- Source #1
- View Source #1
Wakuu hii taarifa ni ya kweli imetolewa na LHRC?
- Tunachokijua
- Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC) ni shirika la utetezi wa haki za binadamu nchini Tanzania. LHRC ilianzishwa mwaka 1995 kama shirika lisilo la kiserikali, la hiari, lisiloegemea upande wowote na lisilo la faida, likiwa na madhumuni ya kufanya kazi ya kuwawezesha na kuhamasisha uelewa wa kijamii, wananchi wa Tanzania kuhusu haki za kisheria na za binadamu.
Madai
Julai 9, 2025 katika mitandao ya kijamii kumeibuka barua yenye utambulisho wa kituo cha sheria na haki za binadamu (LHRC) ikiwa na kichwa kinachosomeka “LHRC KINALAANI NA KUKEMEA KAULI ZA BI. MARIA SARUNGI ZINAZOHATARISHA AMANI KUPITIA MITANDAO YA KIJAMII”.
Barua hiyo imeambatanishwa kwenye grafiki yenye utambulisho wa Mwanahalisi Digital ikiwa na ujumbe (caption) unaosomeka “KITUO CHA SHERIA (LHRC) CHATAKA MARIA SARUNGI AACHE KUCHOCHOE FUJO MTANDAONI”
Uhalisia wa taarifa hiyo
Ufuatiliaji wa kina uliofanywa na JamiiCheck umebaini kuwa taarifa hiyo Si ya kweli.
Kituo cha sheria na haki za binadamu (LHRC) hawajotoa barua yoyote kwa siku ya Julai 9, 2025 kupitia katika kurasa zao rasmi za mitandao ya kijamii kuhusiana na jambo lolote lile ikiwemo la kumuonya Maria..
Aidha grafiki ya Mwanahalisi Digital iliyotumika kusambaza upotoshaji huo ni ya kughushi kwnai haijachapishwa katika kurasa zao rasmi. Grafiki hiyo pia imetumia aina tofauti ya mwandiko ukilinganisha na ule unaotumiwa na chanzo hicho kwenye grafiki zao.