Leseni ya biashara ya duka lako la nguo

Leseni ya biashara ya duka lako la nguo

youngkato

JF-Expert Member
Joined
Sep 3, 2014
Posts
3,638
Reaction score
3,641
1*gPrYsius63hdJmplTV7qRw.png

Kama una duka la nguo, leseni ni kitu muhimu sana kwenye biashara yako. Inakutambulisha kama boss halali wa biashara, inakuondoa stress ya kufungiwa ghafla, na inakufungulia fursa za mikopo na fursa zingine kubwa. Ukiwa nayo, unakua na uhuru wa kufanya biashara bila woga.

Faida unazopata ukiwa na leseni​

Leseni inakupa heshima mbele ya wateja na hata benki. Ukiwa nayo unaweza kufungua akaunti ya biashara, kupata mkopo kirahisi, na kuepuka zile safari za kuficha bidhaa kila ukisikia maneno ya “ukaguzi unakuja.” Pia, serikali inakutambua kama mchangiaji wa uchumi na hiyo inamaanisha biashara yako iko safe.

Masharti unayotakiwa kufuata​

Baada ya kupata leseni, kuna masharti ya msingi. Kila mauzo yako toa risiti, hakikisha nguo zako zina ubora unaokubalika, na usiuze bidhaa feki au zisizoidhinishwa. Masharti haya hayakusumbui yanakusaidia wateja waamini biashara yako na mamlaka ikutambue kama mtu wa maana.

Makundi ya leseni yako ipi?​

Leseni zipo aina mbili Kundi A na Kundi B. Kwa duka la nguo, mara nyingi utakuwa Kundi B, ambalo linashughulikiwa na halmashauri ya mtaa wako kupitia Afisa Biashara. Hapa mchakato ni rahisi na gharama ni nafuu kuliko Kundi A ambalo ni kwa makampuni makubwa kama benki au kampuni za simu.

Nyaraka unazohitaji​

Usijaribu kuanza process bila nyaraka hizi: cheti cha TIN kutoka TRA, cheti cha usajili wa kampuni kama biashara yako ni kampuni, mkataba wa pango kama duka si lako, na Tax Clearance kutoka TRA. Kama biashara yako inahusiana na bidhaa zenye viwango maalum (kama nguo za watoto), hakikisha una vyeti vya ubora kutoka mamlaka husika.

Jinsi ya kulipia ada ya leseni​

Siku hizi hutopelekewa mtu hela mkononi. Malipo yanapitia mfumo wa Local Government Revenue Collection System. Unapewa control number. Ada hutegemea aina ya biashara yako na eneo ulipo. Kwa mfano, duka la nguo dogo linaweza kulipa kama elfu 80 kwa mwaka.

Muda wa leseni na kuifanyia upya​

Leseni yako inakaa mwaka mmoja. Baada ya hapo unayo siku 21 tu kufanyia upya bila faini. Ukichelewa, unaanza kutozwa adhabu ya 25% na itaongezeka kila mwezi. Ni bora ujipange mapema na kuhuisha kwa wakati ili biashara yako ibaki steady.

Biashara bila leseni ni kama kucheza na moto. Faini ni kubwa, unaweza kufungwa, na wateja wanaweza kukupoteza. Bora ufuate hizi hatua jaza fomu, leta nyaraka, lipa ada na biashara yako itakuwa imara na salama. Hiyo ndio njia ya kutoka sokoni kwenda kwenye level ya juu bila stress za serikali.

Usipoteze muda kupanga foleni TRA au kukimbia ofisi za halmashauri mwenyewe. Mimi na timu yangu tupo tayari kukusaidia kupata leseni yako kwa haraka zaidi bila stress. Tuwasiliane sasa hivi ili tuanze mchakato na ndani ya muda mfupi uwe na leseni mkononi +255693880325
 
Back
Top Bottom