wikiend ilikuwa ngumu kwa rafiki yangu jamani wana mmu
Jamaa alikuwa na mchumba wake na wakati amemaliza chuo ikatokea nafasi ya usalama wa taifa na huyo dada aakapewa huo mchongo na akaenda kusoma kwa miezi kadhaa na wakiwa na mipango ya kufunga ndoa baada ya binti kurudi na walikuwa wanapendana sana.
Nyongo imeingia leo baada ya kuambiwa na wazazi wa binti kuwa taarifa walizonazo ni kuwa binti kulingana na nafasi ambayo ameandaliwa harusiwi kufunga ndoa na mtu ambaye si usalama wa taifa labda mpaka baada ya miaka sita na binti ana miaka 26 kwa sasa na mvulana ana miaka 32.
rafiki yangu amechanganyikiwa maana alimsubiri binti kwa muda mrefu na walipanga kufunga ndoa mwaka kesho 2012.
ameniomba ushauri ili kama aweze kusaka nafasi ya usalama wa taifa au aweze kumsubiri hiyo miaka 6 na kinachomuuma ni kwamba mchumba wake inabidi ajilengeshe kwa mtu yeyote ambaye ni usalama wa taifa au wamchagulie.
wana mmu huyu jamaa yuko njia panda hajui afanye nini,mpaka nimemuonea huruma.
naombeni msaada wenu wa mawazo angalau nipate kufkishia maana nimekwama!!