leo yamemkuta jamani!!!!!!!!!!

msani

JF-Expert Member
Jun 13, 2011
1,801
1,191
wikiend ilikuwa ngumu kwa rafiki yangu jamani wana mmu
Jamaa alikuwa na mchumba wake na wakati amemaliza chuo ikatokea nafasi ya usalama wa taifa na huyo dada aakapewa huo mchongo na akaenda kusoma kwa miezi kadhaa na wakiwa na mipango ya kufunga ndoa baada ya binti kurudi na walikuwa wanapendana sana.
Nyongo imeingia leo baada ya kuambiwa na wazazi wa binti kuwa taarifa walizonazo ni kuwa binti kulingana na nafasi ambayo ameandaliwa harusiwi kufunga ndoa na mtu ambaye si usalama wa taifa labda mpaka baada ya miaka sita na binti ana miaka 26 kwa sasa na mvulana ana miaka 32.
rafiki yangu amechanganyikiwa maana alimsubiri binti kwa muda mrefu na walipanga kufunga ndoa mwaka kesho 2012.
ameniomba ushauri ili kama aweze kusaka nafasi ya usalama wa taifa au aweze kumsubiri hiyo miaka 6 na kinachomuuma ni kwamba mchumba wake inabidi ajilengeshe kwa mtu yeyote ambaye ni usalama wa taifa au wamchagulie.
wana mmu huyu jamaa yuko njia panda hajui afanye nini,mpaka nimemuonea huruma.
naombeni msaada wenu wa mawazo angalau nipate kufkishia maana nimekwama!!
 
mmmh!! hiyo sijawahi sikia!! na kama ni kweli, basi jamaa ajue hana lake hapo. Kuna usalama wa taifa mwenzie tayari anamega. mpe pole sana. mwambie asipoteze muda na huyo.
 
yaani hapo ukibandika miaka 6 ijayo jamaa atakuwa na miaka 38 ndiyo anaoa. akijaaliwa mtoto ndani ya mwaka huo huo basi akifikisha miaka 60, first born wake kama hajapitiwa na kipindu pindu au 'kurogwa' atakuwa na miaka 22. Duu, jamaa hataweza hata kuona wajukuu wake huyo.

Huyo demu aachane naye hiyo ni mwanzo wa wazazi kumkata steam mshikaji. kwa nini demu mwenyewe asimuweke wazi mshikaji?
 
Atafute demu mwingine aoe fasta, kama kusubiri matokeo yake ndo hayo, basi ajue hapo hana chake
 
Asing'ang'anie kumuoa kwani iko siku ataambiwa mkewe yuko anaenda nje ya nchi kikazi kumbe ni chakula ya ****** na yupo bongo hii hii analiwa na ******
 
itakua ni gear ya kumpiga chini huyo mshkaji!hakuna kitu kama hicho!anamzingua tuu!aachane naye,sio riziki
 
Mshauri rafiki yako ajiunge usalama wa Taifa ili kuvuka hicho kizingiti...
 
Hiyo ni style ya kumpiga chini jamaa kiaina maana mimi kama Big X sijawahi sikia na marafiki kibao usalama na wake zao au waume si usalama. Nashindwa kuelewa kwann Tanzania tukisikia usalama wa taifa nywele zatusimama na ni kazi tu ya kawaida. Hawa kwa kifupi ni wambea ama kwajina la mtaa spy/snitches. Hawana uwezo wa kuarrest wala kufanya upekuzi ila ni kutoa tu taarifa. Jamaa mke kamkosa aendelee na maisha yake. Kupata uthibitisho amuulize huyo mchumba ake ushahidi wa anayoyasema kama sheria au any code. 6 yrs no way na hivi mapenzi hayana guarantee wala insurance
 
itakua ni gear ya kumpiga chini huyo mshkaji!hakuna kitu kama hicho!anamzingua tuu!aachane naye,sio riziki

mmmh!! hiyo sijawahi sikia!! na kama ni kweli, basi jamaa ajue hana lake hapo. Kuna usalama wa taifa mwenzie tayari anamega. mpe pole sana. mwambie asipoteze muda na huyo.
ndo hivyo mkuu,yaani jamaa hata nikimpigia simu swali la kwanza ni kama nimepata nafasi ya usalama wa taifa au njia ya kumnasua mchumba atoke kwenye hiyo kazi
 
itakua ni gear ya kumpiga chini huyo mshkaji!hakuna kitu kama hicho!anamzingua tuu!aachane naye,sio riziki

Ni kweli mkuu, hii ilikuwa wakati wa Usalama wa Taifa ulipokuwa Usalama wa Taifa, na wakati ule hata kuoa askari ukiwa wewe ni raia tu ilikuwa shida sana, siku hizi haya hayapo, Usalama wa Taifa wanaoa na kuolewa wanavyotaka,tunachanganayika nao mpaka tunajua wao ni nani, na ajabu wanajitambulisha hata kwenye watu kuwa wao ni nani hata bila sababu, pengine iko sababu nyingine ama wazazi wanafuata waliyosikia na ilivyokuwa zamani. Siku zile hata ndugu ama wazazi wasingejua kama mtoto wao yuko usalama wa taifa. Mwambie afuatilie ajue sababu hasa.
 
Thats pretty childish. Usalama wa taifa, so what? Kama tunajua kazi yake, kwanini iwe shida kuolewa? Ingekuwa haijulikan, sawa
 
Changa la macho hilo,achana nae huko walipokuwa kambini kakutana na msela kampiga mbupu zaidi yako so kaona wewe huna issue tena mademu wapo wngi sana tafuta mwingne homebway
 
Sasa si amwambie huyo mchumba wake amuunganishie na yeye kwenye huo mchongo wa usalama wa nini sijui ili maneno yaishe?
 
wikiend ilikuwa ngumu kwa rafiki yangu jamani wana mmu
Jamaa alikuwa na mchumba wake na wakati amemaliza chuo ikatokea nafasi ya usalama wa taifa na huyo dada aakapewa huo mchongo na akaenda kusoma kwa miezi kadhaa na wakiwa na mipango ya kufunga ndoa baada ya binti kurudi na walikuwa wanapendana sana.
Nyongo imeingia leo baada ya kuambiwa na wazazi wa binti kuwa taarifa walizonazo ni kuwa binti kulingana na nafasi ambayo ameandaliwa harusiwi kufunga ndoa na mtu ambaye si usalama wa taifa labda mpaka baada ya miaka sita na binti ana miaka 26 kwa sasa na mvulana ana miaka 32.
rafiki yangu amechanganyikiwa maana alimsubiri binti kwa muda mrefu na walipanga kufunga ndoa mwaka kesho 2012.
ameniomba ushauri ili kama aweze kusaka nafasi ya usalama wa taifa au aweze kumsubiri hiyo miaka 6 na kinachomuuma ni kwamba mchumba wake inabidi ajilengeshe kwa mtu yeyote ambaye ni usalama wa taifa au wamchagulie.
wana mmu huyu jamaa yuko njia panda hajui afanye nini,mpaka nimemuonea huruma.
naombeni msaada wenu wa mawazo angalau nipate kufkishia maana nimekwama!!

asidanganyike, hiyo habari ya miaka sita haina ukweli wowote. anatakiwa afikirie nje ya mduara. kufunga ndoa ni sehemu tu ya mapenzi. kwani nani hajui sheria za huko majeshini?? lakini mbona wana waume, wana wake, na wana watoto kabla ya muda waliowekewa?

na kwa taarifa zaidi ni kuwa hata weza pata kazi kama ya huyo binti kwa sababu yeye anafuata mwanamke na si kazi- hawata mkubalia. hapo ni huyo mama ndo anaona rafiki yako hafananiii kwahiyo ametumia kigezo cha kazi.
ushauri ninao weza kumpa
1. aongee na huyo dada kuwa wao wataishi kama mke na mume ila ofisini ndo mwanaume hatapata haki za mume. mama akizaa atapata haki za watoto kutoka ofisini. ndoa ofisini itatambulika baada ya hiyo miaka sita
2. akikataa anatakiwa kukubali hiyo hali, hili la kusema amesubiri siku nyingi halitakiwi ktk kuchukua maamuzi ya maisha. amesubri siku nyingi , lakini hajui ni siku ngapi zimebaki, na zina uzito gani ukilinganisha na hizo zilizopita
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom