Ligi Kuu Tanzania bara yasimamishwa

Ligi Kuu Tanzania bara yasimamishwa

exalioth

JF-Expert Member
Joined
Jun 22, 2016
Posts
2,395
Reaction score
4,152
Serikali kupitia Waziri Mkuu Kassim Majaliwa imetangaza kusimamisha mchezo yote.

Waziri Mkuu akiongea na Watanzania kupitia vyombo vya habari amesema:

"Tumesitisha michezo yote inayokusanya makundi ya watu kama vile Ligi Kuu Tanzania, Ligi Daraja la Pili, Ligi Daraja la Kwanza na michezo ya Shule za Msingi (UMITASHUMTA), michezo ya Shule za Sekondari (UMISETA) na ya wafanyakazi"

Sitisho hili linajiri siku moja tangu agundulike mgonjwa wa kwanza wa corona nchini huko mkoani Arusha akiwa ametokea nchini Ubelgiji.
 
Kwani mwenye ligi si ni BODI YA LIGI au ile dhana ya Serikali kutoingilia michezo haingii ktk dhana hiii?
 
Nilikuwa nawaza kupiga hat trick mechi ijayo. Wana bahati sana.
 
Back
Top Bottom