Fukuto dhidi ya Gaddaffi linasababishwa na utawala wake Wa kiimla na jinsi ambavyo yeye na familia yake wameshikilia mhimili wa uchumi wa nchi. Mipango ya badaye ya Ghaddaffi ilikuwa ni kumrithisha mwanaye Islam uongozi wa nchi mara yeye atakapofikia stage ya incompetence. Gaddaffi anawapa wananchi wake elimu bure, matibabu bure pamoja na kuwajengea wazee makazi maalum lakini hiyo fedha haitoki mfukoni mwake bali ni raslimali ambayo mwenyezi Mungu amewapatia Walibya wote waifaidi. Kuwa mwananchi ambaye unalelewa kama kuku kisasa (broiler) kwa kupewa vyakula na malazi wakati Huna uhuru kujieleza, huna nafasi ya kuchagua kiongozi umtakaye, huna uhuru wa kuonyesha uwezo wako wa uongozi inakuwa ni kiini macho.
Yeye Gaddaffi alimpindua mfalme Idris mwaka 1967 na ametawala kwa takriban miaka 42 si awaachie na wengine watawale?