Leo tarehe 9 September Apple wamezindua iPhone 17 series na accessories nyingine!

Leo tarehe 9 September Apple wamezindua iPhone 17 series na accessories nyingine!

Mad Max

JF-Expert Member
Joined
Oct 21, 2010
Posts
31,139
Reaction score
88,800
Wakuu, leo September 9 Apple wamezindua simu zao mpya iPhone 17 series pamoja na bidhaa nyingine kama airpods na Apple watch matoleo mapya.

IMG_4984.jpeg
Kwa kuanza na iPhone, jumla ya simu nne zimezinduliwa na CEO wao Tim Cook. Simu tajwa ni iPhone 17, iPhone Air, iPhone 17 Pro na iPhone 17 Pro Max.

iPhone 17 (Base)
iPhone 17 ambayo ndio base model ina cha kioo cha 6.3 inch, Apple A19 chipset, 8GB RAM na storage ya 128/256/512GB.

IMG_4975.jpeg
Kwenye camera ipo na 48MP main camera na 48MP ultrawide lenses na selfie 18MP. Battery lililopo ni 3,600mAh. Pia iPhone wamesema base mode itaanza kwa $900 na utachagua rangi Black, White, Lime, au Red.

IMG_4976.jpeg
Kwahiyo ukifananisha na iPhone 16 ya mwaka jana, tuna camera mpya, kioo kimeongezeka kidogo, chip mpya, battery kidogo kubwa ila ila muonekano karibia sawa.

iPhone Air

IMG_4974.jpeg
Hii ni ingizo jipya katika iPhone series. Ipo na specs karibia zote kama za base iPhone 17 mfano A19 Pro chip, 8GB RAM, ila ina camera moja ya 48MP, na 18MP selfie, kioo kikubwa zaidi cha inch 6.5 Super Retina OLED ikiwa na refreshrate ya 120Hz.

IMG_4982.jpeg
Hii simu ni nyembamba sana just 5.6 mm na battery limepungua sana hadi 2,800mAh lengo kuu ikiwa ni kuifanya iwe nyembamba sana. Na pia itakua e-SIM model tu.

IMG_4980.png
Pamoja na vyote, iPhone 17 Air inauzwa kuanzia $1,000 na rangi zitakua kama kwenye 17 base.

iPhone 17 Pro

Kipenzi cha wengi ni Pro na Pro Max. Hawa maarufu kama macho matatu watakua na camera za nyuma tatu, mbili kama za kwenye base 48MP main na 48MP Ultrawide, sasa ya tatu ni 48MP telephoto lens.

IMG_4981.png
Tukianza na huyu iPhone 17 Pro, ina kioo cha 6.3 inch kama base, pia imepewa chip mpya A19 Pro kama wenzie, 12GB RAM na storage inaanzia 128GB hadi 1TB na huku ikiwa na battery la 3700mAh.

IMG_4985.png
Kuhusu rangi, zilizopo ni White, Black, Blue, na Gold, na bei ni kuanzia $1,110.

iPhone 17 Pro Max

Bwana mkubwa Pro Max ana kioo cha 6.9 inch, A19 Pro chip, 12GB RAM na storage itaanzia 256GB hadi 1TB na battery la 5,000mAh.

IMG_4983.png
Rangi zitakua kama kwenye Pro ila bei itaanzia $1,397 tu.

Airpods Pro 3

Kama wewe ni mdau wa EarPods, basi tutakubaliana hamna inayozido Airpods Pro likija kwenye swala la music, calls na noise cancellation.

IMG_4979.jpeg
Sasa Apple wamezindua pia leo Pro 3, ikiwa ni zaidi ya miaka mitatu toka wazindue Pro 2 wanavyotoa iPhone 14.

IMG_4989.jpeg
Pro 3 inakuja na chip mpya ya H3, pia ina health sensors kwaajili ya kupima mapigo ya moyo na joto. Pia Pro 3 imepewa live translation ability kwaajili ya kuwasiliana na mtu ambae mnaongea lugha tofauti.

Apple Watches

Apple hawajaishia kuzindua simu na EarPods tu, wamezindua pia smartwatches zao.

IMG_4978.jpeg
Jumla ya saa tatu zimezinduliwa, Apple Watch Series 11, Ultra 3 na wameongeza kitu kipya Watch SE 3.

Series 11 haijabadirika sana kutoka series 10 ya mwaka jana, ila imeongezewa blood pressure detection.

Ultra 3 imekuja muda muafaka, ukichukulia mwaka jana hawakuleta Ultra mpya. Imeongezwa 5G connectivity na sasa ina support satellite messaging.

IMG_4986.jpeg
Model ya Watch SE 3 ni cheap version ya series 11.

IMG_4987.jpeg
SE itauzwa kuanzia $ 249, Series 11 $399 na Ultra 3 $799.
 
Fold 7 ni 1,999 base version. iPhone always huwa hawatoi most expensive flagship wala hawatoi features revolutionary na immature za kupandisha bei.
Sawa, swali hao wanaomiliki hizo Samsung nao wanaumiza sehemu za miili yao?
Maana hakuna utofauti wa gharama lakini nashangaa watumiaji wa iPhone kuambiwa wanaumizwa.!!
 
Back
Top Bottom