Life time partner, are you there?? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Life time partner, are you there??

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by El Magnifico, Dec 31, 2010.

 1. El Magnifico

  El Magnifico Member

  #1
  Dec 31, 2010
  Joined: Dec 26, 2010
  Messages: 14
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hellow wana JF jukwaa la MMU,

  Mwenzenu sasa ni kijana mkubwa, umri miaka 29 nimechoka kukaa peke yangu, i need to have someone we can cherish this life together.


  Mwenzenu sitafuti mpenzi tu, natafuta mwanamke wa kuoa na nasikia harufu ya kumpata JF. Hata kama sio member, kama unafahamu mtu mwenye sifa hizi hapa chini, we ni-PM niunge nae bana. Nimechoka maisha peke yangu.


  Sifa
  :Jamani mwenye sifa na vigezo hivi ndie niko tayari akuje sasa tuanze safari hii ya maraha

  1. Uwe tayari kuchukua majukumu (ready to bear parental obligation). kama akili haijakomaa na huamini uko tayari kubeba majukumu kama mama wa watoto na pia wa mtoto mkubwa (yaani El Magnifico)basi hunifai. mimi niko tayari kuchukua majukumu ya kutunza watoto na mtoto mkubwa (yaani mama yao
  2. Uwe angalau kidato cha sita: Mwenzenu sijasoma sana, lakini nina elimu ya kutosha kujidai mbele ya watu kuwa nami nimesoma. Nina kashahada tu kamoja hivi kutoka chuo fulani hapahapa bongo. Hata kama una elimu ya kidato cha 6 hukubahatika kuendelea na utakuwa na sifa nyinginezo we njoo tu mama, nitakusomesha wakati tukiendelea na majukumu ya kifamilia. Degree level preferably.
  3. Uwe uliewahi kujeruhiwa na mapenzi: Japo ni sifa isiyo njema ila mie naitaka mwenzenu. Niliumizwa na mapenzi baada ya kuwa tayari kuoa mwaka huu mwanzoni lakini kwa sababu ambazo sijazijua mpaka leo, mwenzangu alikula kona kwa mtu mwingine. mpaka leo nikimuuliza sababu hana cha kuniambia zaidi ya kuwa "sikuwa chaguo" la wazazi wake. Najua maana ya kupenda sana halafu ukaangushwa na mapenzi. Nahitaji ambae pia anajua hivi na hayuko tayari kufanya mchezo
  4. Uwe mwepesi kunisikiliza na kunielewa: Hili ni muhimu. mimi napenda kumsiliza mtu, napenda wakati wote kumuelewa kabla sijamhukumu. kama uko unaweza kuelewa hili ni la muhimu. Nakuhitaji sana mwenye sifa hizi
  5. Awe Mkristo (sio jina au dini, ila matendo): Sina ubaguzi wa dini, ila ni muhimu kwangu kupata mtu ambae ni mkristo kama mimi ili kuondoa migongano isiyokuwa ya lazima. Sijalishi dini yako ila kama unaamini una mwenendo mzuri sawa na mafundisho ya dini na unaweza kuutunza vema moyo huu usiumie tena, wewe unanifaa.
  6. Asiwe Mpenda makuu: Jamani hapa pagumu. sina mpango wa kufanya harusi ya kuchangisha watu. Nilishaanza hili jaribio kabla ya kuangushwa na mapenzi. nataka kufanya harusi ndani ya uwezo wangu. Usiwaze harusi kubwa sana, waza tu ya kawaida itakayotupa uhalali wa kitaratibu na kijamii wa kuishi kama mke na mume. Hata hivyo, baada ya miaka mi-5 ya mafanikio ndani ya ndoa tutaporomosha jisherehe moja kubwa hujawahi kuona. Vilevile usiwaze maisha ya malkia wa uingereza. Usitake makubwa ambayo mwenzako sitaweza kuyafikia na unajua kwa wakati huo siwezi kuyafikia.
  7. Usiwe mwana-CCM. Kutofautiana ndani ya ndoa ni jambo lisiloepukika. nawaogopa wanawake walioko ndani ya CCM maana mwenyekiti wao (UWT) aliwaambia watunyime unyumba ambao ni anti-CCM. Sasa tusijesumbuana bure huko baadae kunyimanan unyumba kisa siiungi mkono CCM. Uwe tu chama chochote cha upinzani ni poa kabisa
  8. Awe anaependa kupendwa na anaejipenda: Wako wanawake wasiopenda kupendwa. Hata ukimpenda hapendeki. Hawa siwataki, nataka anaependwa kupendwa, alie tayari kupendwa. Mbali na hivi, awe pia mwenye kujipenda mwenyewe na wengine. SIpendi mwanamke asiejipenda. mwanamke ambae hawezi hata kupangilia nyumba yake wala hata kujisimamia mwenyewe. Am smart na napenda kila anaenizunguka awe smart. hii ni muhimu ili nisijekuta siku choo cha mtoto (pot) kimewekwa jikoni pamoja na vyombo vingine au vyombo vimewekwa juu ya kochi living room au nywele kwenye chakula.
  9. Uwe fighter na mwajibikaji binafsi: Napenda mwanamke mpambanaji. Mwanamke talented na anaejua kuwa yuko talented na ano uwezo wa kuthibitsha talent zake. i hate lazy women. Nina kipato sio kikubwa sana ila kinanipa uhakika wa kuuona mwisho wa mwezi bila pressure (given all factors remain constant na hakuna msiba wala kadi nyingi za michango ya harusi ya marafiki). Pia mimi ni mwajibikaji, napenda mtu awe anawajibika. Sipendi mwanamke wa kumuachia housegirl kila kitu. KAMA UNA KA UVIVU KIDOGO, TAMBAA MBELE usije.
  10. Maadili mema na nia njema ni msingi mkubwa: Nina ndoto kubwa za kimaisha. kuwa mtu mwenye heshima yangu ndani ya jamii kwa njia zilizo halali. Napenda niwe na mke mtulivu, msikivuu na ambae kimaadili yuko kwenye viwango vizuri. Hata kama maisha ya siku za awali hayakuwa matulivu, kama sasa hivi mambo ya utulivu yako juu basi unanifaa kabisa wewe. Am not interested on your past, am much more interested of your present and future. Hutahitaji kunithibitishia mimi mwenendo wako, ila moyo wako uwe mkweli na muwazi, ukiona unasita ya kuwa matendo na mwenendo wako hauendani na maadili, tafadhali tambaa mbele, hunifai. Naomba uwe mtu mwenye nia njema, sio nia ya kuumiza wengine.

  Mwenzenu niko serious sitanii, ndo maana sijaandika kwenye jukwaa la Utani/Ucheshi, I AM MORE THAN SERIOUS

  KAMA UNASIFA HIZO, Tafadhali karibia chumbani, ni-PM huko then nitakupatia majibu ya next step na kujibu maswali for any issue of concern bandugu


  Kanuni inayotumika ni FIFS, kwa maana ya wakwanza watapatiwa kipaumbele. Usipoona ujumbe kwenye visitors message kwamba sasa maombi yamefungwa ujue bado application zinakaribishwa.

  Nyongeza: Uwe na uhakika na sifa hizi kabla hujachukua next step, maana ni sehemu muhimu ya mkataba wangu na huyo atakae-qualify, any debasement itaniumiza na itanipa shida nisiyotaka maishani. KARIBUNI

  HERI YA MWAKA MPYA KWENU NA MNIOMBEE MWENZENU NIUANZE VIZURI KWA KUMPATA PARTNER

  WHO KNOWS THAT I CAN GET MY LIFE TIME PARTNER HERE?
   
 2. FirstLady1

  FirstLady1 JF-Expert Member

  #2
  Dec 31, 2010
  Joined: Jul 29, 2009
  Messages: 16,575
  Likes Received: 541
  Trophy Points: 280
  Mwenzangu nakuuliza swali dogo na la nyongeza hivi hapo mtaani kwenu hujaona kabinti ka kukufaa ,kazini,kanisani, sokoni ,ukitoka out hugongani na vibinti vyenye maadili mema?
  condition zako nazo utadhani ajira inatafutwa
  all the best
   
 3. El Magnifico

  El Magnifico Member

  #3
  Dec 31, 2010
  Joined: Dec 26, 2010
  Messages: 14
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  FirstLady wapo huko kote, lakini ni nani ajuae mwenzake atatoka wapi? I feel here in JF. hapo vipi
   
 4. pauline

  pauline JF-Expert Member

  #4
  Dec 31, 2010
  Joined: Dec 26, 2010
  Messages: 651
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  nadhani unakosea saana kuweka vigezo viingi,hii inawapa watu impression uko choosy!...inaweza kuput off wadada..ungesema unatafuta mwenza....wangejitokeza wadada wengi halafu wewe mwenyewe ndio ungewachuja kutokana na vigezo ulivyojiwekea.
  mie sidhani kama watajitokeza wadada wengi kutokana na hili bandiko lako,nadhani umejilimit...anyway nisiseme saana nisije ambiwa sizitaki mbichi hizi...lols!:plane:
   
 5. NewDawnTz

  NewDawnTz JF-Expert Member

  #5
  Dec 31, 2010
  Joined: Nov 15, 2010
  Messages: 1,675
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Mkubwa haya masifa kweli utampata. Duuhh maana nahisi like you have taken to the extreme.

  Anyway, all the best and happy new year too.
   
 6. Preta

  Preta JF-Expert Member

  #6
  Dec 31, 2010
  Joined: Nov 28, 2009
  Messages: 24,111
  Likes Received: 3,031
  Trophy Points: 280
  mi namjua mmoja.....ana-fit sifa zote hizo ila ni diwani wa CCM....inakuwaje?
   
 7. Lizzy

  Lizzy JF-Expert Member

  #7
  Dec 31, 2010
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 22,224
  Likes Received: 244
  Trophy Points: 160
  Vigezo vyako vizuri....havijakaa kitamaa!!!Ndo kusema sura huangalii???Watu wasije wakaleta maombi alafu uwatolee nje !!
   
 8. RayB

  RayB JF-Expert Member

  #8
  Dec 31, 2010
  Joined: Nov 27, 2009
  Messages: 2,754
  Likes Received: 88
  Trophy Points: 145
  Duh kweli umeamua kuja kutafutia hapa JF mke? Kwanza hapa tuna ID anonymity ya high quality yaani huwezi jua hata jinsia ya mtu, usije ukavami kitu sicho. We endelea na juhudi zako katika real field sio humu kwa njia ya pen pals.

  Huo ushauri wangu
   
 9. El Magnifico

  El Magnifico Member

  #9
  Dec 31, 2010
  Joined: Dec 26, 2010
  Messages: 14
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Naogopa, mwenyekiti wao aliwaambia wasitupe unyumba wakati mimi nimechanjiwa damu ya Upinzani
   
 10. El Magnifico

  El Magnifico Member

  #10
  Dec 31, 2010
  Joined: Dec 26, 2010
  Messages: 14
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0

  Awali niliwahi kuangalia sura na ndizo zilizonilet down. Hapa sura kigezo cha mwisho
   
 11. El Magnifico

  El Magnifico Member

  #11
  Dec 31, 2010
  Joined: Dec 26, 2010
  Messages: 14
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0

  Ray B, nimeupokea ushauri wako vizuri, ila nimetahadharisha wazi ya kuwa sitanii, niko serious na mimi ni mwanaume halisi.

  Vilevile ndege wenye mabawa yafananayo huruka pamoja. So i trust in myself kwamba ni great thinker na ni vema nikapata great thinker mwenzangu
   
 12. Maty

  Maty JF-Expert Member

  #12
  Dec 31, 2010
  Joined: Aug 24, 2010
  Messages: 2,170
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 135
  Umri je mi nina sifa zote kasoro nina miaka 35
   
 13. k

  kisukari JF-Expert Member

  #13
  Dec 31, 2010
  Joined: Jul 16, 2010
  Messages: 3,753
  Likes Received: 1,038
  Trophy Points: 280
  mmmh,kweli upo serious,eeeh,yaani tume match haswa,especially no.3{niliumizwa mpaka leo naogopa kupenda}no.6,no.10 na no.1 naamini laaziz wako ni mie.lakini mbona vikwazo vingi?kama tupo darasani tunapewa home work?
   
 14. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #14
  Dec 31, 2010
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,392
  Likes Received: 81,396
  Trophy Points: 280
  El Magnifico, nimevipenda vigezo vyako vyote na ni rahisi kufikiwa na wengi. Nakutakia kila la heri katika kumpata mwenza wako kimaisha. Kitu kimoja tu, umeweka umri wako je hupendi kuweka umri wa huyo mwenza mtarajiwa uwe kuanzia wapi mpaka wapi?
   
 15. El Magnifico

  El Magnifico Member

  #15
  Jan 1, 2011
  Joined: Dec 26, 2010
  Messages: 14
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Age aint a thing but a number. By the way, akiwa 25 to 28 poa sana. Zaidi ya hapo kama vigezo vipo umri ndo vile tena, hapo ni swala la kufikiria tu na kukubaliana.
   
 16. W

  Wakuchakachua JF-Expert Member

  #16
  Jan 1, 2011
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 346
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Vigezo vyoooooooote ninavyo ila sasa sura yangu ni tatizo kwa watu wengi sijui we utaikubaliiiiii:teeth::teeth:
  maana kuwa smart kuna ushirikiano mkubwa unaotolewa na sura plus umboooooooo lolo
  all the best utapata mchizi
   
 17. katelero

  katelero JF-Expert Member

  #17
  Jan 1, 2011
  Joined: May 31, 2010
  Messages: 529
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Nina vigezo vyote hivyo, ila anza wewe kwanza kuniPM
   
 18. C

  Chief JF-Expert Member

  #18
  Jan 1, 2011
  Joined: Jun 5, 2006
  Messages: 1,488
  Likes Received: 194
  Trophy Points: 160
  Du!! Hii kali.
   
Loading...