupotea ndani ya 20 microseconds.Hii ni kwa mujibu wa ANSI C62.1991.

DALILI ZA UWEPO WA VOLTAGE SARGE KATIKA NYUMBA YAKO
1.kupanda au kushuka ghafla kwa kiwango cha umeme nje ya kiwango cha kawaida
2.Kupanda kwa kiwango cha umeme zaidi ya kawaida kwa muda wa zaidi ya sekunde moja.(Mara nyingi husababishwa na radi)
3.Kuugua mara kwa mara kwa vifaa vy umeme ndani ya nyumba kama vile taa n.k.Vilevile kama unatumia Tubelight alafu ukaona kuna rangi nyeusi pembezoni mwa tubelight zako basi ujue unakabiliwa na tatizo hili.

NINI CHANZO CHA VOLTAGE SURGE
Vyanzo vya voltage surge vimegawanywa katika makundi mawili.
(a)Vyanzo vya nnje ya nyumba
i.Radi .Radi huweza kuongeza umeme wa ziada katika power line hivyo hupelekea kutokea kwa voltage surge
ii.Kuwasha au kuzima umeme katika power station
iii.Kulegea kwa waya katika viungio vya kwenye nguzo n.k
iv.Matumizi ya transformer moja zaidi ya nyumba moja.Kama itatokea mmoja wa watu waliounganishwa katika transformer hiyo akafanya vitendo ambavyo vinasababisha uzalishwaji wa transient voltage basi huathili wale wote wanao tumia transformer hiyo.
Vitendo hivyo ni kama vile Uchomeleaji,uendeshaji wa motor kubwa n.k

(b)Vyanzo vya ndani ya nyumba
i.Kulegea kwa viungo vya waya za wiring katika nyumba.
ii.Matumizi ya vifaa vifuatavyo katika nyumba yako-:
-Photocopiers
-PC Power Supplies
-Laser Printers
-Electronic Ballasts
-Welders
-Power Factor Correction Equipment
-Power Supplies
-Temperature Controllers
-Motor Controllers
-Pumps
-Inverters
-Compressors
-Generators
-Variable Speed Motors
-Standard Electric Motors
-High-Frequency Lighting Power Supplies

NINI MATOKEO YA VOLTAGE SURGE?
1.Umeme unatumika mwingi sababu vifaa vinapata sana moto hivyo vinajiongeza resistance ambapo hupelekea kutumika sana kwa umeme(Luku kuisha bila ufasaha)
2.Kuungua kwa vifaa vya umeme ndani ya nyumba mara kwa mara
3.Vifaa vinavyo tumia umeme vinakua vinapata moto sana
4.Energe servers na Fluorescents Tube lights zinaungua mara kwa mara
5.Husababisha kuungua kwa wiring cables mwishowe nyumba kuungua.
6.Vifaa vya umeme vinashindwa kufanya kazi vizuri.
7.Mikwaruzo ya sauti katika vifaa vitoavyo sauti kama vile TV na Radio.

NAMNA YA KUONDOA TATIZO LA VOLTAGE SURGE
Watu wengi wamekuwa wakiishi na tatizo hili bila kujijua katika nyumba zao,Wengi huangaika na vitu vidogodo tu wanapo ona moja ya dalili nilizo zitaja hapo juu.Tatizo hili limekuwa sugu kwasababu wengi hawalijui na hivyo inpotokea dalili kama hizo hapo juu watu hufikilia maamuzi mepesi sana mfano kubadilisha Earth Load ya nyumba alafu ndo basi.
Tatizo la voltage surge lipo nchi nyingi,na imekua moja ya jambo linalo umiza vichwa wafanyabiashara wa vifaa vya electronics ambapo wengi sasa wameanza kutengeneza mifumo ya kuzuia vifaa vyao visiadhirike na tatizo hili.Ndio maana unaweza kuona kifaa kimeandikwa "Volatage Surge protected).

Zifuatazo ni njia za kuodoa voltage surge katika nyumba yako(Hii ni rahisi tu kwa yale matatizo yanayo tokea ndani ya nyumba na sio nje ya nyumba kwani kwa Tanzania mwenye kibali cha kushugulikia line za umeme nje ya nyumba ni TANESCO TU.)
1.Kagua wiring yako kama ina loose connection au laa
2.Uwe na utaratibu wa kuwasha kwanza vifaa vitumiavyo umeme mkubwa kwanza ndipo ufate vile vidogo
3.Jaribu kukitambua kifaa kinacho leta hali hio.
4.Epuka kutumia vifaa feki vya umeme kama vile switch,wire n.k
5.Njia nzuri ni ya ya kutumia MOV na Heat Resistor
Fuse unwaeza kuweka ya ampere 15Amp

>>>><ANGALIZO:
UMEME UNAUA USIJISHUGULUSHE NA KUFUNGA AU KUFUNGUA KIFAA CHA UMEME KAMA HUNA TAALUMA YA UMEME

>> JE, UNAHITAJI USHAURI,UNATATIZO LOLOTE LINALOHUSU UMEME AU VIFAA VYA UMEME* , *JE UNAHITAJI VIFAA BORA NA IMARA VYA UMEME KWA AJIRI YA AJIRI YA NYUMBA YAKO AU OFFICE YAKO*, JE, UNAHITAJI HUDUMA YA EMERGENCY NYUMBANI AU OFFICE YAKO,

>>*WASILIANA NA SISI AL-TIMIMY TECHNICIAN ILI TUKUSHUGULIKIE MATATIZO YA UMEME KATIKA NYUMBA YAKO*, namba ya simu +255622001223

>> *Kama upo TANZANIA na unahitaji au unashida ya kutatuliwa tatizo la aina yoyote linalohusu umeme kwenye nyumba unayoishi, unayojenga/uliyojenga tutafute kwa namba* +255622001223 na TUTAKUJA SEHEMU ULIPO

>> HUDUMA ZETU.

> Ukaguzi salama wa Umeme.
>Uchoraji ramani za wiring ya aina zote za nymba.
>Tunatoa hudama za ushauri wa kitaalamu kuhusu umeme kiujumla.
>Tunafanya marekebisho/matengezo ya vifaa vya umeme vya aina zote.>Tunafanya marekebisho ya wiring za zamani au zilizochoka za nyumba za aina zote.
>Tunafunga CCTV camera.
>Ufungaji wa vifaa vya solar na uuzaji wa vifaa solar
>Tunafunga na kutengeneza Aircondition, Friji, Frezeer, na vifaa vyote vyakuzalisha baridi.
*Umalizapo kusoma tafadhari sana unaombwa kushare kwa wengine ili wapate kuomba maana kazi ni muhimu*.
 
Avatar mok

Avatar mok

JF-Expert Member
Joined
Mar 7, 2012
Messages
7,578
Likes
7,458
Points
280
Avatar mok

Avatar mok

JF-Expert Member
Joined Mar 7, 2012
7,578 7,458 280
Asante kwa Elimu.

Mkuu nina shida hii, nyumba ilizimika umeme tokea juzi hadi leo lkn nyumba zoote zinazonizunguka zina umeme, nimeriport emergence tanesco wanacho niambia tu nisubiri mafundi wao nisizime simu yangu ili wakija wawasiliane nani (asa unajiuliza kwanini isizime wakati umeme ndani hamna ‍♂️‍♂️‍♂️)

Angalia iyo picha nimepiga sasaivi, hiyo taa inawaka lakini hapo hata uchomeke charger simu haichajishi wala taa haziwaki, ni hizi mita za remote.

Nikipiga namba 200 umeme utawaka kama kwa sekunde moja alafu inafifia na kuzimika.

Point ni kwamba sijui tatizo ni nini, linasababishwa na nini...

Ukizingatia vyombo vilivyoumdwa kutoa huduma (tanesco) kila siku ni karenda..

Labda unipe elimu pia juu ya hii ishu...

Asante
 

Attachments:

T

twaleeb

JF-Expert Member
Joined
Oct 13, 2016
Messages
237
Likes
69
Points
45
T

twaleeb

JF-Expert Member
Joined Oct 13, 2016
237 69 45
Asante kwa Elimu.

Mkuu nina shida hii, nyumba ilizimika umeme tokea juzi hadi leo lkn nyumba zoote zinazonizunguka zina umeme, nimeriport emergence tanesco wanacho niambia tu nisubiri mafundi wao nisizime simu yangu ili wakija wawasiliane nani (asa unajiuliza kwanini isizime wakati umeme ndani hamna ‍♂️‍♂️‍♂️)

Angalia iyo picha nimepiga sasaivi, hiyo taa inawaka lakini hapo hata uchomeke charger simu haichajishi wala taa haziwaki, ni hizi mita za remote.

Nikipiga namba 200 umeme utawaka kama kwa sekunde moja alafu inafifia na kuzimika.

Point ni kwamba sijui tatizo ni nini, linasababishwa na nini...

Ukizingatia vyombo vilivyoumdwa kutoa huduma (tanesco) kila siku ni karenda..

Labda unipe elimu pia juu ya hii ishu...

Asante
Hili tatizo linawapata wengi ila kiufupi mara nyingi linakua ni tatizo la meter yao inafanya km kufreeze na km tatizo ni meter io inabidi ucheze na tanesco
 
T

twaleeb

JF-Expert Member
Joined
Oct 13, 2016
Messages
237
Likes
69
Points
45
T

twaleeb

JF-Expert Member
Joined Oct 13, 2016
237 69 45
Tumeongeza na huduma ya ufundi wa dishi
Wote mnakaribishwa
 
T

twaleeb

JF-Expert Member
Joined
Oct 13, 2016
Messages
237
Likes
69
Points
45
T

twaleeb

JF-Expert Member
Joined Oct 13, 2016
237 69 45
Tunatoa offer ya Service bure ya Aircondition kwa wateja watano wa mwanzo na wateja 10 watalipia nauli tu
NYOTE MNAKARIBISHWA
 
Evelyn Salt

Evelyn Salt

JF-Expert Member
Joined
Jan 5, 2012
Messages
48,184
Likes
39,524
Points
280
Evelyn Salt

Evelyn Salt

JF-Expert Member
Joined Jan 5, 2012
48,184 39,524 280
Tunatoa offer ya Service bure ya Aircondition kwa wateja watano wa mwanzo na wateja 10 watalipia nauli tu
NYOTE MNAKARIBISHWA
Nahisi hapa kwangu pia kuna shida ya umeme, make unatumika unit 4 kwa siku, nlimuita fundi akasema normal, hivi inawezekana ikawa normal kweli???
Vitu vinavowashwa mara nyingi ni friji ndogo 1 feni 3
 
donbeny

donbeny

JF-Expert Member
Joined
Aug 19, 2013
Messages
3,424
Likes
2,305
Points
280
donbeny

donbeny

JF-Expert Member
Joined Aug 19, 2013
3,424 2,305 280
Thanks for Important Info Mkuu,,,,
 
nasmapesa

nasmapesa

JF-Expert Member
Joined
Jul 31, 2014
Messages
3,976
Likes
3,036
Points
280
nasmapesa

nasmapesa

JF-Expert Member
Joined Jul 31, 2014
3,976 3,036 280
Hii elimu nzuri sana aisee
 

Forum statistics

Threads 1,249,422
Members 480,661
Posts 29,697,907