Ligi Kuu Bara: Simba 2-2 KMC FC - Uwanja wa Mkapa, Sept 07 2022

Ghazwat

JF-Expert Member
Oct 4, 2015
23,718
66,262
Patashika ya Ligi Kuu Tanzania Bara kuendelea kupigwa leo 07/ 09/ 2022 ambapo Mnyama Mkali Mwituni Simba SC anakiwasha dhidi ya KMC FC kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa Jijini Dar es salaam.

Hii huenda ikawa ni mechi ya kibabe sana kupigwa, hasa ukizingatia Simba SC kuhitaji ushindi maridhawa ili kuweza kurudi kwenye uongozi wa Ligi Kuu, huku KMC wakitafuta walau ushindi wa kwanza kwa Simba SC baada ya kuwa na rekodi mbaya pindi wanakutana na Simba SC.

Kaimu Kocha Mkuu Suleiman Matola amesema kuwa hakuna mechi rahisi.

"Maandalizi yetu yanakwenda vizuri kabisa kwa kuuchukulia umhimu mchezo wa kesho (leo) KMC si timu rahisi, ni timu ngumu, lakini tumeangalia umhimu wa mechi hiyo kuhakikisha tunapata matokeo ya ushindi". amesema Matola.

Naye Kocha msaidizi Ahmad Ally wa KMC FC amesema kuwa wamejiandaa kwa asilimia 90.

"Maandalizi kwa ujumla yapo asilimia 90 na imebaki asilimia 10 kwa kesho (leo) uwanjani, tunakwenda kucheza na, timu bora, timu ambayo ina mbinu na ukiangalia wachezaji wake kwenye zone yoyote wanaweza kufanya lolote, lakini tutaangalia yale mapungufu yao ili tufanyie kazi yale ambayo tumejiandaa kwetu". amesema Ahmad.

Yooote ni ndani ya viunga vya Benjamin Mkapa ambapo dakika 90 kuamua. Kumbuka mchezo ni kuanzia saa 1: 00 Usiku..Usikose Ukapata Simulizi.

Kulitaka Mwana Kulipewa Mwana

===============

00' Naaam mpira umeanza Uwanja wa Mkapa | Simba SC 0-0 KMC FC

02' Phiri Goooooooooooooaaal gooal

Moses Phiri anahesabu bao la kwanza kwa shuti kali likimuacha golikipa Balora akishangaa.

07' KMC FC wamepata Kona ambayo haikuzaa bao, mashambulizi yanaendelea kwa pande zote mbili


10' Phiri yupo chini akipatiwa matibabu, ameinuka mpira unaendelea.

18' Ame anapiga mbele kumtafuta Kijiri, lakini beki za Simba SC zinakaa imara.

Sakho anajaribu kuipenya ngome ya KMC lakini mabeki wanakataa

25' Almanusura Simba SC wapate bao, kichwa kinachezwa na golikipa Balora.

28' Sakho anapiga Krosi, golikipa Balora anapangua, Okrah anapiga shutii anakosa, ilikuwa nafasi nzuri kwa Simba.

Awesu anaingiza ndani mpira lakini Ouattara anakataa

Kijiri anaonyeshwa KADI ya Njano kwa kumchezea madhambi Sakho ni Free Kick kuelekea KMC FC.

Simba SC wamepata Kona ambayo haikuzaa bao, kichwa mparazo cha Phiri kinatoka nje na kuwa goal kick.

37' Emmanuel Mvuyekule anapiga, looo lakini refa anasema ni Offside.

40' Majogoro yupo chini baada ya kufanyiwa madhambi na Kanoute ni mpira wa adhabu kuelekea Simba.

43' Kanoute anaonyeshwa KADI ya Njano kwa mchezo mbaya, ni Free Kick kuelekea Simba, inapigwa kulee lakini wanakosa.

45+2' Kuelekea kuwa mapumziko, Simba wanapata Free Kick nafasi nzuri kwa Simba, Okrah anapiga shutii lakini golikipa Balora anadaka.

Naaam mpira ni mapumziko ambapo Simba wapo mbele ya bao moja kwa bila dhidi ya KMC FC

HT: Simba SC 1-0 KMC FC

Naaam kipindi cha pili kimeanza huku KMC FC wakifanya mabadiliko, Ameingia Matheo Anthony

47' Matheo Goooooooooooooaaal gooal,

Matheo anasawazisha baada ya Israel kurudisha mpira hafifu na kumkuta Matheo na kuweka Kimiani.

50' Okrah anapiga shutii lakini golikipa Balora anadaka bila wasiwasi

KMC FC wamepata Kona ambayo haikuzaa bao, ambapo Awesu anapiga Krosi na kutoka nje na kuwa goal kick.

55' Kanoute anaonywa kwa mara nyingine kww mchezo mbaya | Simba SC 1-1 KMC FC.

57' Goooooooooooooaaal gooal George William anaipatia KMC FC bao la pili

Okrah ametoka na ameingia Bocco upande wa Simba SC, na ametoka Kapama na ameingia Mzamiru

65' Bocco katika nafasi nzuri lakini shutii lake linachezwa na Beki Ame.

Phiri anapiga shutii kali, lakini linambabatiza beki wa KMC FC

Ameingia Kibu na ametoka Kanoute upande wa Simba SC, huku Sakho akifanyiwa faulo

74' Ilikuwa piga nikupige lango la KMC FC, baada ya Krosi ya Bocco upande wa kulia, golikipa Balora yupo chini baada ya kupata rabsha.

77' Mohamed samatta ameingia upande wa KMC

Phiri anaangushwa eneo la box refa anakataa, anasema hapana penalty

80' Bocco anapiga kichwa, lakini inakuwa mboga kwa golikipa Balora, Sakho anatoka na ameingia Kyombo

Kenny Ally ameingia kuchukua nafasi ya Emmanuel Mvuyekule, huku golikipa Balora akionyeshwa Kadi ya Njano kwa kupoteza muda.

89' Kyombo Goooooooooooooaaal gooal Habibu Kyombo anasawazisha. Simba SC 2-2 KMC FC

90+3' kuelekea kumalizika kwa mchezo, hatari langoni kwa KMC, lakini wanaondosha hatari ile

Naaam mpira umekwishaaaaaa ambapo Simba SC na KMC FC wamegawana alama kwa kufungana mabao mawili kwa mawili

FT: Simba SC 2-2 KMC FC

.... Ghazwat...
 
Wiki ya kurudi kwenye mbio za ubingwa wa Ligi Kuu na Dejan Georgijevic atakuwepo kukinukisha
20220907_143314.jpg
 
Kila la kheri KMC.. hao Makolo washazoea kugawa URODA.. kwahiyo nyie Leo endeleeni kuwakaza tu
 
Back
Top Bottom