Leticia Nyerere, John Shibuda (CHADEMA) wajisajili katika Bunge Maalum la Katiba

Wlnaoburuzwa wapo sasa hivi kwenye bunge la katiba ambao siku zote huwa wanaitwa kwenye party caucus kuambiwa cha kufanya bila majadiliano.

Wanaoburuzwa wapo nje ya bunge la katiba ambao wengi wao hawajui kwa nini mbowe lipumba na mbatia wamewalazimisha kususia shughuli za bunge.
 
Mod wana hasira sana, ndio maana kuna mod mmoja kaiponda ukawa kavuliwa umod loh!

MOD tafadhari hii topic iwekeni jukwaa a siasa
 
Mbunge wa viti maalum chadema na mujumbe wa bunge maalum la katiba ( mjumbe wa ukawa) amerudi bungeni kuendelea na vikao vya bunge maalum tupate katiba mpya. Hongera sana leticia. Taifa kwanza, vyama baadae

source: itv habari saa mbili kamili usiku

[h=2]Kakobe: JK Kavuruga Mchakato wa Katiba, amtaka aombe radhi[/h]
Kakobe amlaumu Kikwete

Askofu wa Kanisa la Full Gospel Bible Fellowship (FGBF), Zachary Kakobe, amemshambulia Rais Kikwete kwamba ndiye aliyevuruga mchakato wa kupatikana kwa katiba mpya.

Kakobe amewataka wajumbe wa UKAWA kutorejea katika Bunge Maalum la Katiba ambalo alidai limejazwa unafiki na endapo wakiamua kurejea watakuwa wamerogwa.
Alitoa kauli hiyo jana jijini Dar es Salaam katika maadhimisho ya miaka 25 ya kanisa hilo lililoanzishwa mwaka 1989.
Alisema Rais Kikwete, alipolizindua Bunge Maalum la Katiba, alitumia fursa hiyo kutoa hoja za kuvuruga rasimu ya wananchi ambayo iliwasilishwa na Jaji Joseph Warioba.

Askofu Kakobe alisema hoja za Rais Kikwete za kujikanganya alizozitoa siku hiyo, yalikuwa ni majibu ya maombi ya Jumuiya ya Wakristo wa Kipentekoste (PCT) ya kuvuruga mchakato wa katiba baada ya kutoa upendeleo kwa kuwateua baadhi ya wajumbe wakiwamo viongozi wa dini, kupata uwakilishi kwa baadhi ya Wakristo bila kutenda haki kwa wananchi wote.

Alisema katika mambo yanayofanywa makusudi na wanadamu, Mungu amewapa akili ya kuyavuruga, hivyo ndiyo maana wakiwa katika viwanja vya Sabasaba waliamua kufanya maombi na nguvu ya Mungu inatumika sasa kuonyesha kuwa mchakato huu ulianzishwa pasipo haki.

“Namtaka Rais Kikwete akiri hadharani kuwa amekosea na awaombe Watanzania radhi kwa makosa aliyoyafanya hata kusababisha wanasiasa upande wa upinzani kuunda UKAWA ili haki ya wananchi ipatikane, hivyo atumie busara kufanya hivyo kwa kuwa ndiye baba wa taifa hili.

“Kuna kauli za viongozi wa CCM kuwa wanataka kutawala milele… sasa mimi nasema sawa tu wafanye hivyo, lakini kwa kwenda na haki na siyo kwa kulazimisha kama ilivyo sasa katika suala la katiba… hivyo ni katiba ya wananchi wote wa Tanzania ambao wamo vyama vya siasa na wasiokuwemo,” alisema.

Askofu Kabobe alisema katika kujikweza kuwa hajahusika kuvuruga, Rais Kikwete, amewatumia vibaya viongozi wa dini aliodai wanaegemea upande wa CCM kuwataka waombee mchakato wa katiba na kuwataka UKAWA warudi bungeni, huku akijua watumishi hao wanapaswa kufanya kazi isiyo na upendeleo.

“Daima nitasimama katika kweli nayo itaniweka huru, hapa nasema wazi kwamba Rais Kikwete ameamua kuwatumia vibaya viongozi wa dini… nao wakaona bora watumike ili kupata mkate na chai Ikulu ambayo majani yake ni ya hapahapa nchini, tena Mufindi, siyo dhahabu, wanachoendelea kukifanya kwa wanachi ni unafiki wala siyo maombi.

“Nilidhani Rais Kikwete atawaambia viongozi hao wamwombee yeye aliyevuruga mchakato huu na siyo kuuombea mchakato wa katiba na amani… mimi najua nchi yetu ina amani na amani itavurugwa na hao wanaong’ang’ania hoja zao, kwani katika hili gumzo la katiba linaloendelea mtu mjinga tu ndiye atakayewalaumu UKAWA.

“Nawaomba viongozi wa dini wasijikombe kombe Ikulu maana wao wanamwakilisha Mungu… siogopi kusema kwa sasa hakuna ninachokosa hapa duniani wala sitaki kupendwa na rais, nitafanya yampendezayo Mungu,” alisema.
Huku akirudia rudia neno lake kwamba “sema ukweli ili uwe huru”, Askofu Kakobe alisema anawaunga mkono UKAWA kwa hatua yao waliyofikia hadi sasa hadi hapo Rais Kikwete atakapoomba radhi na kukubali wakajadili rasimu ya wananchi, kama watarudi bila makubaliano hayo, basi watakuwa wamerogwa.

“Nawaunga mkono UKAWA asilimia 100 kwa 100 na ninawaongeza 50 kwa hatua yao… sasa warudi kwa kauli ya rais kukiri mbele ya wananchi kuwa amekosea, anajirekebisha ili wajadili rasimu ya katiba, wasipofanya hivyo basi watakuwa wamerogwa… hakuna maridhiano hapo maana nimefuatilia na kubaini mazungumzo yanayoendelea yamejawa unafiki.
“Kuwaunga mkono UKAWA kwangu si kwamba nashabikia chama kimojawapo kinachounda umoja huo hapana… nazungumza kama baba wa kiroho mwenye kuwachunga watoto wengi wenye vyama vyote vya siasa ambavyo vipo nchini, ambao wanajua kwamba ninasimamia ukweli tupu,” alisema.
 
Mbunge wa Viti maalum kupitia CHADEMA Mh.Leticia Nyerere kwa mujibu wa ITV habari usiku huu ameonyeshwa na amesaini kitabu cha Mahudhurio ndani ya Bunge maalum La Katiba ikiwa ni kinyume na Msimamo wa CHADEMA kwa wajumbe wake kutohudhuria vikao hvyo.

Ni dhahiri sasa Leticia ameonyesha sura yake halisi kutokana na matendo yake ndani ya Chama kwa kutoheshimu maamuzi ya Vikao halali vya chama.

Ni wakati sasa wa Chama kumchukulia hatua kali za kinidhamu ikiwemo kuvuliwa uanachama.


Mkuu huyo si ni dada yako huyo??

Teh teh teh

Msambila kweli umevurugwa.
 
Mapandikizi yanajipambanua. Uzuri ni kuwa wananchi wanawafahamu. Na uzuri wabunge wa Cuf toka znz ndo tu wanaoweza kuzuia maamuzi juu ya vifungu vya katiba.
 
Chanzo.tarifa ya habari ya ITV leo

*************************************************

toa utabiri kesho

1.leticia
2.zzitto kabwe
3.chiku abwao
4.shibuda
5.akidiiiiiii imetoshaaaaaaaaaaa???????? ssssssm hoyeeeeee????? divide and rule + njaaa kali
 
Katika hali ya kushangaza! Mbunge Wa viti maalumu Leticia Nyerere amejiandikisha kwenye orodha ya wajumbe Wa bunge la katiba.hii inaonesha yupo tofauti na msimamo Wa chama chake (chadema) na ukawa!
 
Yan leticia unajua fika kuwa wewe sio mchaga af then unachezea shilingi chooni??

Teh teh teh.

Utafukuziliwa mbali.

Oooh.
 
Back
Top Bottom