Kama unachosema ni kweli basi ndugu ama una hela ya kuchezea au hauko makini kwenye maamuzi yako. Wewe namba hujui mwenyewe tena unahisi ni mchepuko wa wife halafu unatuma Tsh 50,000 eti kujaribisha???????
Ilikuwa hivi,,kuna namba nilikuta kwenye simu ya wife . haina jina, jina alikuwa amesevu kwenye line nyingine. Hatuna mipaka kwenye simu,..sasa badala nimuulize, mi nikachukua hiyo namba, nikawa najaribu kuangalia jina kwa m-mpesa...yani unafanya kama unatuma hela halafu jina linatokea ili nimjue!
Nikajaribu kutuma 50,000. Mara jina likatokea, kumbe ni shemeji yangu wa kike mdogo wake na wife...,mbaya zaidi nilishasahau kumbe kwenye akaunt ya m-pesa kulikuwa na salio,, ile hela ikaenda kweli..sasa huyu binti badala hata anipigie kampigia dadaake, "shemej kantumia hela 50000"
nifanyeje manake naona aibu hata kumwambie arudishe istoshe ni mwanafunzi wa chuo..,
Halafu wife sijui ananielewaje, manake kuanzia jana namwambia sina hela!!
Ameshanuna sasa.
Story ya kweli au kutunga? Mpesa wanakuonyesha jina kabla ya kubonyeza 1 ili kuthibitisha
Leo umetoa komenti ya maana sana.hizi mbwembwe zingine hizi? kwani ungetuma buku isingekuletea jina?
sasa nilishamwambia bi mkubwa sina hela, wakati jana tu kaniomba.
Kumbe hilo unalijua, then go tell your wife the truth and kiss her!
Elfu hamsini tu ndio kiwango chote hiko??? Kweli maisha yako tightJamani kujaribu jina ni nani ndo uweke kiwango chote hicho? Halafu jina huwa linakuja kabla hata ya kukubalikutuma! Walakini..ila pole haha
Story ya kweli au kutunga? Mpesa wanakuonyesha jina kabla ya kubonyeza 1 ili kuthibitisha
hahahaaa!!pole basiusiombe yakukute!
wakati mwingine inakuja namba tu. Jina linafuata baadae kwenye sms