Jamani tujaribu kutaja hata weakness za uwongo basi. au tujivike weakness za wengine. najua hapa itakuwa rahisi. Tutaje weakness za wafanyazi wenzeti, wapangaji wenzetu, viongozi wetu. Tukipata mlolongo wa weakness tunaweza kujitazama katika zilizotajwa zipi zinatuhusu. But hii thread inaweza kukupa picha kwa nini soory ni gumu miongoni mwetu hasa kwa wanasiasa. Kwa nini wengi wetu hatukubali kujikosoa na mbaya zaidi hatupendi kukosolewa. sisi wana jf tukiwa wanasiasa wa au viongozi wa jamii kesho ni yale yale. Je unaweza kuwa mme/mke bora nyumbani, mkazi mzuri mtaani, mfanyakazi bora zaidi ofisini, meneja mzuri zaidi , kiongozi mwenye maadili kwenye ngazi mbali mbali bila kutambua mapungufu na matatizo yako? To be better and even more better we need to identify our weakness and work on them.