Kujichubua hakutoisha hata ukamilifu wa dahari. Inferiority complex imetuingia watu weusi hadi rohoni na inazidi kuongezeka kadri muda unavyokwenda.
Siku hizi kuzaa na mzungu ndio dili ili mtoto atoke .5 ndio tunaona mtoto mzuri, in other words, watoto weusi wabaya ila wazungu na .5 ndio wazuri.
Tulishakataa tamaduni zetu na kuiga za mtu mweupe, tumekataa na tunazidi kukataa majina yetu na kukimbilia ya weupe kwa speed, sahizi unakutana na mtu majina yake matatu ni Happy Charles John au abdallah Salim Mohamed tena siku hizi kuna hadi watoto wa waswahili wanaitwa Sean na Beyonce Ni hatari. Nywele zetu tunaona hazina dili tunataka za kama wazungu. Dada zetu na shape za kibantu wanaona hawana soko nao wanataka shape zakizungu ili kwenda na trend iliyopo
Kifupi inferiority complex imetuingia kiasi Cha kuto-reverse tena hivyo kuchibua kutazidi badala ya kupungua ili tuende sawa na wakati