Ligi Kuu Bara | Simba SC 3-1 KMC FC | Uwanja wa Mkapa | Juni 19, 2022

Ghazwat

JF-Expert Member
Oct 4, 2015
23,718
66,262
Ikiwa wamethibitishwa na Shirikisho la Soka Barani Afrika CAF kuwa ni wataalamu wa kusakata Kabumbu Nchini Tanzania, Wekundu wa Msimbazi, Simba SC leo Juni 19, 2022, watakuwa kwenye Dimba la Benjamin Mkapa kupambana na vijana wenye vipaji, wenye kuweka mpira chini, Klabu ya Kinondoni Municipal, KMC FC.

Simba SC ambayo kila kitu kizuri kinaegemea upande wao, ubora wa Timu na Quality ya mchezaji mmoja mmoja, hivyo ni ngumu kwa KMC kuzuia Simba SC kupata ushindi na hasa ukizingatia kuwa KMC wamekuwa wakipata wakati mgumu kupata ushindi wanapokutana na Simba SC, ambapo kwenye michezo mitano ya mwisho, Simba ameweza kuibuka na matokeo ya ushindi.

KMC FC wao wanaamini kwenye kupishana kwenye Uwanja, na huenda wakaja na mfumo wa 4-3-3 kuweza kuwabana Simba SC kuanzia katikati ya uwanja, ambapo KMC watakapopata mpira kutoka kwa mpinzani ni rahisi kwao kufanya shambulizi la haraka sana kuelekea eneo la lango la mpinzani ambapo kama safu ya ulinzi kama itakuwa imesogea kwa juu wanaweza kukuathibu.

Yote kwa yote dakika 90 mchezo kuamua.. Kumbuka mchezo ni kuanzia saa 1:00 Usiku.. Usikose Ukaadithiwa.

Kulipewa Mwana.....Kulitaka Mwana

Simba SC kwenye mchezo wa leo, watatumia kumuaga Kiungo wao Left Footer Magician, Rally Bwalya mtaalamu wa pasi za kudondosha nyuma ya mabeki, ambaye Simba walitangaza kufikia makubaliano ya kumuuza.
FVn7peJXoAETbxI.jpg

Kikosi cha Simba dhidi ya KMC, leo Juni 19, 2022
FVnpHKwWIAAqg0u.jpg

Kiungo wa Simba, Bwalya anatarajiwa kucheza mchezo wake wa mwisho kabla
ya kuondoka Simba baada ya kupata ofa ya kuelekea katika klabu nyingine.


Timu zinaendelea kupasha misuli hapa kwenye Uwanja wa Mkapa, Dar es Salaam.
FVoFSQgWUAInmu8.jpg

Kikosi cha KMC dhidi ya Simba, leo Juni 19, 2022

Naaam mpira umeanza Timu zote zikifanya mashambulizi kwa kasi..!

05' Simba waliweza kupenya ngome ya KMC FC lakini, Bwalya na Kibu wanashindwa kutumia nafasi

10' zimekatika huku Awesu akijaribu kupiga shuti kumtafuta Miraji lakini Wawa anakaa imara.

15' Simba wamepata Kona ambayo haikuzaa bao, huku mashambulizi yakiwa makali na kukoswa bao hapa

Inapigwa kulee lakini golikipa Beno anadaka bila wasiwasi, huku akiwaambia wachezaji wake namna gani

20' Bado milango ni migumu, KMC wako vema sana kwenye eneo la ulinzi, wanahakikisha hakuna hatari yoyote.

25' Awesu anapiga shutii lakini, mpira unatoka nje ya lango na kuwa goal kick, KMC wameamka sasa

Matheo anakosa nafasi nzuri ya kufunga, mpira unaambaa ambaa kule, ilikuwa nafasi nzuri ya kufunga kwa KMC

Simba wanamiliki sasa, pasi za hapa na pale, kwake Mzamiru anapigaa loooo anababatiza ukuta wa kmc

30' Shikalo anapiga shutii mbele kuleee na anauwahi Henock, na anamuachia Beno

38' Bwalya anapiga shutii lakini, mpira unambabatiza beki wa KMC, hakuna maajabu yoyote kwa sasa

Kibu Denis anakosa nafasi nzuri ya kufunga, ilikuwa nafasi murua

42' Goooooooooooooaaal gooal

Hassan Kabunda anaipatia KMC bao la kwanza | Simba SC 0-1 KMC FC

45+2' Kuelekea kuwa mapumziko

Bwalya yupo chini baada ya kupata rabsha, haya mpira unaendelea Shikalo anaanza kuleee

Naaam mpira ni mapumziko ambapo Simba wapo nyuma kwa bao moja

HT: Simba SC 0-1 KMC FC

Kipindi cha pili kimeanza huku Simba SC wakifanya mabadiliko.. Ametoka Kanoute na ameingia Banda

Krosi ya Banda Kibu anapiga kichwa lakini golikipa Shikalo anadaka bila wasiwasi

Inapigwa krosi Kabunda anatokea na kuondosha hatari ile, huku Simba wakipata kona ambayo haikuzaa bao

51' Kibu Goooooooooooooaaal gooal

Kazi murua kutoka kwa Sakho anapangua mabeki kama wooote na kupiga Krosi na kumkuta Kibu akamalizia | Simba SC 1-1 KMC FC


Banda anajaribu kupiga shuti lango la KMC FC, lakini golikipa Shikalo anadaka

Simba wameamka kipindi cha pili kwa mashambulizi zaidi kuliko mwazo

60' Kadi ya Njano kwa Kibabage baada ya kumchezea madhambi Sakho

KMC wanajiandaa kufanya mabadiliko. Ametoka Miraji na Awesu na wameingia Kenny na Hilal

62' Sakhooo Goooooooooooaaal goal

Simba SC wanaandika bao la pili kupitia kwa Sakho | SIMBA SC 2-1 KMC FC

Simba SC wanaliandama lango la wapinzani, hatari kulee KMC wanazubaa

65' Henock Goooooooooooooaaal gooal

Simba SC wanapata bao la tatu kupitia kwa Henock kwa kichwa | SIMBA SC 3-1 KMC FC

KMC wamepoa sasa, kuliko kipindi cha kwanza..Huku Kibu Denis akitoka nje na nafasi yake imechukuliwa na Kagere.

74' Kabunda anajaribu kupenya ngome ya Simba lakini anatolewa kwenye Reli

KMC wanashambuliwa vibaya mno, uwezo wa kupata bao lingine upo. Beno anaanza kuleee kwake Wawa

Counter Attack lango la Simba, lakini Kijiri anakuwa Offside

Haya Umiliki wa Simba SC katikati ya Uwanja, Biriani kama yoote KMC mambo mazito

83' Ametoka Sakho na Nyoni na nafasi zao zimechukuliwa na Lwanga na Jimmyson upande wa Simba

KMC wanajenga mashambulizi kutoka chini ya lango lao, wanarudisha kwa Shikalo, Shikalo anapiga kulee kumtafuta Kijiri

88' Ametoka Bwalya na ameingia Mhilu upande wa Simba, KMC wanafanya shambulizi kali Matheo anapiga shutii Beno anadaka.

90+3' Kuelekea kumalizika kwa mchezo

Kagere anapiga shutii lakini linapaa nje ya lango ilikuwa nafasi nzuri

Naaam mpira umekwishaaaaaa ambapo Simba wanaibuka na ushindi wa mabao matatu kwa moja

FT: SIMBA SC 3-1 KMC FC

....... Ghazwat......
 
Matola hana vyeti. CAF wanataka kocha mwenye cheti daraja "A"
Ni rahisi tu mbona, inafanyika kama ilivyokuwa kwa Gomes. Gomes hakuwa na vigezo vya CAF ila Simba waka pretend kuwa Gomes ni kocha msaidizi pamoja na Matola halafu Hitimana ndiye kocha mkuu kwavile ana vyeti stahiki. Hivyo hivyo kwa Matola alindwe kama alivyolindwa Gomes.
 
Back
Top Bottom