Kupitia ukurasa wa mtandao wa instagrama Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC) imetoa taarifa ya kuhusu wafanyakazi wake kuvamiwa jana Novemba 12, 2025 wakati wakiendelea na majukumu yao katika Hoteli ya Whitesands Jijini Dar es Salaam ambapo walinyanganywa vitendea kazi na leo Novemba 13, 2025 wameitwa kuhojiwa kuhusu vifaa hivyo
"Wafanyakazi wa wa Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC) walivamiwa usiku wa jana wakiwa wanaendelea na na majukumu yao katika Hoteli ya Whitesands Jijini Dar es salaam. Hoteli yote ilizingirwa, na timu yetu ndiyo ilikuwa inalengwa moja kwa moja. Simu na kompyuta mpakato zao zilichukuliwa. Na asubuhi ya leo wameitwa kuhojiwa kuhusu vifaa hivyo. LHRC tumesikitishwa sana kwa tukio hilo"- Taarifa ya LHRC