LEO TUKO HAPA PUB a.k.a JF Arena

Bujibuji Simba Nyamaume

JF-Expert Member
Feb 4, 2009
75,227
157,425
Enzi hizo Mtambuzi alikuwa na kazi ya pekee sana kuwaunganisha wana JF Wa Dar-es-Salaam pamoja akiandaa mikusanyiko ya members akianzia na ile ya Kebby's kisha muendelezo Leo Tuko Hapa Pub.
Mikusanyiko hii iliweza kunikutanisha Ana kwa Ana na Maxence Melo, Mtambuzi mwenyewe a.k a Baba Ngina, Mwita Maranya, Zion Daughter, ladyfurahia, Madame B, Paloma a.k.a Wa Mtaroni, Kipaji Halisi, Asprin a.k.a Babu, KakaKiiza, Arushaone na wengine wengi.
Kwenye kusanyiko hili mengi yalijadiliwa. Miongoni mwa mijadala ilikuwa ni:-
√ Kuhamasishana kuchangia JF
√Mijadala ya kisiasa
√Biashara na deals mbalimbali
√ Wengine wakapata wenzi

Kwa ufupi ilikuwa raha sana, na tulifundishana mengi sana.
Members Wa Leo Tuko Hapa hebu njooni tukumbushane enzi zile
 
Lakini kukutana kunajenga aibu ya kuchangia mada...thats my observation!
Leo hii ukikutana na Jingalao utaanza kueneza umbea kwamba Jingalao ni mlevi mara hivi mara vile!!
Wengi wa waliokutana wamebadili IDs.


Niliowahi kukutana nao wakiona michango yangu leo hiiwanaweza nivamia nyumbani!

Labda kuwe na mfumo wa kukutana bila kubreach IDs
 
Hadi nikampa jina la utani mtoto wangu akaitwa BUJIBUJI Baada ya wife kukubali posts zako!
 
ilikua inapendeza sana asee,naona toka watu wahamie whatsapp group,huku wadau wachache sana@Bujibuji
 
Mmi mwenyewe nilifurahia sana hasa kukutana na Kipaji Halisi nilidhani kuwa ni mtu wa jeshini yaani ni GP fulani viile kumbe ni
kijana mbichi sana mwenye bashasha la furaha wakati wote hata ukimuudhi yeye anacheka sana yaani nilienjoy kweli

wengine walikuwa watu wa aibu sana hasa nilipomkuta mentor yeye mpaka alikuwa anasikia njaa lakini akutaka kuniambia mm badala yake
akamwambia paloma aisee nilisikia kucheka sana siku hile mweeee jamani mambo haya mkikutana raha sana ila siku hizi watu wapo whatssapp kwani utawaona huku wamehama mji wako washington smart hahahahahaaaaaaaaaaa
 
Back
Top Bottom