Leseni za Teknolojia: Nokia wawafungulia mashtaka Apple

Leseni za Teknolojia: Nokia wawafungulia mashtaka Apple

RASHEEDMTOI

Member
Joined
Apr 13, 2015
Posts
85
Reaction score
68
Kampuni ya Nokia kutoka nchini Finland imesema kuwa inaishtaki kampuni ya Apple kwa kukiuka haki 32 za kiteknolojia.
Kesi hiyo ya Nokia imewasilishwa katika mahakama tatu nchini Ujerumani na Texas.
Madai hayo yanashirikisha matangazo, matumizi ya Interface, programu ,antena, chipu na alama za siri za video.
Siku ya Jumanne ,Apple ilianzisha mashtaka dhidi ya kampuni ya utafiti ya Acacia Research pamoja na kampuni ya umiliki wa mali ya Conversant Intellectual Property managament ikidai kuwa ilishirikiana na Nokia kuilaghai fedha Apple.
Nokia ilisema: tangu kuweka makubaliano kuhusiana na leseni zinazosimamia teknolojia hizo kutoka kwa Nokia 2011, Apple imekataa maombi yaliofanywa na Nokia kuzipatia leseni baadhi ya tekenolojia zilizovumbuliwa ambazo hutumika na bidhaa nyingi za Apple.
Kati ya mwaka 2009 na 2011,kampuni hizo mbili zilikabiliana mahakamani kuhusu uvumbuzi huo wa kiteknolijia uliotumika katika simu zao.
Wakati huo Nokia ilikuwa inaongoza kama kampuni inayootengeza simu duniani lakini ikawa inakandamizwa na kuimarika kwa iPhone ya Apple

Source bbc
 
Mkuu kwani wao apple hawana uwezo wa kuvumbua teknolojia yao au programs zao pekee?
wanaweza ila kila kampuni na utamaduni wake, Apple budget zao za kufanyia utafiti ni ndogo sana hivyo usitegemee wavumbue mambo mengi, wao wanataka wapate tu faida kubwa kwa kutumia teknolojia za watu
 
sasa hawa jamaa nao wanashikilia toknolojia tu na hawazitumii kutuletea simu kali

yes wanayo haki ya kudai haki kama makubaliano yao yalivyo kuwa ila kukumbatia teknolojia tuu acha waibiwe tu
 
sasa hawa jamaa nao wanashikilia toknolojia tu na hawazitumii kutuletea simu kali

yes wanayo haki ya kudai haki kama makubaliano yao yalivyo kuwa ila kukumbatia teknolojia tuu acha waibiwe tu

Nokia ametumia zaidi ya dola bilioni 100 kufanya research za simu (zaidi ya trilioni 200 za kitanzania)

na technology ni zao wamezigundua wao kwanini wawape wengine bure?

Na Nokia hajaanza kumshitaki Apple, bali ni Apple ndio ameanza kumshitaki Nokia hapo Nokia amejibu tu mapigo
 
Back
Top Bottom