Wapenzi wa jukwaa la MMU nimeitwa kwenye kikao cha usuluishi.Jirani na Rafiki yangu wa karibu sana walikuwa na mgogoro wa muda mrefu katika ndoa yao mara kadhaa vikao vya usuluishi vimefanyka bila kupatikana suluhisho la kudumu.Tatizo nililokuwa nikilijua ni tabia ya Rafiki yangu kuzaa na wanawake tofauti tofauti,tayari alikuwa na watoto wanne kwa wamama tofauti.
Nilipoitwa kwenye kikao nilijua hili suala la kuzaa hovyo hovyo lingechukua nafasi kubwa,lakini mambo niliyokutana nayo kwa kweli yalikuwa si ya kawaida.
Mke anadai tatizo la mume kuzaa nje ya ndoa si muhimu kwake wala halimpi taabu,kwanza alishamruhusu baada ya kuchoshwa na tabia yake ya kupenda kunako mchezo wa 6 x 6 kila mara bila kuchoka.Mwanzo wa ndoa yao alidhani labda ni ugeni na kutokuzoeana (baada ya kupewa ushauri na wanawake wazoefu) lakini hali hiyo iliendelea hadi kugeuka kero.Jamaa akirudi nyumba akimkuta wife anaongea na wanawake wenzake umwita kwa hasira utadhani kuna jambo muhimu anataka kumweleza akiingia mlangoni anakumta jamaa keshavua nguo ....... Akiwa anapika jamaa liko jikoni haliwazi ugali wala mboga linauliza kwa hasira hiyo biashara ya kupika itamalizika saa ngapi !.
Naomba wenye uzoefu wa haya maswala ya 6 x 6 hasa upande wa kina Dada,je hii tabia tunaweza kusema ni kero au starehe.