Leo yamenikuta, sirudii tena

baloz89

JF-Expert Member
Mar 26, 2015
495
250
Vipi wadau,

Kwa kipindi kirefu nimekuwa najaribu bahati yangu kuopoa kifaa toka social networks tofauti tofauti kwani wadau kibao wanasema kule ni rahisi afu unang'oa vitu tbs. Wiki iliopita si nikazama kule Ze BADOO kucheki kama kweli, sasa haikupita siku kimwana akajileta mzima mzima ila sasa picha zake ni mwendo wa pasport tu hadi Inster, whatsap ni vilevile ila usoni kama amejiumba vile yaani mkali acha tu.

Event ilikua leo tukutane na ikiwezakana na mechi ya kirafiki ipigwe.Sasa mimi nikawahi eneo la tukio ili nimcheki kama akija sio saizi yangu nijue what to do au kama chenga nimpige tobo nisepe. Kidogo anasema kafika ikabidi nichomeke vizuri jeans langu na shati mpya kabisa ili nimlaki malkia huyu mwenye uso hatari nikijua uzuri wake unasadifu na huku chini nikapiga simu wakati nimejibanza.

Mama yangu sikuyaamini macho yangu yani yule bado revolution haijakamilka yaani uku down chenga kabisa nimekimbia hadi nikasahau Alteza yangu na kupanda bodaboda. Wadau mimi kuanzia leo nimekoma bora nimtongoze mtu baada ya kumwona ila sio mtu anapiga picha za usoni tu ukakurupuka hadi sasa nimezima ile simu ya kazi maana aisee hata kama mapenzi hayachagui ila yule nitamtesa tu.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom