El Magnifico
Member
- Dec 26, 2010
- 14
- 0
Hellow wana JF jukwaa la MMU,
Mwenzenu sasa ni kijana mkubwa, umri miaka 29 nimechoka kukaa peke yangu, i need to have someone we can cherish this life together.
Mwenzenu sitafuti mpenzi tu, natafuta mwanamke wa kuoa na nasikia harufu ya kumpata JF. Hata kama sio member, kama unafahamu mtu mwenye sifa hizi hapa chini, we ni-PM niunge nae bana. Nimechoka maisha peke yangu.
Sifa :Jamani mwenye sifa na vigezo hivi ndie niko tayari akuje sasa tuanze safari hii ya maraha
Mwenzenu sasa ni kijana mkubwa, umri miaka 29 nimechoka kukaa peke yangu, i need to have someone we can cherish this life together.
Mwenzenu sitafuti mpenzi tu, natafuta mwanamke wa kuoa na nasikia harufu ya kumpata JF. Hata kama sio member, kama unafahamu mtu mwenye sifa hizi hapa chini, we ni-PM niunge nae bana. Nimechoka maisha peke yangu.
Sifa :Jamani mwenye sifa na vigezo hivi ndie niko tayari akuje sasa tuanze safari hii ya maraha
- Uwe tayari kuchukua majukumu (ready to bear parental obligation). kama akili haijakomaa na huamini uko tayari kubeba majukumu kama mama wa watoto na pia wa mtoto mkubwa (yaani El Magnifico)basi hunifai. mimi niko tayari kuchukua majukumu ya kutunza watoto na mtoto mkubwa (yaani mama yao
- Uwe angalau kidato cha sita: Mwenzenu sijasoma sana, lakini nina elimu ya kutosha kujidai mbele ya watu kuwa nami nimesoma. Nina kashahada tu kamoja hivi kutoka chuo fulani hapahapa bongo. Hata kama una elimu ya kidato cha 6 hukubahatika kuendelea na utakuwa na sifa nyinginezo we njoo tu mama, nitakusomesha wakati tukiendelea na majukumu ya kifamilia. Degree level preferably.
- Uwe uliewahi kujeruhiwa na mapenzi: Japo ni sifa isiyo njema ila mie naitaka mwenzenu. Niliumizwa na mapenzi baada ya kuwa tayari kuoa mwaka huu mwanzoni lakini kwa sababu ambazo sijazijua mpaka leo, mwenzangu alikula kona kwa mtu mwingine. mpaka leo nikimuuliza sababu hana cha kuniambia zaidi ya kuwa "sikuwa chaguo" la wazazi wake. Najua maana ya kupenda sana halafu ukaangushwa na mapenzi. Nahitaji ambae pia anajua hivi na hayuko tayari kufanya mchezo
- Uwe mwepesi kunisikiliza na kunielewa: Hili ni muhimu. mimi napenda kumsiliza mtu, napenda wakati wote kumuelewa kabla sijamhukumu. kama uko unaweza kuelewa hili ni la muhimu. Nakuhitaji sana mwenye sifa hizi
- Awe Mkristo (sio jina au dini, ila matendo): Sina ubaguzi wa dini, ila ni muhimu kwangu kupata mtu ambae ni mkristo kama mimi ili kuondoa migongano isiyokuwa ya lazima. Sijalishi dini yako ila kama unaamini una mwenendo mzuri sawa na mafundisho ya dini na unaweza kuutunza vema moyo huu usiumie tena, wewe unanifaa.
- Asiwe Mpenda makuu: Jamani hapa pagumu. sina mpango wa kufanya harusi ya kuchangisha watu. Nilishaanza hili jaribio kabla ya kuangushwa na mapenzi. nataka kufanya harusi ndani ya uwezo wangu. Usiwaze harusi kubwa sana, waza tu ya kawaida itakayotupa uhalali wa kitaratibu na kijamii wa kuishi kama mke na mume. Hata hivyo, baada ya miaka mi-5 ya mafanikio ndani ya ndoa tutaporomosha jisherehe moja kubwa hujawahi kuona. Vilevile usiwaze maisha ya malkia wa uingereza. Usitake makubwa ambayo mwenzako sitaweza kuyafikia na unajua kwa wakati huo siwezi kuyafikia.
- Usiwe mwana-CCM. Kutofautiana ndani ya ndoa ni jambo lisiloepukika. nawaogopa wanawake walioko ndani ya CCM maana mwenyekiti wao (UWT) aliwaambia watunyime unyumba ambao ni anti-CCM. Sasa tusijesumbuana bure huko baadae kunyimanan unyumba kisa siiungi mkono CCM. Uwe tu chama chochote cha upinzani ni poa kabisa
- Awe anaependa kupendwa na anaejipenda: Wako wanawake wasiopenda kupendwa. Hata ukimpenda hapendeki. Hawa siwataki, nataka anaependwa kupendwa, alie tayari kupendwa. Mbali na hivi, awe pia mwenye kujipenda mwenyewe na wengine. SIpendi mwanamke asiejipenda. mwanamke ambae hawezi hata kupangilia nyumba yake wala hata kujisimamia mwenyewe. Am smart na napenda kila anaenizunguka awe smart. hii ni muhimu ili nisijekuta siku choo cha mtoto (pot) kimewekwa jikoni pamoja na vyombo vingine au vyombo vimewekwa juu ya kochi living room au nywele kwenye chakula.
- Uwe fighter na mwajibikaji binafsi: Napenda mwanamke mpambanaji. Mwanamke talented na anaejua kuwa yuko talented na ano uwezo wa kuthibitsha talent zake. i hate lazy women. Nina kipato sio kikubwa sana ila kinanipa uhakika wa kuuona mwisho wa mwezi bila pressure (given all factors remain constant na hakuna msiba wala kadi nyingi za michango ya harusi ya marafiki). Pia mimi ni mwajibikaji, napenda mtu awe anawajibika. Sipendi mwanamke wa kumuachia housegirl kila kitu. KAMA UNA KA UVIVU KIDOGO, TAMBAA MBELE usije.
- Maadili mema na nia njema ni msingi mkubwa: Nina ndoto kubwa za kimaisha. kuwa mtu mwenye heshima yangu ndani ya jamii kwa njia zilizo halali. Napenda niwe na mke mtulivu, msikivuu na ambae kimaadili yuko kwenye viwango vizuri. Hata kama maisha ya siku za awali hayakuwa matulivu, kama sasa hivi mambo ya utulivu yako juu basi unanifaa kabisa wewe. Am not interested on your past, am much more interested of your present and future. Hutahitaji kunithibitishia mimi mwenendo wako, ila moyo wako uwe mkweli na muwazi, ukiona unasita ya kuwa matendo na mwenendo wako hauendani na maadili, tafadhali tambaa mbele, hunifai. Naomba uwe mtu mwenye nia njema, sio nia ya kuumiza wengine.
Mwenzenu niko serious sitanii, ndo maana sijaandika kwenye jukwaa la Utani/Ucheshi, I AM MORE THAN SERIOUS
KAMA UNASIFA HIZO, Tafadhali karibia chumbani, ni-PM huko then nitakupatia majibu ya next step na kujibu maswali for any issue of concern bandugu
Kanuni inayotumika ni FIFS, kwa maana ya wakwanza watapatiwa kipaumbele. Usipoona ujumbe kwenye visitors message kwamba sasa maombi yamefungwa ujue bado application zinakaribishwa.
Nyongeza: Uwe na uhakika na sifa hizi kabla hujachukua next step, maana ni sehemu muhimu ya mkataba wangu na huyo atakae-qualify, any debasement itaniumiza na itanipa shida nisiyotaka maishani. KARIBUNI
HERI YA MWAKA MPYA KWENU NA MNIOMBEE MWENZENU NIUANZE VIZURI KWA KUMPATA PARTNER
WHO KNOWS THAT I CAN GET MY LIFE TIME PARTNER HERE?