Wana Jf, Heshima kwenu nyote.
Mimi ni muajiriwa kwenye kampuni ya private. Ninajituma sana kwenye kazi, na huwa niko proactive kwenye kupanga mambo yangu ya kikazi. Huwa sipendi mambo yatokee kwa surprise afu nianze ku react kutafuta soln.
Bidii imenifanya niweze kupitia levels mbali mbali za kikazi kwenye management ya kampuni.
Tatizo linakuja pale ambapo huwa ninaanza kutafakari hatima ya maisha yangu. Huwa sikubaliani na wazo la kufanya kazi mpaka nistaafu. Huwa najiuliza, hivi nikiamua kufanya shughuli yangu mwenyewe ( hasa biashara) sitatoka kimaisha kutokana na bidii yangu? Nilishawahi fanya biashara fulani ambayo ilikuwa inalipa sana, tatizo lilikuja kwenye supervision .....most of the time nakuwa kazini. Na kama mnavojua watu sio waaminifu, basi ile biashara ilikuja ikafa.
Naombeni yeyote mwenye experience ya kuajiriwa kisha kuamua kuacha kwa hiari na kwenda kujiajirii atusaidie kutuelezea ilikuwaje akafikia uamuzi huo?
Mambo mengine kama vile "Kujipanga kwanza kabla ya kuacha kazi ..yapo kwenye mchakato tayari".
shukrani
sasa wewe umeambiwa utoe ushauri au experience yako badala yake unatuambia una bata lako pekea ako??Du unanikumbusha nilipotoa 24hrs notes Vodacom ilikuwa 2009.thanks Jesus now Im on my own Bata daily and got nothing to loose
sasawakani ili nini? acha ukishasoma hii comment hapa.Uwiiiiiiiiiiiiiiiiii
Hi thread inaniumiza sana. Nina a profession ambayo nikiamua kuwa self employed ninaweza kutengeneza kwa kiwango cha chini laki 1 kwa siku. Nimeajiriwa mshahara wangu hauzidi shilingi laki 6. Kweli kuajiriwa ni utumwa. Nimejiwekea malengo niache kazi mwaka ujao!!!!!!!:A S crown-2:
kinachozungumzwa tunapozungumzia kuhusu kuacha kazi sio tu swala la fedha. kuna mambo meni.mimi nina wazo tofauti kidogo,kila mtu akiamua kuacha kazi na kujiajiri na sote tukawa our own bosses,nani atafanya kazi kwa niaba yetu sasa,hili ni wazo kwa wale ambao wanasita kuacha kazi wanaweza kusanya assets ambazo zitawasaidia baadae,maana si kila mtu anaweza fanya biashara,mfano kama unafanya kazi na unalipwa vizuri na wenzako unaofanya kazi wanatumia pesa ktk kununua vitu kama magari ya kifahari na starehe wewe unaweza kuinvest ktk vitu kama nyumba ukazipangisha,endelea kukusanya assets na hata kama unafanya kazi bado utakua in control of your financial futurepasipo kuacha kazi.
kosa nililolifanya mimi ilikuwa ni kuwashirikisha wanafamilia na marafiki ambao wote ni waajiriwa na hakuna aliye na hata kabiashara ka duka. Mkuu tangulia tupo njia moja.
nilima mpunga kijijini baada ya kukoboa nilipata gunia zaidi ya 50 za mchele niliingiza around ---- 12.2m
niliilima mahindi na kuyasaga nilipata gunia kama 130 za sembe 900 per kg nilipata zaidi ya --------10m
ufugaji wa ng'ombe wa maziwa, nauza lita 1000-1200/= na kila siku napata lita si chini ya 75 ---- naingiza 2.5m kila mwezi--- kwa mwaka ng'ombe wananipa ---27m
ufugaji wa nguruwe kwasasa ninao kama 80 na 8 wana mimba----- kila mwaka natarajia kuuza 150--- roughly let say nitapata around 40m
nalima maharagwe, njugu, matikiti kiasi, maembe nk nayo yanaingiza fedha nzuri sana japo sijui mahesabu yake halisi
Majumuisho
total = 10m+10m+27m+40m= 87mil
ukitoa operating costs profit will be around let say 45m kwa makisio ya chini kabisa na hapa ni baada ya kuibiwa sana mazao ya kilimo na mifugo na hii nguvukazi yangu ambayo haina uaminifu hata kidogo yaani kila nikibadili vijana wa kazi wanakuwa na uadilifu kwa miezi 3 ya mwanzo baada ya hapo matatizo ni yaleyale wizi kwa kwenda mbelee.. watu wameoa, wamejenga kwa jasho langu.
Mkuu hebu angalia hapa maziwa nispokuwepo yanapatikana lita 50-70 nikiwepo mwenyewe na kusimamia ukamuaji zinapatikana lita 90 mpaka 100. Mchele nikiacha gunia 10 nikienda mjini na kurudi kijijini nakuta zimebaki gunia 7 nikiuliza sipati majibu.. inaniuma sana sana.. nataka kwenda kusimamia kazi zangu mwenyewe[/QUOTE]
mkuu hapo pa bluu umenitonesha kidonda,yaani watu si waaminifu mkuu mim wafanyakazi waliniibia sana mwishowe nikaamua kuajiri ndugu zangu toka kijijini,walipozoea tu mazingira walinitenda sana roho inauma sana lkn sina jinsi.Heri wewe umeamua kwenda kusimamia mwenyewe,mim natamani nikasimamie mwenyewe sbb simuamin tena mtu lakini kwa sasa haiwezekani.
mkuu hapo pa bluu umenitonesha kidonda,yaani watu si waaminifu mkuu mim wafanyakazi waliniibia sana mwishowe nikaamua kuajiri ndugu zangu toka kijijini,walipozoea tu mazingira walinitenda sana roho inauma sana lkn sina jinsi.Heri wewe umeamua kwenda kusimamia mwenyewe,mim natamani nikasimamie mwenyewe sbb simuamin tena mtu lakini kwa sasa haiwezekani.
Mie niliacha kuajiliwa baada ya kusoma kitabu Chenye title "RICH DAD AND POOR DAD" by KI.... Sikumbuki Sawa Sawa mtunzi, kwa wale waliokisoma watanikumbusha, maana nilimpa za wadi rafiki yangu hicho kitabu. Tafadhali naomba usome hicho kitabu, kitakubadilisha sana. Nakumbuka moja ya sentesi zilizonikaa ni kuwa,kuajiliwa ni utumwa na unashindwa kufikiri. Anaendelea kusema, mwajiliwa baada ya kulipa kodi ya nyumba,Maji,umeme na Ada ya shule anajiona ame win. Sasa kinachobaki hakiwezi kumsitiri baada ya kustaafu na wengine hufa kwa ugonjaw wamoyo au bp baada ya hela atakazozipata baada ya kustaafu
Ndo Obama kasema CHANGE. Mabadiliko yoyote lazima yanakuja na mshituko na lazima tukubaliane nayo.
Moja ya usemi wa Warusi" asiyefanya risk asinywe shampeini" yaani shampeini hunywewa baada ya mafanikio. Sasa utafanikiwaje Kama hutafanya risk au mabadiliko.?
Kaka chukua maamuzi sasa hivi, hujachelewa
Mjinga wewe upo kwenye quadrant ipi?