Leo wivu umenicost

Leo wivu umenicost

Siku ya pili tuma hela ndogo kama elfu 5000/. Baada ya kutumua ulitakiwa kubuni njia ya kujinasua...ulitakiwa umpigie sim shemeji yako umbwambie kuna mzingo nataka uje uninunulie na nitakupa maagizo baade...utakaa siku 2-3 utabuni nini awanunulie awaletee...nafkiri hutakosa cha kumwambia mkeo kua kuna kitu nataka atuletee kwa matumizi ya nyumbani....
 
Hiyo ndiyo ada ya shule uliyoipata. Manake ungeipata bure ungeisahau. Dunia ya leo ukiwa na wivu wewe bado limbukeni wa mapenzi,
 
kwani kuna ubaya kumtumia shemeji yako hela...umeamua kumssupport na hilo ndo liwe jibu lako!
 
Hii taalifa umekosea kuitunga au ulikuwa na mpango wa kumtumia hiyo hela.maana ukituma hela voda kuna kipengele kina kwambia bonyeza moja kukubali je wewe hapo hukupaona?
Pili kwanini mkeo afute namba ya mdogo wake,mala tu akimaliza kuongea nae?,nahisi mkeo kashakushutukia baki njia kuu.
 
Loh kumbe tuko wengi jana nilikuwa nimeifunga simu yangu nilipoifungua tu msg ya mpesa ile inayosema lipa kwa kutumia Mpesa ikaingia,ila ya kuonyesha nimetumiwa pesa haikuwepo,naikahisi kuna mtu katuma pesa nikajifanya nijaribu kutuma pesa kwa wife 100,000/ kutuma ikaenda kweli kumbe jamaa fulani alikuwa amenitumia hiyo hela ilibidi nimwambie wife nimetuma pesa kimakosa, baadaye nikamwambia tugawane na mimi anirudishie hata kidogo tehetehe!
 
hahahahahahahaha umenichekesha kweli,bora umwambie ukweli kuhusu huo wivu wako,asije kufikiria anamtaka mdogo wake
 
nimependa huyo shemejio kwa kumjulisha kwanza dadake badala yako siku nyingine utaacha wivu usio na mpango lol
 
Aisee wivu hauna maana kabisa....! Sawa tu ukinicheka, lakini mi naamini kila mtu ana wivu.,..ila nilichojifunza wivu ni upuuzi mtupu, tuache!

Ilikuwa hivi,,kuna namba nilikuta kwenye simu ya wife . haina jina, jina alikuwa amesevu kwenye line nyingine. Hatuna mipaka kwenye simu,..sasa badala nimuulize, mi nikachukua hiyo namba, nikawa najaribu kuangalia jina kwa m-mpesa...yani unafanya kama unatuma hela halafu jina linatokea ili nimjue!

Nikajaribu kutuma 50,000. Mara jina likatokea, kumbe ni shemeji yangu wa kike mdogo wake na wife...,mbaya zaidi nilishasahau kumbe kwenye akaunt ya m-pesa kulikuwa na salio,, ile hela ikaenda kweli..sasa huyu binti badala hata anipigie kampigia dadaake, "shemej kantumia hela 50000"
nifanyeje manake naona aibu hata kumwambie arudishe istoshe ni mwanafunzi wa chuo..,

Halafu wife sijui ananielewaje, manake kuanzia jana namwambia sina hela!!

Ameshanuna sasa.

Pole inaonekana wewe una michepuko
 
Mambo mengine bwana, ivi kabla hujathibitisha kutuma kuna maelezo ya kuthibitisha jina la mtu unayemtumia ilikuwaje hapo?
 
mambo mengine bwana, ivi kabla hujathibitisha kutuma kuna maelezo ya kuthibitisha jina la mtu unayemtumia ilikuwaje hapo?

kwenye kuthibitisha ilikuja namba tu, then nilivyo bonyeza 'ok' ndo nikapata sms yenye jina sasa.
 
Nawe unaamini kuwa umemaliza uchunguzi wako iko kuna swali la kujiuliza hapi iweje namba mkeo asiisave na akipigiwa aifute fasta kuna mawili
1) kuna lijamaa likula mzigo kilaini lakini limesajili line kwa jina la shemeji yako
2) mdogo wa mkeo anashirikiana kumchepusha dadaake.
WAJINGA NDO WALIWAO

wewe na mwenzio hapo juu mnajibu kabla ya kelewa, ni hivi mkewe ana simu mbili sasa hiyo namba ya mdogo wake ameisave kwenye hiyo simu nyingine, kwahyo kwenye hii simu nyingine hajaisave, hata mimi nina simu mbili sijasave namba zote kwenye simu zangu zote
 
Basi hali imekwisha tokea
Mwambie mkeo umemtumia shemeji pesa kidogo kwasababu umemkumbuka na unahisi maisha ya chuo ni magumu nyie mtajipinda mtapata nyingine! huku unamtania tania mkuu
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom