Life Jackets zinatumika ipasavyo ndani ya Ndege, Meli au Boti?

Life Jackets zinatumika ipasavyo ndani ya Ndege, Meli au Boti?

lukelo sakafu

JF-Expert Member
Joined
Feb 19, 2015
Posts
2,938
Reaction score
517
Mliowahi kusafiri na Ndege, Meli, Boats mtakua mnauelewa mzuri kuhusu LIFE JACKETS AU JAKETI LA MAISHA ambalo humsaidia abiria katika kuokoa maisha yake wakati wa ajali.

Katika Meli na Boti abiria utakiwa kulivaa na kujitosa majini ambapo atakuwa akielea majini mpaka msaada ukifika ataokolewa na katika ndege abiria atalivaa na kujitupa nje ambapo atakua akielea angani taratibu mpaka akitua chini na kupata msaada.

Lakini nilichogundua ni kwamba hizi life jackets hatuzitumii inavyotakiwa na ndio maana hata ikitokea ajali ya meli, boti au ndege utasikia abira wote wamefariki wakati kulikua na life jackets za kutosha na wahudumu wake walitoa demonstration nzuri kwa abiria jinsi ya kujiokoa kwa kutumia haya majaketi.

Kuna mifano ya ajali kama ile ya ndege ya Germany Airways Airbus iliyoua abiria wote 150, kuna ajali ya meli Nungwi Zanzibar, ajali ya meli MV VICTORI MWANZA, ajali ya boti ya MV STUGART Zenji, hizi ajali zimeua wapendwa wetu, tatizo nini?

LIFE JACKETS zipo maelekezo yametolewa mazuri lakini abiria hawaponi.
 
Labda niulize kidogo.......Lufthansa ilianguka milimani........life jackets hapo zilikuwa zinaingiaje...........?......
 
Labda niulize kidogo.......Lufthansa ilianguka milimani........life jackets hapo zilikuwa zinaingiaje...........?......

Ha ha ha Zinasaidia kuelea angani mkuu,life jackets husaidia abiria kwenye maji tu,kwenye ndege Kama rubani ameona ndege Ina tatizo hawezi kuendelea na safari,ni bora kutua kwenye maji kwani kutakuwa na uwezekano mkubwa wa abiria kuokolewa na hapo ndipo life jackets inapoingia..
 
Labda tuchukulie mfano........kutoka Dar kwenda Mbeya........au Dar-Kia.........life jacket hapo linanisaidiaje.........?......unless otherwise litageuga parachute................
 
mliowahi kusafiri na ndege,meli,boats mtakua mnauelewa mzuri kuhusu LIFE JACKETS AU JAKETI LA MAISHA.ambalo umsaidia abiria katika kuokoa maisha yake wakati wa ajari. katika meli na boti abiria utakiwa kulivaa na kujitosa majini ambapo atakuwa akielea majini mpaka msaada ukifika ataokolewa na katika ndege abiria atalivaa na kujitupo nje ambapo atakua akielea angani taratibu mpaka akitua chini na kupata msaada. lakini nilichogundua ni kwamba hizi life jackets atuzitumii inavyotakiwa na ndio maana ata ikitokea ajari ya meli,boti au ndege utasikia abira wote wamefariki wakati kulikua na life jackets za kutosha na wahudumu wake walitoa demonstration nzuri kwa abiria jinsi ya kujiokoa kwa kutumia haya majaketi. kuna mifano ya ajari kama ile ya ndege ya germany airways airbus iliyoua abiria wote 150, kuna ajari ya meli nungwi zanzibar, ajari ya meli MV VICTORI MWANZA, ajali ya boti ya MV STUGART zenji, hizi ajari zimeua wapendwa wetu, tatizo nini LIFE JACKETS zipo maelekezo yametolewa mazuri lakini abiri hawaponi.

mtoa mada jarib kujiongez mwenyew. Ndege inapotaka kuruka inakimbia speed 600 then unafikir ikishapata level speed yake inakuwaje? kuna ndege zinakimbia hadi km 1000 kwa saa .Ebu nambie ndugu ikipata itiraf utavaa life jacket saa ngapi ? watu wanajarib sana kujiokoa lakin inashindikana kutokana na speed yake bro. kwenye mel huko sawa ila ujue life jacket haiwez kukusaidia kama wew hujisaidii hata kidogo.
 
lukelo sakafu ni kweli kwenye ndege kuna life jacket na huwa zipo chini ya kila kiti cha abiria wa daraja zote na pia kuna life raft kwa ufafanuzi kama mtumbwi wa mpira. kabla ndege haijapaa juu wahudumu wa kwenye ndege hutoa maelekezo ya kuvitumia vifaa hivyo iwapo itatokea hitilafu kwenye ndege na kutua kwenye maji kwa dharura na siyo kama life jacket hizo zina uwezo wa kumfanya mtu aele hewani
 
Unafuatilia hizi ajali? Au unaunga matukio usiuoyaelewa?

mliowahi kusafiri na ndege,meli,boats mtakua mnauelewa mzuri kuhusu LIFE JACKETS AU JAKETI LA MAISHA.ambalo umsaidia abiria katika kuokoa maisha yake wakati wa ajari. katika meli na boti abiria utakiwa kulivaa na kujitosa majini ambapo atakuwa akielea majini mpaka msaada ukifika ataokolewa na katika ndege abiria atalivaa na kujitupo nje ambapo atakua akielea angani taratibu mpaka akitua chini na kupata msaada. lakini nilichogundua ni kwamba hizi life jackets atuzitumii inavyotakiwa na ndio maana ata ikitokea ajari ya meli,boti au ndege utasikia abira wote wamefariki wakati kulikua na life jackets za kutosha na wahudumu wake walitoa demonstration nzuri kwa abiria jinsi ya kujiokoa kwa kutumia haya majaketi. kuna mifano ya ajari kama ile ya ndege ya germany airways airbus iliyoua abiria wote 150, kuna ajari ya meli nungwi zanzibar, ajari ya meli MV VICTORI MWANZA, ajali ya boti ya MV STUGART zenji, hizi ajari zimeua wapendwa wetu, tatizo nini LIFE JACKETS zipo maelekezo yametolewa mazuri lakini abiri hawaponi.
 
Life jacket za kwenye ndege hazikuwezeshi kuelea hewani, zinakusaidia kuelea kwenye maji.
 
lukelo sakafu ni kweli kwenye ndege kuna life jacket na huwa zipo chini ya kila kiti cha abiria wa daraja zote na pia kuna life raft kwa ufafanuzi kama mtumbwi wa mpira. kabla ndege haijapaa juu wahudumu wa kwenye ndege hutoa maelekezo ya kuvitumia vifaa hivyo iwapo itatokea hitilafu kwenye ndege na kutua kwenye maji kwa dharura na siyo kama life jacket hizo zina uwezo wa kumfanya mtu aele hewani

Kwa mara zote nilizopanda ndege life jacket zote zilizokuwa zikionyeshwa kwa abiria niliziona kama hazina uwezo wa kumuwezesha mtu kuelea angani bali kwenye maji. Labda wenye uelewa zaidi naomba mtujulishe tafadhali
 
Naomba usome vizuri bandiko langu wapi,nimeandika life Jacket inauwezo wa kuelea angani?!!
 
Kwanini wasitengeze L.J zinazoelea angani?
 
mkuu nafuatilia ajali zote za ndege life jacket inakusaidia kuelea angani than ukitua chini unapata msaada

Wewe unafuatilia, mimi nimesafiri na ndege nne tofauti za kq yaani kenya airways kwa hiyo nina uhakika na ninachosema . Ukiwa ndani ya ndege kabla ya kuruka mnapewa maelekezo yote ya safari ikiwa ni pamoja na usalama, mtapita wapi na umbali gani juu. pia mtatumia muda gani safarini. Life jacket zilizopo zitasaidia ikiwa ndege utaangukia au kushuka kwenye maji, pia unaambiwa usijaze upepo life jacket ukiwa ndani ya ndege.
 
.. lukelo sakafu kinachokufanya uelee an gani ni parashut, na kinachomkuta ya uelee majini ni life jacket au boya.
Kama unataka kufanya research khsu life jacket upande wa majini panga safari uende mafia boti zao ndiyo utajua kama life jacket zinatumika au laa
 
Last edited by a moderator:
Mliowahi kusafiri na ndege, meli, boats mtakua mnauelewa mzuri kuhusu LIFE JACKETS AU JAKETI LA MAISHA. Ambalo humsaidia abiria katika kuokoa maisha yake wakati wa ajali.

Katika meli na boti abiria utakiwa kulivaa na kujitosa majini ambapo atakuwa akielea majini mpaka msaada ukifika ataokolewa na katika ndege abiria atalivaa na kujitupa nje ambapo atakua akielea angani taratibu mpaka akitua chini na kupata msaada.

Lakini nilichogundua ni kwamba hizi life jackets atuzitumii inavyotakiwa na ndio maana hata ikitokea ajali ya meli, boti au ndege utasikia abira wote wamefariki wakati kulikua na life jackets za kutosha na wahudumu wake walitoa demonstration nzuri kwa abiria jinsi ya kujiokoa kwa kutumia haya majaketi.

Kuna mifano ya ajali kama ile ya ndege ya Germany airways airbus iliyoua abiria wote 150, kuna ajali ya meli Nungwi Zanzibar, ajali ya meli MV VICTORI MWANZA, ajali ya boti ya MV STUGART Zenji, hizi ajali zimeua wapendwa wetu, tatizo nini LIFE JACKETS zipo maelekezo yametolewa mazuri lakini abiri hawaponi.

Hiyo niliyokuwekea nyekundu, si kweli.

Life jacket au life vests za kwenye ndege za abiria (commercial aviation) nazo hutumika baharini kukusaidia kuelea. Na si za mwavuli kama utakavyo kutuaminisha. Jionee, uzijuwe:

Naomba muwe mnafanya ka research japo kiduchu kabla ya kuja na mada zenye mambo msiyoyaelewa.

Miamvuli (parachutes) nijuavyo hutumika katika baadhi ya ndege za kijeshi (military) nazo huwa na viti maalum (ejector seat) vya rubani na msaidizi wake vinavyorushwa nje wakibonyeza kifungo fulani (eject button) pindi wakitunguliwa au kukiwa na dharura, na hivyo viti hutoka kwa kasi (huwa na rocket motor) vikielekea juu zaidi na halafu hufungua mwamvuli. Vimetengenezwa kitaaalaam sana, kwani hata ndege ikiwa chini chini basi kiti kitakupaisha kwanza juu ili kipate urefu wa kuweza kufunguwa mwamvuli ipasavyo na kushusha salama.

mkuu nafuatilia ajali zote za ndege life jacket inakusaidia kuelea angani than ukitua chini unapata msaada

Lukelo Sakafu nadhani itakubidi kama upo Dar-es-salaam au kilimanjaro nakushauri uende ukatembele kwenye karakana za ufundi wa ndege kwenye viwanja vya ndege vya hiyo Mji utapata elimu tosha kuhusu hizo life jacket iwapo hujaridhika na majibu ya humu kwenye jamvi.

Nasisitiza kuwa life jacket haimwezeshi binadamu kuelea angani
 
Back
Top Bottom