Ligi ya vodacom na siasa za bongo. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ligi ya vodacom na siasa za bongo.

Discussion in 'Sports' started by kasyabone tall, Sep 20, 2009.

 1. k

  kasyabone tall JF-Expert Member

  #1
  Sep 20, 2009
  Joined: Sep 13, 2009
  Messages: 255
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 33
  Ligi ya vodacom na siasa za bongo.
  Jana kwa mara ya pili toka ligi ya bongo ianze nimeangalia mechi ya yanga na mtibwa, kwa mara ya kwanza niliangalia mechi ya yanga na simba pale taifa. Nilikatishwa tamaaa kabisa, sijui ni tatizo langu peke yangu yaani ukizoea kuangalia mechi za nje runingani , halafu ukaangalia mechi zetu hapa nyumbani unaona kama unapoteza muda wako bure. Nilikuwa nawalaumu sana wale wanaoendekeza mechi za man u baada ya kungalia yanga na simba za hapa nyumbani lakini kwa sasa nimegundua kwa nini hawapendi mambo ya kwetu. Ngoja niwape kidogo story za uwanja wa jamuhuri morogoro. Kwa kuanza mimi ni mshabiki wa simba kwa kuaminishwa enzi za utoto kuwa simba ndio taifa kubwa, nashangilia tu kwani wakati nipo mtoto nilishuhudia jamaa anatupa redio kisa yanga kafungwa na simba. Mimi nikaapa hapa SIMBA sitoki. Jana nilifika uwanjani saa kumi na nusu na kukuta mpira umeanza basi mimi sijui wapi manakaa simba na wapi wanakaa yanga. Nikajichomeka mpaka mahali nilipoamini kuwa naweza kuona vizuri kumbe niko katikati ya wakereketwa wa yanga, sasa mimi nilikuwa sijui nikaona jamaa mmoja wanamsukuma toka juu ya jukwaa baada ya kuona kipindi cha kwanza bila bila. Nikauliza kulikoni nikaambiwa hule ni mdudu, jamani mdudu kivipi? Jamaa akajibu kwa ukali mshabiki wa simba. Nikasema hii balaa sasa anauhusiano vipi na matokeo ya uwanjani? Nikajua ndo mambo yetu ya bongo yetu. Kikubwa zaidi nikaangalia wahudumu wa huduma ya kwanza cha ajabu kila mtu alivaa kivyake na mmja kiatu kilikuwa kimeachana katikati. (nikaona hawa watu hawako siliasi). Sasa ukatokea mgogoro pale nilipo kaa watu wamemngangania jamaa eti ni mdudu (jamaa alikuwa jirani yangu) nusura apigwe mpaka pale alipojitambulisha kwa msg za kwenye simu yake jinsi alivyokuwa akitukanana na waandi hi kwa sababu ya kuandika vibaya yanga. Sasa nikageukia kwa waandishi wa habari da vifaa ni duni kupita kiasi, basi nikaendelea kupiga mayowe kama mshabiki wa yanga nisije hisiwa vibaya.( mambo ya bongo bwana). Sasa upande wa askari polisi ni hali mbaya zaidi kwani wao no kutwanga virungu tu mpaka mtu unaishi kwa kukosa uhuru kwa kweli wanakatisha tamaa kwenda uwanjani. Sasa kwa hali hii ambayo ukienda usalama wa kurudi nyumbani salama ni mdogo kuna haja kweli ya kwenda kuchangia kuinua vipato vya vilabu vyetu?
  Hali ya wachezaji ndio usiseme kwani afya zao ni dhoofu sana, sasa sijui dayati kwao ina matatizo. Lakini pia wanaonekana ni watumiaji wa madawa ya kulevya au pombe kali sana. Hapa kuna haja ya vipimo!!
  Kioja kingine ni pale mchezaji kaumia anawasiliana na kocha msaidizi wa kondic hawaelewani, kocha anafoka akiwambia wacheze kwa nguvu na wao wanamuonyesha ishara kuwa jamaa kaumia anataka kutoka. Nikawauliza washabiki wa yanga hivi mzungu (sina uwakika) anasikia kiswahili nikaona hawajanijibu na wamenuna. Basi nikajua pale lugha ni matatizo.
  Lakini nilienda mbali zaidi na kufikiri wachezaji wengi wamekimbia shule pia nimewahi soma na wachezaji wengi wao ni mbumbu darasani. Sasa nikajiuliza kama darasani hawaelewi sasa kocha watamuelewa vipi?
  Sasa alipoingia abromovic wa bongo Manji basi hapo palitokea vionjo vya kila aina kwani wengine walishangilia huku wengine wakiimba kuwa fisadi papa ameingia. Sasa hizi siasa bwana ebu tuwachie mafisadi, sasa kama wanaingia mpaka kwenye mpira sijui nini hatma ya soka ya bongo.
  Cha ajabu zaidi ni matusi yanayotukanwa uwanjani, yaani kila mtu utatukanwa kwa njia moja au nyingine., mwingine anatukana wanasimba bila kujua inawezekana hata babake au mamake ni mwanasimba. Wengine refa, wengine hata mgeni wa heshima, na hata kamisaa wa mchezo.
  Tabia ya ulalamishi ni wimbo wa watanzania, maana hata pale tulipofungwa na kuondolewa na zambia watu walilia na refa bila ya kujilaumu wenyewe kwa kushindwa kurinda goli lao. Kwa matusi anayotukanwa refa kama refa anayechezesha ni ndugu yako usiende uwanjani kwa matusi hayahesabiki, pia usiende na mtoto wala mkeo lolote laweza kutokea.
  Ninajua kuwa wabongo wanajifanya much know maana kila mtu anajifanya refa, eti refa kachemsha hata mtoto wa la kwanza naye analalamika sasa ukimuuliza umesomea wapi kuchezesha mpira hajui. Lakini hiyo ndio bongo yetu bwana. Kuna mengi mazuri ya kujifunza kwa wenzetu ni kuiga kurusha chupa uwanjani tu. Soka yetu inahitaji mengi marekebisho kama sio matengenezo kuanzia kwa wanamichezo mpaka wachezaji. la sivyo itakuwa duni milele
   
Loading...