Dunia ina watu wa ajabu wasiotaka kuukubali uhalisia. Kuna watu hata wakati Saddam alipoangushwa hawakuamini, walikuwa wanasubiri aibuke atoe pigo la mwisho kwa majeshi ya uvamizi, Osama alipouawa hawakuamini wanasubiri aibuke atoe vitisho vyake kama kawaida! Gadhafi kakurupushwa hawakubali wana matumaini kuwa anaweza kurudi kwa namna fulani! Leo hii Maembe anaweza kuona ni wapi sheria zisizoidhuru Tz zimevunjwa lkn serikali hii na wizara anayoiongoza hawawezi kutwambia sheria zilizovunjwa na hatua stahiki zilizochukuliwa kurudisha wanyama wetu wanaotoroshewa uarabuni kila leo. Kama kweli wanamkubali Gadhafi kiasi hicho, yale ambayo tunaambiwa ameyafanya kulinda maliasili za Libya kwa nini hawajayafanya nchini mwetu kulinda maliasili zetu? Wanamkubali kwa lipi? kupewa zawadi binafsi ambazo zimeibwa kutoka Libya??? Kupandishwa kwa bendera tofauti kungeipa Tanzania hasara gani? Kurudishwa kwa bendera ya gadhafi kunatupa faida gani kama taifa? Waendelee kumsubiri gadhafi (ambaye ni mfalme wao) atawakumbuka akirudi madarakani!!!